The Official Azam FC Thread

The Official Azam FC Thread

Patashika nguo kuchanika leo uwanja wa taifa Yanga vs Mbeya City, anayeshinda anakaa juu ya mwenzake, Je Mbeya City atakubali kuvunja rekodi yake ya kutofungwa tangia ligi ianze? Je Yanga atathibitisha kuwa sare waliyoipata uwanja wa Sokoine ilikuwa ya kuonewa? Mbeya City waliweka kambi Pemba na Mwakaleli. Yanga wao Uturuki na Bagamoyo... naambiwa itakuwa ni vita kati ya Bagamoyo na Mwakaleli (usiniulize namaanisha nini) kule Chamazi Azam FC itaendelea kuchanua mbele ya Kagera Sugar? usikae mbali na Luninga yako kuanzia saa kumi jioni mechi zote mbili Live on Azam One & Two
 
Ni muda wa mapumziko kipindi cha kwanza kikiwa kimemalizika kwa Azam kuongoza kwa bao 1 dhidi ya Kagera Sugar.Umony akiwa kinara kwa kuipatia Azam goli la kwanza ndani ya dakika ya 10 kipindi cha kwanza
 
Azam tunaongoza tatu bila jamani..Kombe letu hili wakuu.

"Nlikuwepo":bolt:
 
11_0.jpg

REKODI tatu za klabu na ligi zilivunjwa jana jioni, Azam FC ilivunja rekodi yake ya ushindi mnono baada ya kufungamagoli manne katika mechi moja, idadi hiyo ya magoli ikiwa ni kubwa zaidi msimu huu.
AZam FC ikajiongezea rekodi ya pili ya kushinda mechi muhimu tena ikishinda kwa idadi kubwa ya magoli dhidi yatimu ngumu ya Kagera Sugar. Rekodi ya klbu ya Azam FC tangia kuanzishwa kwake inaonesha kuwa haijawahi kuwana uwezo wa kushinda mechi inapotakiwa kushinda kwa udi na uvumba ili ikae kileleni.
Mara ya mwisho ilikuwa ni mechi ya kumaliza raundi ya kwanza ambapo ikiwa nyumbani Azam FC ilipaswa kuifunga Mbeya City ili imalize raundi ya kwanza ikiwa inaongoza lakini ikajikuta ikipata sare ya 3-3.
Rekodi nyingine ambayo ni ya kuvutia zaidi ni ile ya kufikisha mechi ya 16 bila kufungwa. Azam FC imecheza michezo 16, imeshinda michezo 10 na kutoka sare michezo 6 huku ikiwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja hadi hivi sasa.
Katika mchezo wa jana jioni Brian Umony alitakata baada ya kufunga magoli mawili ya awali katika dakika za tisa na 52 huku kinda la miaka 18 Kevin Friday aliyeingia kuchukua nafasi ya Joseph Kimwaga aliyeumia akifunga goli la tatu na Jabir Azizi Stima akikamilisha karamu ya magoli.
Azam FC jana ilikuwa ikicheza mchezo wake wa tatu mkwenye ligi bili kuruhusu nyavu zake kutikisika. Huo ulikuwa ni mchezo wa 12 kwa kocha Marius Joseph Omog bila kuruhusu nyavu zake kuguswa kati ya michezo 13. Aliruhusu kufungwa goli tatu na KCC ya Kampala Uganda Pekee.
Azam FC sasa inajiandaa na mchezo wa kimataifa kukwaana na Club De Ferroviario da Beira mechi itakayochezwa jumapili tarehe 9 February 2014 Chamazi Stadium
 
Ahsante Mkuu kwakuziweka kumbukumbu vizuri. Huu ni mwaka wetu wana Azam, Yanga na Simba wanatusindikiza tu.
 
kina makoye wakisikia hivi wanaumia kweli wakati ukweli ndio huu..
 
mpaka dk ya sasa hivi azam yupo nyuma kwa goli moja nyuma..
 
ft ferro 2 - 0 azam
agg 2 - 1
niuzembe wetu hapa kushinda nyumba goli moja ili hali hujui huko uendako..

tutaonana msimu ujao...
 
Back
Top Bottom