Hoja hujibiwa kwa hoja!
Mnadai hoja nzito, haya ngoja niwanyang'anye tonge mdomoni! Mnaweza kuwaandikia wengine hoja dhaifu kama hizi wakaziamini, bahati mbaya madai yangu kuwa mimi ni "mchambuzi niliyebobea katika masuala ya siasa na jamii" siyo ya bure!! Naweza kuona uongo wa hoja hata kama zipambwe kwa maneno mazuri maili mia moja kabla hazijanifikia!
Sikiliza Mwanakijiji,
Watu corrupt wako pote kwenye CCM na kwenye upinzani. Hata nje ya taasisi hizo, wamo. Hoja hapa ni kwamba si corruption yao inayowapeleka kwenye upinzani.
umesema vizuri kuwa watu corrupt wako pote "kwenye CCM na kwenye Upinzani" halafu unajichanganya unaposema walioko kwenye upinzani "siyo corruption inayowapeleka" kule! Sasa corruption kwenye upinzani imefikaje? Kama wanaoingia CCM wana "Hulka" ya corruption ndio maana wako kwenye CCM, wale watu corrupt walioko upinzani "hulka" yao ni nini? Kitu hakiwezi kuwa na kutokuwa kwa wakati mmoja kikihusisha kitu kilele kizima siyo kama sehemu ya kitu ( It is impossible for a thing to be or not to be concerning the same thing as a whole not as a part!) Kama kuna watu corrupt kwenye CCM na hivyo kufanya CCM kuwa corrupt, basi kama kuna watu corrupt kwenye upinzani, basi kunafanya upinzani kuwa corrupt!
Lakini hulka hiyo hiyo ndiyo inayowapeleka CCM, kwa sababu there is something to reap within CCM! Upinzani hauna cha kuvuna, unahitaji kujengwa.
Upinzani hauna cha kuvuna? are you kidding me? Unachotaka kutuambia ni kuwa walioko upinzani ni malaika wasiovutiwa na pesa, sifa, ukubwa, na heshima! Unataka kutuambia kuwa walioko CCM ndio binadamu pekee ambao wanapenda ujiko na ruzuku za chama! Unataka kutuambia kuwa wapinzani wote (hata wale corrupt) wakipewa msosi wa nguvu watakataa! Ushahidi unao wewe mwenyewe. Kama baadhi ya viongozi wa upinzani na wanachama waliweza kurubuniwa na kununuliwa na CCM hadi kuhamia CCM, je watu hao walikuwa hawana hulka ya corruption walipokuwa upinzani au hulka hiyo waliipata walipojiunga na CCM! Kama viongozi wa CCM wanaweza kununuliwa na watu wenye maslahi fulani wakanunulika na tukawaita wako wafisadi, kwanini wale wa upinzani wanaonunulika wasiitwe wafisadi pia? Kama baadhi ya viongozi wa CCM wako corrupt na hivyo kufanya CCM kuwa chama kibovu, kwanini viongozi corrupt walioko upinzani wasifanye upinzani kuwa mbovu? This is an extreme example of double standard!!
Tena ni bahati nzuri kwamba watu sasa wamefikia kutumia resources zao kujenga upinzani. Wasioona mbali wanawacheka. Ikumbukwe TANU ilijengwa hivyo. Kuna watu walitoa pesa zao kuunga mkono harakati za kuleta mageuzi na mabadiliko ya kimfumo.
Kwa maoni yako ni sawa kwa wapinzani kutumia resource zao kujenga upinzani, na ni sawa waasisi wa TANU kutumia mali zao kujenga chama chao, lakini leo ni dhambi kwa wapenzi na mashabiki wa CCM kutumia mali zao kujenga chama chao! Hili haliingii akilini hata chembe. Kama Mbowe na wenzake wanaweza kutumia majina yao, mali zao kujenga CHADEMA ni dhambi gani kwa Rostam Azizi, na matajiri wengine ambao ni mashabiki wa CCM kutumia mali zao kujenga chama chao! Ni sawa kwa wapinzani kufanya hivyo (wanapewa sifa ya kujitolea) lakini ni vibaya kwa wanaccm kufanya hivyo (wanabezwa)?
Jitihada hizo zimekufa baada ya TANU kukamata serikali na kuzaa CCM, ambayo sasa inatumia kodi ya watanzania kufanya mambo yasiyo na maslahi kwa Watanzania.
Hili hata sitaki kulielezea kwa kina. Hakuna kitu kibaya katika kujenga hoja kama "haste generalization". Madai kuwa CCM inatumia "kodi ya watanzania, kufanya mambo yasiyo na maslahi" yamezidishwa! Ubadhirifu wa mali za umma upo na mimi wa kwanza kukemea, viongozi wabaya wapo majina nimeyataja, viongozi wasio na uwezo wa kuongoza wanajulikana! Lakini kusema kuwa CCM kupitia serikali yake inafanya mambo yasiyo na maslahi kwa Watanzania kwa kutumia kodi zao ni tusi ambalo kila Mtanzania asilikubali! Je wamefanya yote ambayo tungependa wafanye? la hasha! (mifano ya mabadiliko ya Katiba, utekelezaji wa tume wa ya Warioba na ile ya Jaji Kisanga inanijia); Je wamefanya jinsi ile tungependa wafanye? hata kidogo!(mifano ya mikataba mibovu ya nishati na madini ni dhahiri) Je kuna mambo ambayo wameyafanya yenye maslahi kwa watanzania!! jibu ni NDIYO!! (nitajaza vitabu kuanza kuorodhesha). Hili tendo la kudharau na kukebehi mafaniko na mambo mazuri yaliyofanywa na CCM kuliwagharimu wapinzani!! Mwenye macho haambiwi "tazama"!
Huwezi kwenda kijijini na kuwaambia wananchi CCM haijafanya lolote wakati wanaona barabara ya lami! Huwezi kuwaambia CCM haijafanya lolote wakati wanaona shule zinajengwa, visima vinachimbwa, kliniki zinakarabatiwa!! Endeleeni kudai CCM haijafanya lolote muone kama watu watawachagua!
Tunahitaji kufikiri kama watu wa kizazi tofauti. Upinzani wa leo hauwezi kujengwa kwa kufuatafuata maagizo ya CCM na staili yao ya kufanya siasa. Wakati umefika, sasa yanahitajika mapinduzi ya lazima katika fikra zetu, ili kuathiri mwenendo wetu na utendaji wetu katika masuala ya kisiasa.
Tunajaribu kuwasaidia kuwapa "mapinduzi ya fikra" lakini nyinyi wagumu! Mnafikiri kila mtu anayekosoa upinzani basi ni mwana CCM au hautakii mema upinzani! kalaghabao! Wakati mwingine huna budi kuiga mbinu za mpinzani wako. Jifunzeni siasa za nchi nyingine muone ni jinsi gani kutumia mbinu za ushindi za chama tawala zaweza kuwapeleka madarakani! Unafikiri Bill Clinton aliingia madarakani bila kuiga mbinu za chama cha Republican? Nenda wikipedia na tafuta "triangulation politics" utajua nina maana gani!
CCM sasa kimekuwa kichaka ambamo kina anayetaka kula kwa mikono miwili bila kunawa anajiunga nacho, maana ndiyo maficho. Vijana waadilifu hawendi huko siku hizi. Ukiona mtu ambaye hakuzaliwa CCM, na ni msomi, anatamani kujiunga CCM, ujue kuna mawili. Ama usomi wake haujamwezesha kuijua CCM, au naye anatamani kufanya yale wanayofanya hao tunaowasema - mabovu.
Au ameona udhaifu wa upinzani na ameona mahali pekee anakoweza kwenda kuleta mabadiliko ni CCM. Ulimwengu hauna mambo mawili tu ya kuchagua. That is one of the oldest fallacies in the book - you only have two choices! "Kusuka au Kunyoa". no you don't. Labda nataka nizichane tu!
CCM hapa ilipofikia, pa kuongozwa na wasanii wasio na vision, kina JK na EL, wanaojiita wajamaa huku wakiishi ubepari, wanaofadhiliwa na wahindi na waarabu wanaozengea mikataba na migodi minono - rejea suala la Patel na Mchuchuma - CCM inayoongozwa na Makamba...ujue sasa tumefika mahali nchi imo mikononi mwa wajinga! The country has gone to the dogs!
Fanyeni hima mje kututoa utumwani enyi manabii wa ahadi!! Wapinzani wanaofadhiliwa na Wamarekani, Waingereza, na Wajerumani ni bora kuliko CCM inayofadhiliwa na Wahindi na Waarabu! Kama kufadhiliwa na watu wasio weusi ni kosa, Chadema wawe wa kwanza kutupia CCM mawe!
Watu wenye uchungu na nchi yao wanapaswa kujua hilo na kuchukua hatua kuwaimarisha wapambanaji katika opposition, si kuwapiga mawe. Kila element nzuri inayochomoza kwenye opposition inafaa itumike kujenga hatima ya taifa letu...
Tunajaribu kuwaimarisha lakini nyinyi mnafikiri tunawatakia mabaya!!
Wakati unakaribia kwa ufalme wa CCM kung'oka. Historia inaonyesha kuwa falme zote duniani zilivuma, lakini ilifika mahali zikaanguka kwa sababu kama hizi ninazoziona ndani ya CCM. Wasiokubaliana na mtazamo huu, waendelee kuamini watakavyo. Siku ukweli ukidhihirika tutaambizana na kukumbiushana haya. Lazima tuangalie mbali ya pua zetu, kama kweli tunataka kujiita wachambuzi.
yeah right! CCM ing'oke kisa Chadema, CUF, TLP jinsi zilivyosasa!! Endeleeni kutamani nchi ya ahadi!
Unajua Mwanakijiji wewe unapotea sasa . U CCM wako unakutoa maana sana ndugu . Watu wamegundua hili na ndiyo watu wamehama radio yako wanaishia Radio Butiama .
Dues na Radio Butiama naziunga mkono kwa nguvu zote! Wala usidhani linanitia wivu au linanifanya nishtuke. You have no idea how petty that sound! Kusikiliza maoni ya upande mmoja peke yake ni ufinyu wa kisiasa!
Halafu mmeng'ang'ania miye CCM! Niwaambie mara ngapi mimi si mwanachama wa chama hicho! Lakini ukinipa uchaguzi wa vyama upinzani, CCM au mambo mengine pamoja na udhaifu wote! I'll still pick CCM! mamilioni wengine wanakubaliana nami!