Karibu tena Muh.Mbowe huku tulikuwa tuna subiri wewe useme kwa mdomo wako kwamba uliibiwa kura 2005 kwa sababu ulikaa kimya sana hatukukuelewa kama ulikubaliana na matokeo au vipi,
Unachosema kinafanana kutokana na mazoea ya chama tawala CCM kuwa na mchezo kama huo, na jinsi wengi mitaani kusema nilimpigia Mbowe katika kundi la watu kumi sita wanasema nilimpigia Muh. Mbowe sasa tufanyeje na limeshapita?
Na mshindi kasha patikana na matokeo ndiyo hayo. ok tuingie ndani kidogo atakama kinauma simnajua ukweli unamachungu yake, usemi wa Muh.Mbowe unaukweli ndani yake,ujumbe ulishafika kwa wapiga kura CCM kitaongoza daima.
Itatumika njia yeyote ile CCM ishinde natumaini wengi mnakumbuka 1995 NCCR Muh. A,MREMA mchezo uliyochezwa, kwanini Mbowe asichezewe ''same game'' na uwezo upo mitandao wanayo,
katika mikutano ya Mbowe haikutofautiana na ya JK tofauti yake ilikuwa kitu kidogo sana walitofautiana asilimia 10% ya mikusanyiko ya watu. na siyo kwamba watu walikuwa wanafuata ndege ''HELIKOPTA'' la asha '' kama ilikuwa hivyo leo siyo siku ya kampeni hao watu bado wana fuata NDEGE au ni sera za CHADEMA, JK anamvuto kwa watu kama vile Mbowe alivyo, kila mahali Mbowe atapita anamikusanyiko ya raia kama JK.
Sasa kilichotokea kilicho kuwanyima CCM usingizi presha kuanguka kwenye majukwaa ni nini?CHADEMA na mvuto aliyonayo mwenyekiti wa chama hicho na sera zake. jamani tumechoka ugali tule basi mihogo tuangalie kama inatesti vizuri .
Hatuwezi kujua CCM wanafanyakazi kama hakuna kujuta watanzania, chama kipya unaweza kukikemea lakini chama cha zamani uwezi. tuwe na misimu ya uongozi kama nchi zingine kuwe na ushindani wa maendeleo kwamba CCM walifanya nini miaka 45 iliyopita na CHADEMA watafanya nini miaka mitano ijao.
habari za ndani kabisa 80% ya ushindi wa kura ni wa vyama vyote alivyo visajili TENDWA haiwezekani chama kimoja kushinda kwa asilimia kubwa hivyo tanakataa.
kura alizopata Muh.Mbowe ni tofauti ya JK na Mbowe piga hesabu utapata jibu nitaota maelezo zaidi baadaye na ushaidi kamili hapa hapa JFna sauti za kamati ya kumaliza upinzani, ni wakina nani
stay tune hizo ndizo habari za kuaminika njia ya kumaliza upimzani kwa kutumia vyombo vya habari lakini kwa sauti za walio wengi watanzania kila kitu kina mwisho,
Tulifuraia sana JK kushinnda lakini yeye ndiye kafungua njia ya chama kingine kushinda chaguzi zijazo, nina nukuu maneno ya Muh.Mbowe karibu sikiliza....
MBOWE NILIIBIWA KURA 2005
NA SULEMANI ABEID
Shinyanga
Jumanne 2.1.2007
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)bado kina endelea kukubwa na mizimu ya matokeo ya uchanguzi mkuu uliopita ambapo sasa kinadai hakikushindwa uchaguzi huo bali kura ziliibiwa.
hali hiyo ilielezwa juzi na mwenyekiti ya chama hicho na Bw.Freeman Mbowe alipokuwa akiutubia wakazi wa mji huu,katika mkutano wa hazara uliyofanyika katika uwanja wa kambarage mjini hapa
Bw.Mbowe alisema matokeo yalio tangazwa na mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi nchini. jaji Lewis Makame yalikuwa ni yake na si ya wananchi walivyo amua katika masanduku ya kura.
Wananchi, mimi ninaamini kura katika uchaguzi wa urais zilitosha lakini hazikutangazwa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi jaji makame,alizo tangaza zilikuwa zakwake hata za mgombea wetu wa ubunge zilitosha lakini ziliibiwa mungu yupo tutakutana nazo haera alieleza Bw.Mbowe.
pamoja na hali hiyo mwenyekiti huyo aliwashukuru wananchi wa mkoa wa shinyanga walivyo kionga mkono chama chake katika uchaguzi huo,kwa kuwa na subira ,uvumilivu na kuwezesha uchaguzi kufanyika kwa amani na utulivu.
hata hivyo alisema kwa pamoja na kwamba CCM hivi sasa ni chama tawala,ni vizuri wananchi wakaelewa chama hicho kina wenyewe na sio chao.
Ndugu zangu hapana ...... muelewa ,kuwa pamoja na na kwamba chama hicho CCM ndiyo inatawala nchi hivi sasa ,lakini chama hicho sio chenu kina wenywe nyiye mnatawaliwa tu hata kama ni wa CCM.
Wenye CCM wako Dar es salaam kule OSYTERBAY,MBEZI BEACH, NA MASAKI alieleza Bw.Mbowe
Aidha mwenyekiti huyo alisema hawezi kumuombea mabaya rais JAKAYA KIKWETE katika utawala wake.kwani anaamini akifanya hivyo atakuwa anawaumiza wananchi wa nchi hii.
Aslisema kinacho takiwa sasa ni wananchi kuwakaba koo viongozi wote waserikali kuona kuwa wanatekeleza ahadi walizohahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu ,
Akizungumza tatizo la wanachama wa vyama vya upinzani kurudi CCM ,alisema hali hiyo ina sababishwa na uoga wa chama tawala kwa vile hakijiamini katika utawala wake.
kama kweli mgombea wa CCM alipata asilimiA 80% ya kura zote zilizopigwa sasa uoga wa nini kukimbilia kununua wapinzani,hawataki tume huru ya uchaguzi,wanatumia mabavu katika uchaguzi.yote ya nini kama wananchi wana wapenda ,alihoji.
Aidha alishanganzwa na katibu mkuu wa CCM bW.YUSUFU MAKAMBA kuwashawishi wapinzani na kuwanunua ,na kwamba wanafanya kazi burekwa vile wapi nzani wanao wanunua ni wazeena upinzani hupata damu mpya kila siku. tu mefungua tawi katika mitandao tofauti katika internet tuna wafikia vijana kwa urahisi kutoa hoja za msingi,tembelea
www.jamboforums.com. alisema
CHADEMA tunapenda kumueleza Bw.Makamba asipoteze muda kununua wapinzani,wapinzani wapya wanazaliwa kila siku tena vijana,anaonunua ni wazee wamesha choka alieleza na kushangiliwa na wananchi.
Mwenyekiti huyo alikuwa mkoani hapa katika ziara ya siku moja akiwa na madhumuni ya kuwashukuru wananichi kwa kukiunga mkono chamachake katika uchaguzi ulioapita ambapo juzi aliutubia mikutano mitatu katika mji wa kahama .shinyanga mjini,na kishapu
.