The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

Okay, so Mbowe yuko Moshi, anafanya degree mbili, ametoa misaada etc etc. etc
What the hell does it have to do with Christianity or tribalism? jeeez! aren't we mentally mature?



Imagine Libumba angetoa msaada msikitini hali ingekuwaje? upande wangu sioni kama kuna tatizo lakini nadhani hili la dini wanasiasa wangeliacha liwe tuuu kwa sababu kesho kuna wasio na dini watasema wanabaguliwa
 
Philimon mikael.
mwenye akili za kuku unamjua alitakiwa awe shule muda huu ametoroka yuko Moshi.
nimewasiliana na university registrar on +441482465136 kasema undergraduate wote wanatakiwa wawe shule.

Nilisoma stori ya Mbowe akiwa Moshi. Nikashtuka na kuanza kufuatilia. Baadaye niligundua mwandishi alimnukuu Mh. Grace Kiwelu ambaye alimwakilisha Mh; Mbowe katika hafla hiyo. Mwandishi wa stori, katika kuandika, hakueleza kwamba Mbowe aliwakilishwa. Waandishi wetu nao!

Uchunguzi zaidi umeonyesha kwamba Hull wamefunga chuo Desembe 15. 2006. Mbowe aliondoka tarehe 16. Nilikutana naye London akiwa njiani kuelekea Dar es Salaam. Alalal usiku mmoja na kupanda ndege ya Emirates kupitia Dubai Jumapili 18. Aliwasili Dar es Salaam jana Desemba 19, kupitia Dubai.

Nilimuuliza swali hilo la utoro, nikasema 'mbonaunatuchanganya?' ndipo akanijibu kwamba naye alisoma kwenye mtandao, lakini ukweli ni kwamba alikuwa na mawasiliano na huko Moshi, kwani alikuwa amealikwa awe mgeni rasmi, lakini kwa sababu ya shule alimtuma Kiwelu amwakilishe.

Nilijitambulisha kwake na kusema mimi ndiye naitwa Kichwamaji katika Jambo Forum; akacheka sana, na kusema "kumbe ni wewe? Sasa mbona unaficha jina lako?" Nami nikacheka, na kueleza kuwa huo ni utamaduni nilioukuta kwenye forum hiyo.

Nikamhoji pia mbona amesoma uzeeni, akacheka na kusema elimu haina uzee, na kwamba yeye hatafuti tu cheti au digrii ya karatasi, na kwamba kama angependa angezipata kama hao wengine, na kwamba anachotafuta yeye ni ELIMU na UJUZI unaoendana na dunia ya sasa, na utakaomfaa katika kazi zake za siasa na biashara, nan akasema ndiyo maana ameamua kufanya fulltime programme yenye mchanganyiko wa masomo muhimu (hakuyataja).

Nikamhoji mbona ameingia mitini kwenye mtandao; akasema alikuwa amebanwa na assignments kiasi alikuwa hawezi hata kusoma.

Akasema ameshaona baadhi ya kejeli anazorushiwa kwenye forum, na kwamba atakapojiweka sawa atatoa majibu; na kwamba sasa anakwenda Tanzania kufanya siasa kidogo. Sikuhoji mambo binafsi yanayorushwa kwenye forum...Nilimwachia ayasome mwenyewe ajibu.

Kwa hiyo Mbowe hakutoroka. Kama nisingekutana naye London, nami ningekuwa nimeingia kwenye mkumbo wa wa kujadili utoro wake bila utafiti..nadhani tunahitaji kutafiti si kujadili mambo juu juu kwa kusoma hapa na pale.
 
Naelewa fika umuhimu wa swali alilouliza Mheshimiwa Mbowe kuhusu wachangiaji kuficha majina yao. Nilishawahi kuuliza hilo swali zaidi ya mara moja.

Kwa sasa, nakubali kwamba kuna watu inabidi wasitumie majina yao. Kwa mfano, inawezekana JK au Malecela ni wachangiaji humu. Haiwezekani waingie na majina yao ya kweli.

Hata hivyo, tuko wengine tunaficha majina kwa sababu za woga tu. Tunaishi bado kwenye miaka ya 60 - 85 ambapo Watanzania walikuwa wakiongea kwa kunong'oneza. Kulikuwa na sababu ya kufanya hivyo. Kuna watu walishakamatwa na kutishwa sana kutokana na maoni yao.

Augustine Moshi
 
Karibu tena Muh.Mbowe huku tulikuwa tuna subiri wewe useme kwa mdomo wako kwamba uliibiwa kura 2005 kwa sababu ulikaa kimya sana hatukukuelewa kama ulikubaliana na matokeo au vipi,

Unachosema kinafanana kutokana na mazoea ya chama tawala CCM kuwa na mchezo kama huo, na jinsi wengi mitaani kusema nilimpigia Mbowe katika kundi la watu kumi sita wanasema nilimpigia Muh. Mbowe sasa tufanyeje na limeshapita?

Na mshindi kasha patikana na matokeo ndiyo hayo. ok tuingie ndani kidogo atakama kinauma simnajua ukweli unamachungu yake, usemi wa Muh.Mbowe unaukweli ndani yake,ujumbe ulishafika kwa wapiga kura CCM kitaongoza daima.

Itatumika njia yeyote ile CCM ishinde natumaini wengi mnakumbuka 1995 NCCR Muh. A,MREMA mchezo uliyochezwa, kwanini Mbowe asichezewe ''same game'' na uwezo upo mitandao wanayo,

katika mikutano ya Mbowe haikutofautiana na ya JK tofauti yake ilikuwa kitu kidogo sana walitofautiana asilimia 10% ya mikusanyiko ya watu. na siyo kwamba watu walikuwa wanafuata ndege ''HELIKOPTA'' la asha '' kama ilikuwa hivyo leo siyo siku ya kampeni hao watu bado wana fuata NDEGE au ni sera za CHADEMA, JK anamvuto kwa watu kama vile Mbowe alivyo, kila mahali Mbowe atapita anamikusanyiko ya raia kama JK.

Sasa kilichotokea kilicho kuwanyima CCM usingizi presha kuanguka kwenye majukwaa ni nini?CHADEMA na mvuto aliyonayo mwenyekiti wa chama hicho na sera zake. jamani tumechoka ugali tule basi mihogo tuangalie kama inatesti vizuri .

Hatuwezi kujua CCM wanafanyakazi kama hakuna kujuta watanzania, chama kipya unaweza kukikemea lakini chama cha zamani uwezi. tuwe na misimu ya uongozi kama nchi zingine kuwe na ushindani wa maendeleo kwamba CCM walifanya nini miaka 45 iliyopita na CHADEMA watafanya nini miaka mitano ijao.

habari za ndani kabisa 80% ya ushindi wa kura ni wa vyama vyote alivyo visajili TENDWA haiwezekani chama kimoja kushinda kwa asilimia kubwa hivyo tanakataa. kura alizopata Muh.Mbowe ni tofauti ya JK na Mbowe piga hesabu utapata jibu nitaota maelezo zaidi baadaye na ushaidi kamili hapa hapa JFna sauti za kamati ya kumaliza upinzani, ni wakina nani stay tune hizo ndizo habari za kuaminika njia ya kumaliza upimzani kwa kutumia vyombo vya habari lakini kwa sauti za walio wengi watanzania kila kitu kina mwisho,

Tulifuraia sana JK kushinnda lakini yeye ndiye kafungua njia ya chama kingine kushinda chaguzi zijazo, nina nukuu maneno ya Muh.Mbowe karibu sikiliza....

MBOWE NILIIBIWA KURA 2005

NA SULEMANI ABEID Shinyanga
Jumanne 2.1.2007


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)bado kina endelea kukubwa na mizimu ya matokeo ya uchanguzi mkuu uliopita ambapo sasa kinadai hakikushindwa uchaguzi huo bali kura ziliibiwa.

hali hiyo ilielezwa juzi na mwenyekiti ya chama hicho na Bw.Freeman Mbowe alipokuwa akiutubia wakazi wa mji huu,katika mkutano wa hazara uliyofanyika katika uwanja wa kambarage mjini hapa

Bw.Mbowe alisema matokeo yalio tangazwa na mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi nchini. jaji Lewis Makame yalikuwa ni yake na si ya wananchi walivyo amua katika masanduku ya kura.

Wananchi, mimi ninaamini kura katika uchaguzi wa urais zilitosha lakini hazikutangazwa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi jaji makame,alizo tangaza zilikuwa zakwake hata za mgombea wetu wa ubunge zilitosha lakini ziliibiwa mungu yupo tutakutana nazo haera alieleza Bw.Mbowe.

pamoja na hali hiyo mwenyekiti huyo aliwashukuru wananchi wa mkoa wa shinyanga walivyo kionga mkono chama chake katika uchaguzi huo,kwa kuwa na subira ,uvumilivu na kuwezesha uchaguzi kufanyika kwa amani na utulivu.

hata hivyo alisema kwa pamoja na kwamba CCM hivi sasa ni chama tawala,ni vizuri wananchi wakaelewa chama hicho kina wenyewe na sio chao.
Ndugu zangu hapana ...... muelewa ,kuwa pamoja na na kwamba chama hicho CCM ndiyo inatawala nchi hivi sasa ,lakini chama hicho sio chenu kina wenywe nyiye mnatawaliwa tu hata kama ni wa CCM.
Wenye CCM wako Dar es salaam kule OSYTERBAY,MBEZI BEACH, NA MASAKI alieleza Bw.Mbowe

Aidha mwenyekiti huyo alisema hawezi kumuombea mabaya rais JAKAYA KIKWETE katika utawala wake.kwani anaamini akifanya hivyo atakuwa anawaumiza wananchi wa nchi hii.

Aslisema kinacho takiwa sasa ni wananchi kuwakaba koo viongozi wote waserikali kuona kuwa wanatekeleza ahadi walizohahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu ,

Akizungumza tatizo la wanachama wa vyama vya upinzani kurudi CCM ,alisema hali hiyo ina sababishwa na uoga wa chama tawala kwa vile hakijiamini katika utawala wake.

kama kweli mgombea wa CCM alipata asilimiA 80% ya kura zote zilizopigwa sasa uoga wa nini kukimbilia kununua wapinzani,hawataki tume huru ya uchaguzi,wanatumia mabavu katika uchaguzi.yote ya nini kama wananchi wana wapenda ,alihoji.

Aidha alishanganzwa na katibu mkuu wa CCM bW.YUSUFU MAKAMBA kuwashawishi wapinzani na kuwanunua ,na kwamba wanafanya kazi burekwa vile wapi nzani wanao wanunua ni wazeena upinzani hupata damu mpya kila siku. tu mefungua tawi katika mitandao tofauti katika internet tuna wafikia vijana kwa urahisi kutoa hoja za msingi,tembelea www.jamboforums.com. alisema

CHADEMA tunapenda kumueleza Bw.Makamba asipoteze muda kununua wapinzani,wapinzani wapya wanazaliwa kila siku tena vijana,anaonunua ni wazee wamesha choka alieleza na kushangiliwa na wananchi.

Mwenyekiti huyo alikuwa mkoani hapa katika ziara ya siku moja akiwa na madhumuni ya kuwashukuru wananichi kwa kukiunga mkono chamachake katika uchaguzi ulioapita ambapo juzi aliutubia mikutano mitatu katika mji wa kahama .shinyanga mjini,na kishapu





.
 
...................

MBOWE NILIIBIWA KURA 2005

NA SULEMANI ABEID Shinyanga
Jumanne 2.1.2007


.........
Aidha alishanganzwa na katibu mkuu wa CCM bW.YUSUFU MAKAMBA kuwashawishi wapinzani na kuwanunua ,na kwamba wanafanya kazi burekwa vile wapi nzani wanao wanunua ni wazeena upinzani hupata damu mpya kila siku. tu mefungua tawi katika mitandao tofauti katika internet tuna wafikia vijana kwa urahisi kutoa hoja za msingi,tembelea www.jamboforums.com. alisema.

Hasara,

Hii habari umeitoa wapi?
Hayo hapo juu ndio maneno ya Mbowe au nawe umeongeza ya kwako?
 
Mzee hasara ataibuka na nyingine mpya wala msiwe na wasiwasi.
 
No Kibunamgo, Let us be constructive. It is now 2007. Tuache hayo.
 
Kuna mahali humu ndani imeripotiwa kuwa Mbowe anadai aliibiwa kura katika uchaguzi uliopita. Wakati wengine tukitaka kuamini hivyo, yeye huyo huyo anaonyesha kukiri kuwa "aligaragazwa" na sasa kishaamka. Kukiri huku kuwa "aligaragazwa" nakuchukulia kuwa ni kukubali kuwa alishindwa kihalali!


Mbowe atamba kumng'oa Kikwete 2010,awataka wapinzani kuungana

Na Ally Sonda, Manyara

MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Freeman Mbowe, amesema chama chake kinajipanga vilivyo kuhakikisha kuwa mwaka 2010, Rais Jakaya Kikwete anang’oka madarakani.

Mbowe ambaye yupo kwenye ziara ya Tumaini jipya, alisema hayo juzi Jumanne mbele ya umati wa watu waliofurika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mererani, wilayani Simanjro mkoani Manyara.

Alisema Rais Kikwete ajiandae kuiachia Ikulu mwaka huo kwa madai kuwa mbinu na mikakati iliyotumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupata ushindi wa ‘miujiza’ imefahamika na sasa Chadema inaifanyia kazi.

Mbowe ambaye mwaka jana aliwania urais kwa tiketi ya Chadema na kushindwa, alikiri mbele ya hadhara kuwa Rais Kikwete na CCM yake ‘walimgalagaza’ kwa kura nyingi mwaka jana, lakini alisema yeye kama mwanaume ameishanyanyuka na kujikung’uta.

“Napenda nikiri mbele yenu wananchi wa Mererani kuwa Rais Kikwete na CCM yake walinigalagaza vibaya mwaka jana. Lakini mimi ni mwanaume, nimenyanyuka, nimejikung’uta na sasa nina hasira ya kuwakomboa watanzania wanaonyanyasika ndani ya nchi yao,” alisema Mbowe.

Alisema Serikali ya Kikwete ambayo wananchi wengi maskini walidhani itawakomboa kimaisha, bado inaendelea kukumbatia ubabe wa kila aina na sasa baadhi ya makamanda wa polisi wamefikia hatua ya kutangaza vita ndani ya nchi yenye Amiri Jeshi Mkuu, jambo ambalo ni la hatari.

Alitoa mfano wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Manyara ambaye hivi karibuni alinukuliwa na gazeti moja la Kiswahili la kila siku (siyo Mwananchi) kwamba ameruhusu wawekezaji wa kigeni wa Kampuni ya Kuchimba Madini itumie silaha za moto kuwapiga wanaapolo.

Alidai kuwa hayo ni maagizo yanayostahili kulaaniwa na kumtaka Rais Kikwete na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Saidi Mwema, kumfukuze kazi mara moja kamanda huyo, kama kweli alitoa kauli hiyo yenye lengo la kuhatarisha amani kwenye eneo lote la Miererani.

Alisema serikali ya Kikwete inaweza kuingia kwenye balaa kubwa la vurugu za wenyeji na wageni, hususan wawekezaji endapo itaendelea kuwakumbatia wageni hao na kuwanyanyasa wazalendo.

“Mimi simtetei mchimbaji mdogo anayekwenda kuvamia wageni kwenye machimbo yao, bali ninachopinga ni serikali ya CCM kutoa raslimali zote muhimu kwa wawekezaji wageni na kuwaacha vijana wa kizalendo wakizurura hovyo,” alisisitiza.

Mbowe, ametoa wito kwa vyama vyote vya upinzani nchini kuungana ili kupata ya nguvu ya kuking’oa chama tawala madarakani.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara juzi uliofanyika katika viwanja vya NMC Unga Ltd uliohudhuriwa na mamia ya watu, Mbowe alisema bila vyama hivyo kuungana ni vigumu kushinda katika uchaguzi mkuu ujao.

“Leo hii nimekuja hapa na ujumbe wa tumaini jipya, ni kweli tulishindwa katika uchaguzi uliopita kwa kuhujumiwa, lakini tumepata funzo hivyo lazima tuanze mikakati ya mwaka 2010 sasa na kuna umuhimu wapinzani wote kuungana ili kuwa nguvu kubwa,” alisema Mbowe.

Mwenyekiti huyo alisema katika uchaguzi uliopita chama chake kilipatia kushinda wa viti 40 na kwa mujibu wa takwimu walizonazo kuna majimbo 10 walishinda lakini wasimamizi wa uchaguzi walitangaza washindi kuwa ni CCM.

“ Tulishinda kwenye majimbo mengi ikiwepo Ubungo, Hai na sehemu nyingine lakini kama ambavyo mlisikia jamaa wakajitangazia ushindi. Tulikaa tukaona haina haja ya kuendeleza mapambana, ila tusibiri uchaguzi ujao,” alisema Mbowe.

Akizungumzia tatizo la rushwa na madawa ya kulevya, alisema Rais Jakaya Kikwete kamwe hawezi kuyamaliza kwani viongozi na marafiki wanaomzunguka ndio watuhumiwa wakubwa.

Mbowe alisema, Watanzania wengi na hata yeye awali walikuwa na matumaini makubwa na uongozi wa Rais Kikwete, lakini kadri siku zinavyoongezeka matumaini hayo yanatoweka.

“Ningekuja hapa baada ya miezi mine mara baada ya kuchaguliwa Kikwete na ningemsema vibaya, nadhani mgenipiga mawe lakini leo hii naamani kuwa mnakubaliana na mimi kuwa mlijazwa upepo tu, nusra na mimi niingie mkenge,” alisema Mbowe.

Hata hivyo, alisema kinachotakiwa kufanywa hivi sasa ni kuungana kwa watanzania wote wanaopenda mageuzi ya kweli, ili kuhakikisha kuwa wanaiondoa CCM na serikali yake madarakani katika uchaguzi wa 2010.

“ Kama nilivyosema awali, mikutano ninayofanya sasa ni ya matumaini mapya kwa watanzania, hivyo lazima tukae na kujifunza makosa yaliyopita ili tusiyarudie tena,” alisema Mbowe.

Katika mkutano huo, Mbowe aliwaalika viongozi kadhaa wa vyama vya upinzani na wagombea wao wa ubunge, ambao pia walipewa nafasi ya kuwasalimia wananchi.
 
Kuna mahali humu ndani imeripotiwa kuwa Mbowe anadai aliibiwa kura katika uchaguzi uliopita. Wakati wengine tukitaka kuamini hivyo, yeye huyo huyo anaonyesha kukiri kuwa "aligaragazwa" na sasa kishaamka. Kukiri huku kuwa "aligaragazwa" nakuchukulia kuwa ni kukubali kuwa alishindwa kihalali!

Mwanagenzi,
naona hukusoma habari kamili au ulikuwa unataka kupotosha jambo kama ilivyo jadi yenu angalia hii quote hapa ya mbowe.

“Leo hii nimekuja hapa na ujumbe wa tumaini jipya, ni kweli tulishindwa katika uchaguzi uliopita kwa kuhujumiwa, lakini tumepata funzo hivyo lazima tuanze mikakati ya mwaka 2010 sasa na kuna umuhimu wapinzani wote kuungana ili kuwa nguvu kubwa,” alisema Mbowe.

habari imeendelea

Mwenyekiti huyo alisema katika uchaguzi uliopita chama chake kilipatia kushinda wa viti 40 na kwa mujibu wa takwimu walizonazo kuna majimbo 10 walishinda lakini wasimamizi wa uchaguzi walitangaza washindi kuwa ni CCM.

“ Tulishinda kwenye majimbo mengi ikiwepo Ubungo, Hai na sehemu nyingine lakini kama ambavyo mlisikia jamaa wakajitangazia ushindi. Tulikaa tukaona haina haja ya kuendeleza mapambana, ila tusibiri uchaguzi ujao,” alisema Mbowe.

kwakumalizia hizi habari hata mimi nilizipata kutoka kwenye reliable source of information na zaidi ilikuwa kwenye kura za wabunge hujuma nyingi zilitokea.
 
Mwanagenzi,

Hii hotuba ya Freeman baaabu kubwa!...
This guy is for real!...kanipa hata za Muhammad Ally kugalagazwa kisha anaamka na machungu mapya!
Eeeeh bwana weee, msalie mtume. Hasira za Simba aliyejeruhiwa!
 
Quarz
Sina haja ya kupotosha na sijui hao wenye jadi hiyo unaowazungumzia. Kwangu mimi habari ni kukiri kuwa "aligaragazwa" na binafsi sijawahi kumsikia mheshimiwa huyu kusema hayo kwa uwazi kama alivyosema.
Isitoshe sasa nimekumbuka kuwa hata mheshimiwa Lyatonga aliwahi kudai kuibiwa kura lakini baadaye akawageuka mashabiki wake kwa kuwaambia kuwa waache unafiki kwani pamoja na kuhudhuria mikutano yake na kusukuma gari lake mara kadhaa wakati wa kampeni, mashabiki hao kamwe hawakujiandkikisha kupiga kura! Akawauliza, "Sasa mlidhani nitashindaje?"

Mkandara,
Nakubaliana na Mtuhuru kwa ujasiri wa kusema anaanza mapambano upya. Hiyo ni bora kuliko kulalama kila mara. Na siasa inapaswa kuwa hivyo.
 
Mwanagenzi,

Hii hotuba ya Freeman baaabu kubwa!...
This guy is for real!...kanipa hata za Muhammad Ally kugalagazwa kisha anaamka na machungu mapya!
Eeeeh bwana weee, msalie mtume. Hasira za Simba aliyejeruhiwa!

Hiyo ndiyo inayomtofautisha Freeman na wanasiasa wengine bongo!
 
mwanasiasa, ni jambo moja kutoa hotuba za kuvutia, na ni jambo jingine kabisa kujenga chama kinachoweza kushika hatamu za uongozi!! Mbowe analo la kwanza, la pili sina uhakika nalo!
 
mwanasiasa, ni jambo moja kutoa hotuba za kuvutia, na ni jambo jingine kabisa kujenga chama kinachoweza kushika hatamu za uongozi!! Mbowe analo la kwanza, la pili sina uhakika nalo!

Kwa hilo la pili hawezi kufanya peke yake. Ni jukumu letu kumsaidia. Yeye kama binadamu, akiachiwa peke yake ataanguka kama ccm ilivyoanguka. Ndio hapo ninapotoa wito kwa wananchi wenzangu katika forum hii kujiunga kwa wingi na hiki chama. Hakuna njia nyingine ya kukomesha udhalimu wa mbwa mwitu ccm zaidi ya kujiunga na vyama vya upinzani hasa vile ambavyo vimeonesha kuwa makini. Tutatoa hoja kali sana katika hii forum na kwingine, lakini mwisho wa yote ni wananchi kuamua kwa njia ya kura. Basi tuamue tuwe washiriki wa kuleta mabadiliko kwa kujiunga na CHADEMA badala ya kukaa pembeni na kufanya critical analysis hali tukiwaachia wachache katika mstari wa mapambano.

I mean we have lamented enough about the woes of opposition parties in Tanzania; time has come for us to become lynchipin of our politics.
 
mwanasiasa, ukiwauliza watu utaona kuwa vyama vya upinzani bado havijawa chaguo la kwanza la wanaotaka kuingia kwenye siasa za nyumbani. Wengi wetu licha kasoro na kero zilizoko CCM bado tunavutiwa na CCM zaidi kuliko upinzani!! Siyo kwa sababu CCM ina sera nzuri kuliko vyama vingine, la hasha sababu kubwa tumeiona ikiongoza!! Viongozi wa upinzani hawajaonesha uongozi ulio mathubuti na wenye kujali Taifa!

Lazima tuwaone viongozi hawa wakiongoza ndipo tutavutiwa na vyama vyao!! Nilikuwa nakiheshimu Chadema sana, lakini baada ya kampeni za mwaka jana na hadi leo wamenikatisha tamaa!! Sasa naanza kukiangalia kwa karibu CUF huku moyo wangu bado uko CCM!!
 
nimefurahishwa sana na mh mbowe kuanza kampeni ya kukitangaza chama,ni
muhimu sana ,naomba watanzania bila kuangalia ushabiki wa vyama tuwaunge mkono wapinzani wenye moyo ili tuwatie moyo,upinzani sio dhambi ni muhimu kuwa na upinzani imara .
demokrasia ya kweli huleta maendeleo,tusiogope,tukiwa na chama kinachoua upinzani tutakua na serikali isiyo wajibika,tunataka "siasa itumikie uchumi na sio uchumi utumikie siasa"
 
Mzee Mwanakijiji: Una haki ya kusita huku ukifanya tafakuri. Pengine kitu kimoja kinachotutofautisha sisi watanzania na majirani zetu kama Kenya ni kuogopa mabadiliko. Hata mimi nilihama CCM kiakili siku nyingi sana, lakini ilinichukua kama miaka kumi kuja kuhama na mwili. Kwa hiyo ni hatua. Lakini natamani watu wengi wanaopenda mabadiliko wasingechukua muda mwingi kama mimi kuhama CCM maana nilipoteza muda na utumishi wangu bure. Hata ukienda CUF ni heri tu, cha msingi ni kuipa nguvu hii kambi ya upinzani na mabadiliko. Ninachosisitiza ni kwamba watu wote wanaofikri kwamba vyama hivi vinaendeshwa vibaya, ni muhimu wakiingia huko ili kurekebisha. Naamini vijana wachache kama kina Mnyika, Zito, n.k. wamesaidia sana kuipa chadema angalau taswira ya kutongozeka (kwa lugha ya Mkandara) kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Sasa tukiwa wengi mambo yanaweza kuwa mazuri zaidi. Ninachokataa mimi ni hii jadi yetu vijana watanzania kupenda kulalama kwa pembeni tukifikiri kwamba hivi vyama kama chadema ni vya kina Mbowe. Hapana, hivi vyama ni vya watanzania; watanzania wenyewe ndio sisi wenyewe. Tukumbuke hivi vyama vinatumia pesa ya wananchi (kodi) kwa hivyo lazima tuvimiliki. Hatuwezi kuvimiliki kama hatutajiunga navyo.

Najiuliza tena na tena, kwa mfano, watu wanapolalamika kuwa chadema ni family business. Hivi njia ya kuondoa ufamily business ni kuvisusa. Je, sio kwamba tukiingia wanachama kutoka sehemu mbalimbali za Tanzani kama wewe kutoka kule kijijini kwetu itasaidia kutoa huo 'ufamily business' kama upo?
 
Mwanasiasa, vyama vya upinzani ni lazima vijioneshe kuwa viko relevant. So far they have not, their accomplishments (if any) negligible! Nimezungumza huko nyuma kuwa CCM haiko ili kuimarisha upinzani na wala hawana jukumu la kuhakikisha vyama vya upinzani vinafanikiwa!! Lengo la chama cha kisiasa ni kushika hatamu za uongozi na kufanya kila mbinu kuuvunja upinzani!! CCM siyo tofauti!!

Kutegemea kuwa CCM itafanya mambo ambayo yataviimarisha vyama vya upinzani ni kujidanganya. Ni kwa sababu hiyo kuwa baada ya miaka kumi ya kuwepo vyama vya upinzani, vyama hivyo vimekuwa havina maana zaidi ya kutoa upinzani kwa majimbo machache na kitaifa kutokuwa na ubavu wowote! Kama vyama hivi vinataka kutiliwa maani na kuvutia watu wengi hata wale walioko CCM (kiakili au kimwili) havina budi kuchukua hatua za kujenga imani.

Vyama Vikuu vya Upinzani (CUF, CHADEMA, TLP NA NCCR) vikutane pamoja na kutoa tamko la kutambua udhaifu wake na kuahidi kujiimarisha (siyo kuomba CCM iwaimarishe). Tamko hilo lifuatiwe na hatua kadhaa.

a. Viamua kujiunga na kuwa Chama Kimoja cha Kikubwa badala ya vipande vya vyama! Hapa sizungumzii Shirikisho la chama bali kuunda chama kipya kimoja (mara tu sheria ya kuruhusu vyama kuungana itakapopitishwa).

b. Viongozi wa Vyama vya upinzani (vitakavyoungana) havina budi kutambua kuwa siyo wote watakuwa wenyeviti!! Lazima wakubali kujitoa kafara kwa manufaa ya Chama. Kwa hili CCM wako mbali sana! Kama Salim angeamua kuachana na CCM baada ya kuchezewa rafu wakati wa kampeni CCM ingetikisika kidogo, lakini hakufanya hivyo! Je Mrema, Lipumba, Mbatia, na Mbowe wako tayari kuachia Uenyekiti wa hicho chama Kipya kwa mtu mwingine ili wao wagombee Ubunge n.k?

Wakifanya kwanza jambo hilo, baso tutawaona wako makini (serious) na wamejifanya kuwa wao ni wa maana (relevant). Then tutachukua sera zao na kuzisoma kuona kama zinawezekana!

Ni hadi pale kuwe na Chama cha Upinzani ambacho Watanzania wanaweza kukiamini kuchukua uongozi wa nchi bila nchi kutetereka ndipo wengine tutajiunga navyo. Ama sivyo, tutaendelea kuikosoa CCM kwani mbadala wake hakuna!!
 
Hivi vyama vya siasa Tanzania ni ulaji tu.

(1). Kwa nini wameshindwa kuandaa maandamano kumpinga Richmonduli kuwanyamazisha wabunge?

(2). kwa nini wameshindwa kuandaa maandamano kupinga mikataba feki?

(3). kwa nini wanashindwa kuandaa maandamano kupinga unyanyasaji wa watanzania na vishirika koko vilivyowekeza TZ kwa miradi bomu?

haya ni mambo ambayo vyama vya upinzani wanatakiwa wafanye sio kusubiri wakati wa uchaguzi ndio tuwasikie. [WORK UP YOU GUYS, THE COUNTRY IS JUST WAITING FOR YOU TO START]
 
Back
Top Bottom