MUGONGO MUGONGO
Tumekuonya na hizo siasa zako za kutumwa ninaona ujasikia kama wewe unajipendekeza kwa JK
sasa tunakuumbua kwa sababu JK apendi watu ambao uwezo wao wa kufikiri ni mdogo imefika muda wa kuweka picha yako kila mtu akujue jinsi unavyo tumiwa hii forum ina msaidia JK kujua mapungufu katika serikali yake
JK awezi kutembea kila nyumba kusikiliza matatizo ya kila mtu pia awezi kutembea kila mkoa,wilaya,kijiji, kusikiliza matatizo ya mtu moja moja ,
kwahiyo sisi tuna mrahisishia kila kitu anakiona kwenye komputa yake anajua ni kiongizi gani anamatatizo siyo mwaminivu,siyo mkweli kwa sababu watu wake watamuandika rama ya kwanza mara ya pili mara ya tatu anamuondoa au kumuamisha wapo walio amishwa kutokana na forum hii.
Kwasababu viongozi wote mpaka mtendaji wa kata amenunua wahariri,ili asiandikwe maovu yake sasa hapa kila mtu anaandikwa atakama una pembe mia
Sasa soma kwamakini hii forum wewe unakwenda kubaya watu wote katika hii forum mimesha watumia private massege info. zako na picha na aliye kutuma maelezo yake yapo hapo na ushabiki
wakijinga mlionao, unafanya kazi mahali nyeti sana na tupo jengo moja tunajua jinsi ulivyo ingia hapo kazini,tuna jua hauna mtu kwenye forum hii bora uache au ubadilishe topick ongea hoja za msingi
Mimi ni CCM lakini sishabikii ujinga hata JK ananijua kwahiyo chunga mdomo wako ujui JK anafaidikaje kuhusu hii forum kwanza leo tumepishana hapo getini na tumepishana kwenye ngazi,dunia ndogo kijana sikuamini unatumiwa na
mwanaume mwenzako mbona uko simati sana nini unataka umbeya ufike kwa JK ,JK hana muda na watu kama wewe japo kuwa anakuona mara kwa mara
soma kwa makini ujuwe Muh Mbowe kaona mbali wewe badala ya kuwaalika viongozi wa CCM huku wajue faida za internet unalumbana na mambo binafisi ya Mbowe
Teknolojia ya Internet ina nafasi ya pekee, kwa miaka ijayo, ya kuwezesha wananchi na watu wengine toka katika sekta mbalimbali kuweza kuwasilisha ujumbe wao kwa umma moja kwa moja
bila kupitia mlango wa vyombo vya habari ambavyo mara nyingi habari muhimu za kimaendeleo zinaonekana kuwa "haziuzi" gazeti.
Teknolojia hii ina nafasi ya kumpa mwananchi uwezo wa kutimiza haki yake ya kikatiba ya kujieleza na kuwasiliana na watu wengine (wawe ndani ya nchi au nje).
Nguvu ya teknolojia hii ndio imefanya serikali za nchi kama vile China, Morocco, Misri, Pakistani, Bahrain, n.k. kuanza kukamata wanaforum na kuwatia jela au kutumia teknolojia zinazozuia
Internet zao kusomwa na wananchi katika nchi hizo.
Ni teknolojia hii iliyowezesha kufumuka kashfa ya mbunge wa Marekani aliyekuwa akiandika ujumbe mchafu wa maandishi kwa vijana wadogo. Kabla vyombo vikubwa vya habari na uongo kuwa na
habari hii tayari wanaforum walishaipata na kuchapa ujumbe aliokuwa akiandika mbunge huyo. Ni teknolojia hii iliyowezesha taarifa muhimu kuwafikia wahusika wakati wa janga la Tsunami na hata Katrina.
Ni teknolojia hii iliyowezesha dunia kujua kuhusu kukamatwa kwa mwanasheria na mtetezi wa haki za binadamu huko Ethiopia, Yalemzewd Bekele, siku kadhaa kabla vyombo vikubwa kama BBC
kuipata habari hiyo. Mwanaforum Ethio-Zagol wa Ethiopia aliandika kuhusu tukio hilo la mwisho wa mwezi uliopita ndipo vyombo vingine vya habari vikaanza kulifuatilia. Matukio na habari kawaida havisubiri mwandishi au mpiga picha.
Ni tekinolojia hii ndiyo iliyo mfanya MUH.KIKWETE na KARUME kushinda uchanguzi 2005 kupitia mtandao wa
www.uchaguzitanzania.com iliyo kuwa inaendesha kura za maoni kwa wagombea urais, bara na visiwani'' ZANZIBAR''
pia ni tekinolojia hii ndiyo iliyo fanya kampani za CCM kujulikana dunia nzima kupitia mtandao wa
www.kikweteshein.com pia Muh.JK alipokutana na waziri wa mambo nje wa marekani CONDOLEEZA RICE alimuambia JK alikuwa anafuatilia kampani za CCM, ilikuwa nzuri Ongera kwa ushindi tuko pamoja, karibu sana,
Ni tekinolojia hii iliyo tumika kwa serikali ya Tanzania kutoa tamko kuhusu filamu ya mapanki kupitia mtandao wa
www.darwinsnightmare.org
Ni tekinolojia hii wafanyabiashara wa tanzania wanatumia kutanga biashara zao nje
Nitekinolojia hii Tanzania inatumia kutangaza vivutio vya utalii na kutafuta wawekezaji nje
Matukio hutokea wakati wowote. Wakati wa shambulio la kigaidi kwenye treni na basi kule Uingereza, picha za wananchi wa kawaida waliokuwa na simu za mkono zenye kamera na habari za wanaforum vilikuwa ni hazina kubwa kwa umma uliokuwa ukihitaji kujua nini kilitokea na kilitokea vipi.
Ni umuhimu wa teknolojia hii uliomfanya aliyekuwa rais wa Marekani, Bill Clinton, kuamua, miezi kadhaa iliyopita, kukaribisha wanaInternet ili anywe nao chai.
Vyama vya siasa Marekani vinajua nguvu na mambo makubwa yanayoweza kufanyika kwa kutumia teknolojia ya Internet. Tena nguvu na sauti za wanaforum ni moja ya mambo ambayo yamebadili kabisa uwanja wa siasa nchini Marekani.
Na wachambuzi wa nyanja ya habari na siasa wanasema kuwa kati ya sababu nyingi zilizochangia kushindwa vibaya kwa chama cha Joji Kichaka ni teknolojia hii.
Sio ajabu unaposikia kuwa aliyekuwa mgombea mwenza wa John Kerry katika uchaguzi wa uliopita wa urais Marekani, John Edwards na mkewe, Elizabeth Edwards, ni wanaforum. Mkewe anasema
kuwa ni teknolojia hii iliyomfanya akawa hai na afya njema hadi leo baada ya mwanaye kufariki na yeye kugundulika kuwa ana kansa.
Ni teknolojia hii iliyomfanya mwenyekiti wa chama cha Democrat, Howard Dean, kupata umaarufu wa ghafla (ingawa alishindwa katika harakati za kuwa mgombea urais) na hatimaye kuwa mwenyekiti wa chama hiki.
Ni teknolojia hii ambayo imewawezesha wanaforum kule nchini Kenya, kupitia mradi wa Mzalendo (
http://mzalendo.com/) kuwa maripota wa masuala na habari za bunge la Kenya.
Kwa kutumia teknolojia ya Internet, mwanaforum aitwaye Kenyan Pundit na mwingine, Thinkers Room, wameanzisha forum ambayo nia yake ni kuwawezesha wananchi wa Kenya kujua nini
kinatokea bungeni, kuweza kushiriki katika mijadala kuhusu miswada mbalimbali na kupata taarifa kuhusu wabunge wao (kama vile kiwango cha elimu cha wabunge, jinsi ya kuwasiliana nao, na
hata kutumia Internet hii kuwatumia maswali).
Wameona bunge halitoa taarifa muhimu kwa wananchi (halina tovuti inayofanya kazi!) na vyombo
vya habari/uongo havitoi taarifa za kutosha kwa Wananchi
Samahani Muh. JK kwa kukutaja ndini ya forum hii ninaomba radhi kama nimemkwaza mtu yeyote haya ni maoni yangu na pia tunaelimishana CCM DAIMA-Ninaomba kutoa hoja
BY KING
ASANTENI