The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

The Only Thing We Have to Fear is Fear itself

Muh.mbowe
Tunashukuru kwa kutuelewa na kutaka ushauri kutoka kwa wananchi wa Tanzania pia itakuwa wewe nikiongozi makini katika jamii kwasababu unapenda kujifunza kila siku hata kwa mtu mdogo bila kuzarau maoni yake

Sisi kama wana forum tumekuruhusu kutumia forum hii kama jukwaa la siasa pia wengine katika vyama vyao wanaruhusiwa pia kutumia forum hii kisiasa kwanza uchaguzi wa maseneta marekani mwaka huu chama cha DEMOCTRATIC kimeshinda viti vingi kwa kutumia Mitandao ya Internet kwa hiyo Muh. Mbowe uko pazuri pia mimi nina shauri viongozi wa chama changu CCM waje huku kuongea na wananchi kusikiliza viliovyao.

Muh.mbowe forum hii ipo hapa kwasababu sauti za watu wengi zilikuwa hazisikiki hasa wanyonge vyombo vya habari vimenunuliwa vyote kutoa Tanzania Daima, vinaongelea upande mmoja tu wa mafanikio je upande wa mapungufu kama wa umeme ,mapanki,mikopo kwa wanafunzi ,n.k vitaongelewa wapi?

Huku hakuna kumfunga mtu mdomo pesa tuna kula na kukuandika tuna kuandika.

Mimi nina fikiri kuzaliwa mtanzania ni bahati kubwa sana tumekuwa na viongozi wachache wazuri wenye uchungu na nchi hii kama Muh.JK na Mbowe

Tumebarikiwa kwa vitu vingi kama mali asili, Lakini watendaji wake ndiyo wana muharibia sana hata mwaka haujaisha viongozi wamenza kujionyesha kabla hawaja timiza ahadi zao sasa hawa watendaji wa JK wanatoa mwanya mkubwa sana kwa chama kujulikana uzaifu wake.

Chama changu kina wazee wengi sana sina uhakika kama wanajua kutumia komputa. kwa sababu baadhi ya wabunge na mawaziri wana tumia email za watoto wao na wake zao, bila aibu wana ziandika kwanye business card zao nitaziweka kwenye forum hii siku chache zijazo, wengine hawajui email ni nini,

JK ana kibarua kizito tuna mkaribisha katika forum hii angalau kusoma tu kama hata kuwa na muda wakuchangia,

Ushauri wangu kwa JK jaribu kutumia wapinzani watu wako wanakuangusha utakuwa na kipindi kigumu sana 2010

asanteni
 
Wanaforum, Salaam sana!

1. Nawashukuru sana kwa makaribisho.Ukaribisho uliotoka kwa "Senior Members" kadhaa na wengine wote naupokea kwa heshima kubwa.
2. Nimesoma dhamira yenu thabiti ya kupenda kuendelea kutumia "pen names". Hoja zenu zina msingi na sina sababu ya kuendeleza mjadala wa somo hili.
3. Nitashiriki kadri fursa zitakavyoniruhusu, hata hivyo, mniruhusu nisijiingize kwenye malumbano yasiyo na "substance."
4. Nategemea hoja kadhaa zinazohusu Chadema na hata viongozi wake, zitaibuliwa. Ni lengo langu zijibiwe zote. Sisi kama chama hatuendeshi siasa za kificho na woga. Mimi na timu yangu yote tunaamini katika kujenga Chama Taasisi. CHADEMA siyo mali ya Mbowe na viongozi wenzake, ila Mbowe ni kiongozi wa taasisi hii. Uongozi ni dhamana na naheshimu na kulisimamia hili.
5. Kila taasisi makini ina taratibu zake za ki-utawala sambamba na mfumo wa utoaji habari. Naheshimu forum hii kama chombo kamili cha habari chenye haki ya kuhoji na kujua chama hiki kinachangia nini katika mustakabali wa Taifa letu. Kama tulivyo tayari wakati wowote kuhojiwa na chombo chochote cha habari, tutakuwa tayari kujibu hoja yeyote yenye mantiki. Hivyo basi, itawezekana baadhi ya hoja zikajibiwa na watendaji wa chama na nyingine nikajibu mimi.
6. Pale hoja itakapokuwa imepewa majibu rasmi ya chama, watendaji wa chama watatumia majina yao halisi na nafasi zao ndani ya chama zitawekwa wazi. Lengo hapa ni kuepuka majibu yasiyo rasmi yakapewa tafsiri potofu kuwa ni majibu rasmi ya chama.
7. Sina hakika kama utaratibu huu utaendana na azma ya forum hii. Aidha, si kusudio langu kugeuza forum hii jukwaa la siasa la Chadema, ila naamini jamii na wanaforum wana kiu ya kuelewa vyama vinasimamia vipi maslahi ya Taifa.
8. Wanabodi na wanaforum, kama uelewa wangu ni sahihi, naomba ushauri ili hoja zianze kujibiwa.
9 .Sitasita vilevile kutoa maoni yangu binafsi inapobidi.

Nawashukuru kwa kunisoma

Freeman Mbowe

Huyu ndiyo Mbowe ninaye mfahamu miye. Karibu sana Bw. Mbowe na naamini utafaidika na forum hii na wanabodi watafaidika pia na uwepo wako. Jambo moja nakuhakikishia hapa kuna watu hata utakapowapa majibu murua namna gani bado watakwambia upinzani ni wababaishaji. Kosa lenu? Hamkuamua kubakia CCM nakutumia mali zenu kununua uongozi
 
Freeman Mbowe

Umepewa maswali mengi, sasa ni jukumu lako kuamua kujibu kwa kipindi ambacho unaona ni sawa, ingawaje maswali mengine ni ya kurudiarudia utakayoyaacha tutakukumbusha. Sina sababu ya kuongeza maswali mengine hadi pale ya kwanza yatakapojibiwa.

By the way nafikiri ingekuwa vizuri ukaanza na yale nyeti maana MGAWOO ndio hivyo tena.
 
Guys, I am not sure if this is going to work...Mbowe being here as Mbowe and not using "Pen Name".

My suggestion to you Mr Mbowe is to use your real name to answer questions directed to Chadema. But when it comes to comments based on your personal opinion then use "Pen Names".


That will protect wanaforum wenye brain dhaifu kama mimi kutokuchanganya msimamo/opinion ya Mbowe kama Mbowe na msimamo wa Chadema.

Much Respect to you and the party for being here.
 
Mzee Freeman,

Sasa tuanze kazi sasa, hebu tuanze kukata issues! Yameshawekwa maswali ya kutosha sasa kazi!
 
Mheshimiwa Mbowe
niliomba utupe utaratibu wa kupata degrii zako, kuna wengine wanasema unasoma full time wengine wanasema PT wengine wanadai distance Learning naomba unifahamishe hilo.
kama litakuwa limekaa vibaya tuma kwenye PM yangu.
umeamua uamuzi mzuri sana hata Obasanjo amufuata nyayo zako kweli nimeamini TZ tunaye shujaa.Mbowe
 
Muh. Mbowe
Ninaomba kuchukua nafasi hii kueleza machache jinsi ninavyo mfahamu Muh. FreeMan Mbowe, tumesha kuwa namaongezi miaka ya nyuma akiwa katika safari zake za kibiashara anaongea kuhusu kuwa na wabunge vijana bungeni ili kubadilisha mfumo mzima usiobadilika kwa miaka mingi na kuwa na watu walewale bungeni wanao tuwakilisha na sura zile zile.

Kwa kweli Muh. Mbowe alikuwa anaongea kwa uchungu sana mimi niliona kama ndoto au maongezi ya kawaida tu ya kisiasa muda ulivyo kwenda nilizidi kuona mabadiliko yake katika siasa aliwezakuniambia jinsi tanazani ilivyo barikiwa jinsi watuwake wanavyo shindwa kufaidi au kutumia mali saili tulizonazo kujikomboa katika janga la umasikini basi alinipa mifano mingi sana.

kwa kweli sikuweza kumuelewa kwakipindi kile kwasababu na mimi sikuwa ninauelewa nilimsikiliza na sikuweza kuchangia hiyo mada kwa sababu mimi sipendi siasa ilikuwa juu ya uwezo wangu wa kufikiri.

Rafiki yangu aliye nikutanisha na Muh. Mbowe bwana PETER yeye aliweza kuchangia mada hiyo ya kisiasa, mimi baada yapo niliendelea na shuguli
zangu zakawaida, sikuwa na mawasiliano tena naye kwa kipindi kirefu,

Siku nilipo onana na muheshimiwa huyu alinipa heshima kubwa sana alinipokea kama mfanyabiasha mkubwa sana alichukuwa muda wake kunifahamisha kwa rafiki zake ,kipindi hicho bado hajawa mbunge natumaini alikuwa katika maandalizi hayo miaka michache baadaye,

Mimi kama bwana KING ni mtu mdogo sana wala sikustailikuonge na Muh. Mbowe nilikuwa dereva wake kwa muda wa wiki moja tu, huko ugaibuni niliombwa na rafiki yangu PETER kama ni weza kumpeleka Muh. aliko niagiza
nilifurai sana kukutana naye kwa sababu nilikuwa nina msikia lakini nilikuwa simfahamu na ni mtoto wa kifaru, alianza umaarufu siku nyingi ninatumaini mnakumbuka zama hizo za watoto wa matajiri walivyo kuwa wanatesa,

nilikuwa na Muh. Mbowe kwa muda huo wa wiki moja kama nilivyo agizwana boss wangu pia nilijifunza mengi sana ALINISAIDIA alinishauri mengi na mifano mingi sana mimi nikiwa kama kijana mdogo nina ishi ugaibuni.

Akanishauri niende shule nisijiusishe na mambo ya anasa kama mnavyojua majuu kulivyo na vituko vyo kidunia, muheshimiwa alinionea huruma sana maisha ninayo ishi alipenda kunisaidia alinipa nafasi hiyo akanipa namba zake zote za simu nikiwa na shida basi nimtafute lakini mimi sikufanya hivyo, kwasababu mimi ni mtu mdogo sana niliogopa hata kumpigia kwa kumsalimia

Mimi nimechukuwa nafahi hii kuelezea maneno machache unapokutana na mtu kwa mara ya kwanza akaongea kitu baada ya miaka kumi na mbili ( 12 )
akafanya kile ulicho kisikia basi inamana huyu yuko siriazi na ni mtu anaye weza kuleta mabadiliko makubwa sana katika taifa letu kama atarudi CCM .Nina fikiri baada ya JK tunaitaji kiongizi anyetoka katika sekta binafisi.
Samahani kiswahili changu siyo kizuri Asanteni
 
mi pia mgeni hapa naiepnda Chadema na nina mambo kadhaa nataka kuongea:

1. eti ni kweli anna komu bibi yako ndio maana akawa mgombea mwenza baada ya kufa yule mzenji na vilevile akawa kwenye nafasi ya kuwa mbunge viti vya wanawake chadema

2. naomba maelezo kuhusu sakata la wagombea viti maalum chadema manake kamati kuu yenu ilitaka kukuondoa lakini wazee wa busara kina makani, mtei na wengineo wakaingilia wanasema eti mmechagua mabibi zenu tu zitto na muhonga, wewe na anna komu na kiwelu na halima mdee na yule binti wa ndesamburo. what happened?

3. je unadhani wanaosema huna haki ya kuongelea mapambano ya kumkomboa mnyonge wakati umekuta kila kitu kwenye silver plater na dingi wako alikuwa mtu pekee aliyeruhusiwa kununua benzi na mchonga wanakuonea?

4. biashara zako: inasemekana hakuna nidhamu katika uendeshaji biashara zako ndio maana una madeni mengi na una-reschedule kila mara. wanasema kuna ushahidi kwamba uamuzi wa mahakama kuku-liquidate unausogeza mbele for legal technicalities. nssf, remember? sasa kama huwezi kuendesha biashara zako, utaweza kuendesha nchi?

5. hiyo hapo juu inaeleweka ila natoa ushauri kwamba umejiingiza kwenye siasa kama mfanyabiashara it is really trick kwasababu biashara in bongo is synonimuos with scandal. there is no clean businessperson in bongo. wanasema washikaji zako ccm ndio kwasababu ya biashara. basically you have been compromised na unayosema yote kuhusu ukombozi ni rhetoric tu.

6. magwanda. wakati wa kampeni yale mavazi yalikuwa interesting. ulisema eti kwasababu uko vitani. sasa huoni kufananisha kampeni na vita haileti ujumbe mzuri kwa nchi yetu ya amani? niliona mnyika na zitto na jamaa wengine nao walikuwa wanayavaa. tena mnyika na kamwili kake kadogo ndio ilikuwa kituko. did you force them to wear the gear? au walilazimika kwa kuona unayavaa?

7. mwakagenda v. baregu. kwanini mlimuengua mwakagenda an incumbent member wa EALA na kumweka baregu kama mgombea? mwakagenda haku-perform? au ni tishio kwa mbowe?

8. tanzania daima. kwanini usije tu hadharani ukasema you own the paper, and free media inc. na unawatumia kina ansbert ngurumo na waandishi wengine kama ambavyo ccm inawatumia wengine. nadhani itakuwa jambo la heshima kuwa mkweli kwenye hili.

9. ushauri: siasa sio environmental movement. you win if you play dirty. wadau bongo wanajua you play dirty, na tatizo ni the limited impact of your dirty politics, ila kinachokera ni kujifanya clean hadharani. you will never win an election kwa frame hii. i think you have a good team: zitto is bright, but reactionary. mnyika is wise, but naive. mzee mtei is a management guru is still bitter about mwalimu and the lost glory of machame empire. makani is witty but as useless as a TV wrestler. yourself is really good, but as ethically compromised as those you condemn. mwakagenda is good, but he is feared therefore underutilised. kaburu was good, but he was feared and underutilised, therefore left. slaa is my man, a legal and constitutional matador, i hope he won't be feared and underutilised and leave. the ladies of chadema bungeni, well, what can I say?

10. ushiriki wako hapa forum. a strategic mistake, ungekuwa unasoma tu. this place is addictive and you and your team will be bogged down here badala ya kufanya homework yako hapo shuleni. i think you have potential but you are a very naive politician.

aisee hivi ilikuwaje ukatoa bastola na kutishia yule mhuni kule karatu wakati wa kampeni. hauni ile incident inaku-disqualify kama kiongozi. tofauti na ditto ni kwamba yeye alifanya kweli.
 
Mugongo,

Looh! haya maswali kwa mheshimiwa Mbowe naona kiboko kweli kweli.

Huenda hata aandike nini bado anaweza kuishia kuwa bogged down na kazi
zake zingine kudorora.

Ndio maana vigogo wengine wanaogopa kujitambulisha wazi kwenye forums
maana kuna maswali mengi mno ya kuwauliza. Imagine Lowassa anakuja hapa, nafikiri maswali yanaweza kuzidi 100.

Mheshimiwa Mbowe kama unahitaji ushauri, soma maoni ya Watanzania na yafanyie kazi chinichini na kujifunza na ndio shule yenyewe na ni kubwa kuliko hata kuka darasani. Pale unapoona kuna haja ya kujibu fanya hivyo ila maswali
yaliyomengi ukiamua kujibu basi utaishia kutengeneza maswali 20 mengine.

Haya mambo yanayoongelewa kwa mheshimiwa Mbowe ni dalili kwamba
Watanzania bado hatuna uhuru kamili wa kuuliza maswali magumu magumu
au waandishi wetu hawana uwezo, hawana pesa au hawana nguvu ya kufuatilia kwa kina juu ya tuhuma zinazowahusu baadhi ya viongozi wetu.

Ingelikuwa hapa UK, tusingesubiri forums ili kuweza kuuliza baadhi ya maswali yetu na badala yake The SUN wangeweza kutusaidia kutupatia majibu yetu
kwa muda mfupi sana hasa haya ya uhusiano wa sex na kupeana madaraka. Hili ni jambo zito na linahusu maslahi ya taifa. Wengine tungetaka kujiepusha kuongelea mambo binafsi ya watu lakini kama mambo hayo binafsi yanaingiliana na utendaji wa chombo kama Bunge basi yanageuka na kuwa maswali halali.
 
Mugongo:

Haya maswali ya Anna Komu kuwa nanihii wa Mbowe mtumie kwenye PM yake hayana nafasi hapa, uwe na heshima na wanaforum.

Maswali muhimu ni kama ni kweli kuna issues za liquidation katika biashara zake tungependa kujua manake ni relevant with his credibility as a good manager.

Kama na wewe una ushahidi weka hapa, sio kuuliza kama vile mgeni humu, weka ushahidi kwamba hao nssf wanamdai kiasi gani, kesi ipo wapi nk, usiwe kama akina.....ambao ushahidi wao humu ni kwamba waliingia nyumba husika [angalia thread ya mkapa kwenye makabrasha]

Kwa sasa ni haya.
 
mzee tafiti,

samahani mzee unajua waswahili wanasema ukimuona jumbe mwambie shida zako zote, kwahiyo nimekuwa excited kumuuliza mweshimiwa mbowe mambyo yanayoongelewa mtaani na kwenye vijiwe vya siasa hapa bongo. mimi mgeni sikujua kwamba kuna limit ya mambo ya kuongea hapa. na sikujua kwamba maswali hayaruhusiwi. lakini naamini katika methali inayosema kuuliza si ujinga. umesema nitoe ushahidi. sina. ndio maana yangu yamekuwa maswali tu.

wasalaam mzee
 
Tafiti,

Hivi kama kweli Ann Komu kapewa ubunge kwasababu ni nyumba ndogo
ya mheshimiwa Mbowe huoni kama hilo tayari linakuwa suala linalohusu maslahi ya nchi na kuuliza is a fair game?

Kama mheshimiwa X ana uhusiano na dada Y na mambo yanaishia hapo, hata mimi naona hayatuhusu sisi wengine.
 
mzee mtanzania

tena kuna mengine mengi ambayo nimeona niyaache mpaka tusikie kwa mweshimiwa mbowe. i hate to bring kids into this, lakini mweshimiwa mbowe anaongelea sana uzalendo wakati some of his kids wana passports za marekani.

the bottom line ni kwamba mbowe needs to tread carefully anapo-attack kwamba there are lots of stuff about him watu hawajui. lakini guess what? watu wakiyasema utasikia "hizo ni mbinu chafu za ccm".
 
Well well well,

Nilikuwa pembeni kidogo ktk sakata la kutafuta hela. Nimefurahi kumuona Mheshmiwa Mbowe humu, safi sana.

Kama kawaida nitaanza na kuangalia upande mwingine wa shilingi.

Mugongo Mugongo, aisee maswali umeuliza mazuri sanaa ila unapotaka kuingiza personal issues sasa inabidi tukuchukulie kama wale jamaa wa mango garden kwenye Mugongo*2. Mfano, issue ya watoto wake inakujaje humu?, hata issue ya biashara zake pia ninaamini sio mahali pake. kwani wakati yupo ulaya kuna watu wanaiendesha kama ikifa kwa kubadilika kwa soko au tech basi ni kawaida, zimekufa kamapuni ngapi kubwa sembuse ya mbowe. Hivi kuwa na benz inasaidia nini taifa? jamani we better be serious lasivyo Mbowe ataona ameingia kwenye kijiwe cha bunch of wajinga wasiojua nini cha kuongea. Hayo ya uchaguzi na kuteuliwa ninaunga mkono anaweza kujibu atakavyo.

Kwako Mbowe, Frankly mimi ni CCM damu. Tena kunishawishi nihamie upinzani ni sawa na kunibadili dini. Sera zako nyingi ninazikubali ila ile ya MAJIMBO, kaka pale hapana, pale naona unataka mikoa ya Lindi na Mtwara zife kabisa. Sioni uzuri wa hiyo sera, unaweza kunifafanulia?

Thanx

FD
 
i think mbowe is a big boy who can take care of himself kwahiyo hakuna haja ya kum-patronise hapa.

i think ukifikia level ya kuutaka na in fact kuugombea urais, everything is fair game, iwe ulaya, marekani hata hapa bongo. ya kusema tutenganishe personal and public ni mambo ya theory tu. nothing is irrelevant. i am sure mbowe amekuwa anasoma hapa and he has seen how vicious members have personally exposed lowassa, jk, mkapa, salim, ro, ra and other public figures. nadhani we have the right and luxury ya kuwaabuse kwasababu ya nafasi zao. why take that privilege away when it comes to mbowe? ndio maana nasema siasa sio sawa na kuongoza greenpeace anti-whaling campaigns.
 
Muh. Mbowe
Ninaomba kuchukua nafasi hii kueleza machache jinsi ninavyo mfahamu Muh. FreeMan Mbowe, tumesha kuwa namaongezi miaka ya nyuma akiwa katika safari zake za kibiashara anaongea kuhusu kuwa na wabunge vijana bungeni ili kubadilisha mfumo mzima usiobadilika kwa miaka mingi na kuwa na watu walewale bungeni wanao tuwakilisha na sura zile zile.

Kwa kweli Muh. Mbowe alikuwa anaongea kwa uchungu sana mimi niliona kama ndoto au maongezi ya kawaida tu ya kisiasa muda ulivyo kwenda nilizidi kuona mabadiliko yake katika siasa aliwezakuniambia jinsi tanazani ilivyo barikiwa jinsi watuwake wanavyo shindwa kufaidi au kutumia mali saili tulizonazo kujikomboa katika janga la umasikini basi alinipa mifano mingi sana.

kwa kweli sikuweza kumuelewa kwakipindi kile kwasababu na mimi sikuwa ninauelewa nilimsikiliza na sikuweza kuchangia hiyo mada kwa sababu mimi sipendi siasa ilikuwa juu ya uwezo wangu wa kufikiri.

Rafiki yangu aliye nikutanisha na Muh. Mbowe bwana PETER yeye aliweza kuchangia mada hiyo ya kisiasa, mimi baada yapo niliendelea na shuguli
zangu zakawaida, sikuwa na mawasiliano tena naye kwa kipindi kirefu,

Siku nilipo onana na muheshimiwa huyu alinipa heshima kubwa sana alinipokea kama mfanyabiasha mkubwa sana alichukuwa muda wake kunifahamisha kwa rafiki zake ,kipindi hicho bado hajawa mbunge natumaini alikuwa katika maandalizi hayo miaka michache baadaye,

Mimi kama bwana KING ni mtu mdogo sana wala sikustailikuonge na Muh. Mbowe nilikuwa dereva wake kwa muda wa wiki moja tu, huko ugaibuni niliombwa na rafiki yangu PETER kama ni weza kumpeleka Muh. aliko niagiza
nilifurai sana kukutana naye kwa sababu nilikuwa nina msikia lakini nilikuwa simfahamu na ni mtoto wa kifaru, alianza umaarufu siku nyingi ninatumaini mnakumbuka zama hizo za watoto wa matajiri walivyo kuwa wanatesa,

nilikuwa na Muh. Mbowe kwa muda huo wa wiki moja kama nilivyo agizwana boss wangu pia nilijifunza mengi sana ALINISAIDIA alinishauri mengi na mifano mingi sana mimi nikiwa kama kijana mdogo nina ishi ugaibuni.

Akanishauri niende shule nisijiusishe na mambo ya anasa kama mnavyojua majuu kulivyo na vituko vyo kidunia, muheshimiwa alinionea huruma sana maisha ninayo ishi alipenda kunisaidia alinipa nafasi hiyo akanipa namba zake zote za simu nikiwa na shida basi nimtafute lakini mimi sikufanya hivyo, kwasababu mimi ni mtu mdogo sana niliogopa hata kumpigia kwa kumsalimia

Mimi nimechukuwa nafahi hii kuelezea maneno machache unapokutana na mtu kwa mara ya kwanza akaongea kitu baada ya miaka kumi na mbili ( 12 )
akafanya kile ulicho kisikia basi inamana huyu yuko siriazi na ni mtu anaye weza kuleta mabadiliko makubwa sana katika taifa letu kama atarudi CCM .Nina fikiri baada ya JK tunaitaji kiongizi anyetoka katika sekta binafisi.
Samahani kiswahili changu siyo kizuri Asanteni


King umesema kumbukumbu zako. Sawa. Lakini umehitimisha vibaya kwa kutaka watu serious warudi CCM. Niamini. Kurudi CCM ni kusarenda, ni KUFA. Kama kuna mtu anajidhania serious, na anataka kufanya siasa, CCM haina nafasi kwake. Hivi unaona seriousness ndanii ya CCM? Kinachonekana pale ni mabavu, ujanjaujanja na corruption ambayo si rahisii kuikemea kwa kujiunga nao. Hatuna mfano wa mtu yeyote aliyerudi CCM akabadilisha au akaathiri chochote. CCM ni system KUBWA MBOVU. Suluhisho ni kuibomoa ama kutoka ndani au nje. Kipande kitakachosalia ndichokitawafaa Watz. Lakini kuibomoa kutoka ndani ni kazi kubwa kuliko kuibomoa kutoka nje. Maana walio ndani wanafahamiana na wanashahabiana kwa tabia na wimbo wa CCM INA WENYEWE!
 
Mugongo una maswali mengi mazuri kwa Mbowe. Nadhani hawa jamaa wakuache umuulize. Kwa wadhifa wake na kazi anazofanya, na aina ya siasa anazo-introduce Tanzania, haaswi kukwepa maswali haya. Hata hivyo, itabidi afanye kazi ya ziada maana ni mengi mno. Naona tanaingiakila mara, na sidhani kama naye atakuwa anakaa kwenye mtandao muda wote. Bila shaka alikuwa mjanja pale alipoomba kuwa atakuwa anaingia mara moja moja na kujibu atakayoweza. Binafsi simtarajii awe na majibu yakila swali, lakini nimjuavyo hatakaa kimya.

Ila sasa naona kama hatuna moderation nzuri ya maswali kwa watu kama hawa. Kinachoonekana hapa, watu wanamwaga nyongo zao. Mtu anaweza kudhani hizo ni hisia za watu, ni maoni yao, akazibariki na kuondoka. Lakini hebutuone atakavyojibu. Lakini kungekuwa na namna yakumoderat maswali ingesaidia, tukajua lipi lifuate lipi, lipi limejibiwa na lipi bado. Vinginevyo, kama alivyosema Mtanzania hapo juu, inaweza kumchukua Mbowe kuandika kitabu katika kujibu maswali haya. Itambidi awe mwangalifu na mwelekevu. Ni hapa ndipo tutapima seriousness yake.

Ila nadhani, to be serious, tungetanguliza issues kwanza, personalities tukaziweka mwisho. Watu makini hawaanzii kwa mtu bali kwa masuala. Mbowe hana namna ya kukimbiza nafsi yake katika siasa. Tutamjadili tu. Lakini tuanze na issues kwanza. Tusije kuwa kama waliomshabikia Kikwete kwa kuangalia sura badala ya kujadili masuala ya nchi na kuona kama miongoni mwa wanaoyaweza Kikwete yumo. Watu walianzia kwenye personality wakaishia kwenye personality kwa sababu ni rahisi kuzungumzia personality. Si unajua kila mtu ana udhaifu wake? Yaani hata sisi tunaoandika, hatuko safi.

Laiti Watanzania tungeanzia kwenye issues, Kikwete asingekuwa na shida hizi zinazomkabili, kwa kuwa inawezekana asingepewa dhama hiyo. Uwezo wake ni mdogo kuliko sifa tulizompa. Kweli, tulitenda dhambi. Tusiirudie hapa.
 
Mugongo Mugongo-CCM-umetumwa Issue Binafisi Za Muh. Mbowe Hatuzitaki Kwa Wakati Huu Tunataka Hoja Za Msingi Kama Umeme Wa Richmond , Elimu, Mikopo Kwa Wanafunzi Wa Elimu Ya Juu ,Ukimwi, Mpasuko Wa Kisiasa Zanzibar, Safari Za Kikwete,Lowasa, Shirikisho La Afrika Mashariki, Rwanda Na Burundi Kujiunga Na Eac, Nyumba Za Serikali, Issue Ya Mapanki ,Ajira , Afya na kadhalika.

Tuna Jua Jina Lako Baba Yako Familia Yako Komputer Unayotumia Unapoishi Naukitaka Picha Yako nitaiweka Hapa Sasa Hivi Watu Wana Lala Giza Wewe Unaongea Mamboya Ki........., Unatukera Sisi Tunahamu Ya Kuongea Na Viongozi Siyo Wewe Unaye Tumiwa Kama.....naaliye Kutuma Mwambie Hatulipani Fazila Hapa Tuna Jadili Hoja Nzito Nzito ,

Ninavyo Kujua Hiyo Siyo Akili Yako Unafahamiana Na Watu Wakubwa Sana Unakazi Nzuri Sana Na Maisha Yako Mazuri

Sasa Wewe Ndiye Msemaji Wa Wanaume Wengine Tunamjua Aliye Kutuma Hatulipani Fazila Hapa Na Ninani Aliye Kutuma .

Mimi Ni CCM Damu Kuliko Wewe Unaye Fuata Mkumbo Babu, Bibi Mama Baba Yangu Ndiye Waanzilishi Wa Asp,Tanu,ccm Wewe Umerukia Wakati Wa Jk

Kwanza Wewe Unamchafulia Na Kumuaribia Jk Sisi Sote Tuna Taka Kujifunza Kutoka Kwa Viongozi Wetu Hata Kama Wako Upinzani

Mimi Nina Amini Muh.Mbowe Siyo Mpinzani, Angalia Historia Ya Baba Yake Alivyo Muwezesha Mwalimu Nyerere Sasa Unasema Huyu Ni Mpinzani ,

Kila Kitu Alicho Nacho Ni Matunda Ya Asp, Tanu, CCM Nguvu Anayo Tumia Ni Ya CCM Sasa Wewe Unajipendekeza Uonekane Mzuri,

Muh. Mbowe Na Jk Wanatofauti Gani Wakati Sasa Hivi Ndani Ya CCM Kuna Mpasuko Mkubwa Sana Kuna CCM Asili Na CCM Mtandao

Basi Jk Naye Ni Mpinzani Kutesa Kwa Zamu Mbowe-na-Chadema Jk-na-CCM Mtandao Sasa Tuwache Hayo Mr. Mugongo Kama Unataka Tuiandike CCM.... Siwezi Ninapenda Sana Chama Changu

Na Tumuombee Jk Maisha Marefu Kwa Sababu Anakipindi Kigumu Sana Jk Pia Anataka Kujuwa Watu Wake Wanasema Nini Kuhusu Hali Ya Uchumi Kwa Maisha Ya Mtu Wakawaida Abaye Ataandika Tatizo Lake Hapa

Asikie Kutoka Kwetu Sisi Wanyonge Ametupigania Sana Ameahaidi Kufa Kwa Ajili Ya Wanyonge Sasa Kwanini Wewe Unamnyima Muh. Jk Uhuru Wakujua Maoni Ya Watu Wake,

Sisi Ndiyo Wapiga Kura Wake ,ni Rais Mvumilivu Na Msikivu Sana Hatuwezi Kuwa Na Rais Wa Matumaini Kama Jk Wananchi Wake Wanavyosubiri Maisha Bora Kama Jinsi Waumini Wanavyo Msubiri Bwana Wao Atarudi Kuwachukua Waende Peponi. Kwenye Maisha Bora Kwa Kila Binadamu

Asante
 
Mbowe amefanya vizuri kuingia humu lakini maswali kama hayo ya so called Mugongo yana subtsance yeyote? yatatusaidaje au ni kutaka tu kuvuruga?

wavurugaji wapo na ukiwapa watu uhuru mkubwa wa kuuliza maswali yatatoka hata ya chumbani!

Sasa topic itageuka kuwa udaku udaku tu kwa misingi ya imani za vyama vyetu.

waafrika ndivyo tulivyo!
 
Back
Top Bottom