mi pia mgeni hapa naiepnda Chadema na nina mambo kadhaa nataka kuongea:
1. eti ni kweli anna komu bibi yako ndio maana akawa mgombea mwenza baada ya kufa yule mzenji na vilevile akawa kwenye nafasi ya kuwa mbunge viti vya wanawake chadema
2. naomba maelezo kuhusu sakata la wagombea viti maalum chadema manake kamati kuu yenu ilitaka kukuondoa lakini wazee wa busara kina makani, mtei na wengineo wakaingilia wanasema eti mmechagua mabibi zenu tu zitto na muhonga, wewe na anna komu na kiwelu na halima mdee na yule binti wa ndesamburo. what happened?
Habari za siku nyingi?
Mimi naomba kwa ufupi nitoe maelezo kuhuusu hili suala la viti maalumu maana linaibuliwa na kuzimika na kisha kuibuliwa tena na tena. Naomba radhi kuwa imenibidi nijibu hoja hii tu maana ndio nimetoka hospitali ambako nililazwa kwa siku mbili tatu hivi. Ninaendelea vizuri sana.
Kwa wale wasiojua, viti maalumu vya ubunge kwa chama vinapatikana kutokana na idadi ya kura ambazo kila chama kimepata katika uchaguzi ili mradi tu chama hicho kiwe kimefikisha asilimia 5 ya kura zote.
CCM walipata asilmia 69, hivyo viti 58, CUF walipata asilimia 14 hivyo viti 11 na CHADEMA asilimia 8 na hivo kupata viti 6.
CHADEMA kama chama cha siasa, na kama mwenyekiti wake alivyosema kuwa ni chama asasi, kina taratibu zake za kupata wabunge wa viti maalumu. Sio lazima utaratibu wa CHADEMA uwe kama wa CCM au CUF. Ninavyoelewa mimi na kufuatia utafiti wangu niliofanya kama mwananchama wa CHADEMA utaratibu ulikuwa nimzuri na ulizingatia matokeo ya uchaguzi.
1. Mkoa wa Kilimanjaro ndio mkoa uliotoa kura nyingi zaidi kwa CHADEMA katika uchaguzi wa 2005 (
www.chadema.net/matokeo). Ulikuwa mkoa wa kwanza. Katika viti 6, Kilimanjaro ikapewa viti 2 - Grace KIWELU ambae alikuwa Mbunge na alitunukiwa heshima na Kamati Kuu ya Chama kwa utendaji mzuri na kuheshimu maagizo ya chama alipokuwa Mbunge) na Lucy Owenya ambae ni mwanachama wa CHADEMA toka 1992 na amekuwa akisaidia sana chama kimali nyakati zote za kampeni. Pia aligombea na kushinda mkoani Kilimanjaro.
2. Mkoa wa Dar es Salaam ulitoa kura nyingi ukiwa wa pili. Wakapewa viti 2 - Halima Mdee, mwanasheria kijana ambae alijiuunga na CHADEMA mara baada ya kumaliza chuo kikuu na licha ya kuwa mfanyakazi wa serikali alikuwa akitumia muda wake kufanya kazi za chama mpaka pale alipopata likizo baada ya kuwa Mbunge. Nafasi nyingine ikaenda kwa dada wa Chuo KIkuu cha Dar, Susan Lyimo, na kila mtu anajua jinsi CHADEMA ilivyopata kura nyingi kutoka jumuiya ya chuo kikuu na umuhimu wa kufanya recruitment kutoka chuo kikuu.
3. Mkoa wa kigoma ulikuwa wa tatu kwa idadi ya kura kwa chadema. Wakapata kiti kimoja - Mhonga ruhwanya. Huyu baada t ya kumaliza chuo alijiunga na CHADEMA akiwa afisa maendeleo ya chama. Pia aliongoza katika kura za Kigoma.
4. Anna Komu - Unapokuwa na Mgombea mwenza mwanamke, halafu mnashindwa hawi makamu wa Rais, halafu hawi Mbunge, jamii ingawaelewa nini chadema?
Kati ya wabunge sita wa chadema wa viti maalumu, watatu elimu yao ni shahada za uzamili, mmoja shahada moja ya kwanza na wawili elimu ya sekondari. Hivyo nusu ya wabunge wanawake wa CHADEMA ni wasomi wa posgraduate, theluthi mbili wasomi wa ngazi yaa chuo kikuu. Hebu fuatilieni wa ccm muone.
Sasa mgongo mgongo, nakujua, ulitaka nani awe mbunge wa viti maalumu chadema? maana hoja hii umeishika sana wewe!
Ngoja nipumzike............. nisijerejeshwa hospitali