The power of failing successfully (Kuna nguvu katika kufeli kabla hujatoboa)

The power of failing successfully (Kuna nguvu katika kufeli kabla hujatoboa)

Joined
Apr 5, 2024
Posts
81
Reaction score
117
Habari wanajamvi,
Leo sina maneno mengi. Katika pitapita zangu nimekutana na concept moja inaitwa "How to fail successfully". Kwamba kufeli ni lazima, inategemea tu unaichukuaje, na unaishije baada ya changamoto. Ni hivi:

Failure as a Path to Success: (Kushindwa ni sehemu ya njia ielekeayo katika mafanikio)
  • Watu wengi waliofanikiwa walishindwa na kupata changamoto njiani. Thomas Edson alifanya majaribio (experiments) zaidi ya 1000 kabla ya kufanikiwa kutengeneza bulb za taa tunazotumia leo. Mengi alitoka katika familia maskini na kujaribu sana. Na mangi wengi wamepitia changamoto kadhaa kabla ya kunusa kilele cha ushindi.

    You never succeed more times than you fail (mafanikio yako kamwe hayawezi kuzidi idadi ya changamoto ulizopitia).

  • Attitude Toward Failure: (Mtazamo wako ni upi kuhusiana na changamoto/kushindwa).
    • Mtazamo hasi dhidi ya kushindwa kutafanya ushindwe kuvumbua njia ambazo hazifai. Kumbatia changamoto na kushindwa kama sehemu ya kujifunza. Kaa ngumu, kuwa mkakamavu.
  • Learning from Mistakes: (Jifunze kitu kila unaposhindwa)
    • Changamoto lazima zikupe uzoefu ambao hukuwa nao awali. Na mafunzo haya hayapo kwenye mitaala ya shule, au wosia uliopewa na wazazi wako. Failure is original, specific and tailored to your circumstances.
  • Failure vs. Identity: (Kushindwa kusiathiri utambulisho wako)
    • Jifunze kutofautisha kati ya mapito magumu na wewe unayepitia nyakati hizo. Usijiambie "mimi ni kilaza" kisa ulifeli mtihani.

      Mfano: nilisoma shule nchi jirani. Mtihani wa mwisho wa form 4 haukuenda vizuri. Alama zangu zilifaa kwenda chuoni, lakini hazikukidhi kozi nlotaka kuchukua. Mama mdogo aliyekuwa akinisomesha alinitia moyo nirudie shule. Huku nina divishen 2 inayoelekea kwenye 1. Nilimsikiliza.

      Mwisho wa mwaka uliofata, niliongoza darasa, nikapata 1 iliyoshiba, na nikafanya kozi iliyoridhisha moyo wangu. Wewe sio kilaza, umepata ajali tu usiyotarajia. Inuka, jifute, jaribu tena...
  • Failure Cultivates Qualities: (Kushindwa hujenga tabia)
    • Yeyote aliyepata changamoto au kushindwa lazima anyenyekezwe na tukio hilo. Ni wakati basi wa kusuka upya mkakati na mtazamo, itakayokusaidia kukua kiakili, kitaaluma na kimaisha.
  • Innovative Perspective: (Mtazamo wa kibunifu)
    • Jua hili: kila changamoto ni somo na fursa inayokusogeza karibu na kesho unayoitamani. Pambana, kazana, kuwa mbunifu. Jaribu kwa namna tofauti. Jaribu tena. Na tena. Iko siku... Anza tena na busara ambayo hukuwa nayo hapo awali.
  • Growth Mindset: (Mtazamo wa Kukua)
    • Changamoto ni mwalimu anayekushauri uwe na mtazamo chanya kila wakati. Maisha ni shule, wasemavyo wahenga, na shule hii hutahitimu hadi utakapolala mauti. Ukilalamika, itasaidia nini? ukitafuta mchawi ukamuondoa, utawajibikaje? Na, ukikimbia shule kwa kukata tamaa, inakuwaje sasa?

      Maisha siyo rahisi, na kila uzoefu unakupa fursa ya kuchagua. You either choose the pain of discipline, or the pain of regret. Chagua utungu wa nidhamu, au uchungu wa majuto.

      Fail successfully!
 
Back
Top Bottom