kili255
Senior Member
- Apr 12, 2018
- 100
- 184
Mkuu ufafanuzi makiniBizness ina watu wa aina mbili
1.Ndege, 2.Chura.
1.Ndege.
Ni watu wenye visiona na maono ya mbali. Anafahamu na kuona kwa mbali kuwa ule ni msitu, umeanzia hapa na kuishia pale.
Ndege huona hata nje ya msitu, huona bahari, hayupo limited na wapi anaona. Na vision zake huenda fasta sana.
Hujua vitu vingi sana, kwa kidgo kidgo. So utajua masoko, huduma nzuri kwa wateja, kuhifadhi fedha, uongozi nk
2.Chura.
Huwa ardhini, hawaoni pori lote kiujumla, hawaoni bahari wala nin, wanachokiona kipo limited. Lakini kile wakionacho mbele ukifahamu kiundani sana kuliko ndege.
Kama ni pori, akiona mti mmoj mmoja. Anajua ukubwa wake, mizizi yake na taarifa zote kiujumla, kuhusu mti
Sasa utakuta chura huyu anajua ujenzi, ni fundi mzuri, mchoraj mzuri, mkulima mzuri, lakina hana ujuzi na skillz zingine hana maono mengi.
Ila sasa akiwa na ndege akamuongoza, ndege huweza chukua chura kutoka miti tofauti tifaut, wenye taarifa za kutosha akatengeneza combo moja matata sana. Ikawa biashara kubwa.
So, usikomae kutafuta ujuzi mmoja, jua vitu vingi kwa kidgo kidgo, then utaanza kutafuta mtu anayejua sana kitu kimoja wapo kiundani, then Ona mbali jinsi ya kumtumia.
Mmiliki saluni, hajui kunyoa, lakini anajua taarifa nyingi kuhusu saluni, akamtafuta mjuzi wa kunyoa akajua kumtumia.
Mtaalamu wa upasuaji ni chura, mmiliki wa hospital ni ndege. Cheza na hizo mbinu mzeee
Sent using Jamii Forums mobile app