The reason Gaddafi was ousted..he intended to withdraw all of the Libyan oil billions from Europe

Sasa wengine wanasema hizo ni facts. Wengine wanatuambia sio kweli ni propaganda. Sasa sijui tumsikilize nani!!

Mkuu ni kawaida propaganda kuenezwa nje ya nchi husika utasikia wanamaisha mazuri na mambo kibao ni kweli wanaweza kuwa na maisha mazuri kulinganisha na nchi zingine ila sio kiasi hicho

Mf. Venezuela kipindi cha Hugo Chavez kweli walikua na maisha mazuri kiasi chao ila sio kwamba hawakuwa na shida kabisa nchi yote
 
Kwa Venezuela ni kweli kuwa jamaa alisaidia wananchi lakini haikuwa wote. Ilikuwa ni baadhi. Nilivyosikia nchi yenye mambo ya dezo dezo dizaini hizo kwa wananchi wake ni Brunei wengine wanasema Qatar.
 
Kama unapewa nyumba bure, elimu na afya bure na kwa $0.15 unanunua mikate 40 watu huko wanafanya kazi kwaajili gani? Wapate nini zaidi

Mkuu ina maana wewe usingefanya kazi kama hivyo vyote ungepata bure?Je hujui kuna watu wanautajiri wa kupindukia na wanafanyakazi kwa bidii sana ili waendelee kutoa msaada kwa wengine?Je unadhani ukipewa $ 50000 za kujenga nyumba huna haja ya kufanya kazi upate zaidi ili ujenge nzuri zaidi na ya kifahari?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Haina mchango kwa watanzania. Inawezekena wewe mleta mada hii ni pro-CCM ambayo imefanya yote haya yashindikane. Upuuzi mtupu kutuleta hapa.

 
Haina mchango kwa watanzania. Inawezekena wewe mleta mada hii ni pro-CCM ambayo imefanya yote haya yashindikane. Upuuzi mtupu kutuleta hapa.
I report you decide.
Kama majibu ya great thinkers siku hizi ndio hayo, pole sana
 
Dah....hii report imenigusa sana.Safi sana.
 
Ulitaka kufindisha nini na ripoti yako. Acha maswala ya kukopi na kupesti changanua hii hali inavyowezekana kwa tanzania na si kuweka tu alafu ukaishia hewani
I report you decide.
Kama majibu ya great thinkers siku hizi ndio hayo, pole sana
 
Waliwahi kuletwa wanafunzi UDSM kutoka Libya nadhani walikuwa kama 15 hivi,miaka ile ya mzee Punch.Walikuwa na nyodo kuzizd hata wanafunzi waliotoka Ulaya.Kwanza wakilikataa kula chakula Cafeteria wakidai hawana imani na nyama inavyochinjwa heti wanaogopa kula haramu,enzi izo hata na nyati walikuwa wanapikwa cafeteria.Ubalozi wa Libya ukawa unawaletea chakula maalumu kutoka ubalozini,kuanzia breakfast na vinginevyo.Baadae wakadai hawataki vyoo vya kukaa,wakaomba chuo kiwabadilishie vyoo vyumbani mwao viwe vya kuchuchumaa,chuo kilipokataa walikatisha masomo na kurudi kwa.
 
Ulitaka kufindisha nini na ripoti yako. Acha maswala ya kukopi na kupesti changanua hii hali inavyowezekana kwa tanzania na si kuweka tu alafu ukaishia hewani
Jifunze spelling kwanza kabla hujaposti chochote
 
Sasa wengine wanasema hizo ni facts. Wengine wanatuambia sio kweli ni propaganda. Sasa sijui tumsikilize nani!!

Libya ina vuna mapipa Milion 2.9 kwa siku na bei ya pipa la wese kwenye soko la dunia ni above $ 80

Ukipiga hesabu ni kuwa Gadafi alikuwa anaweka Hazina Dola Billion kadhaa kwa siku na Libyans wapo chini ya watu Million 7 tu

Kweli ningekuwa Libyan ningefurahia unipe elfu 50 ktk maisha yangu yote ili hali wewe a day unakunja billions?Gadafi asingepona ktk dunia hii ya facebook!

Waliokuwa wanafaidika na mafuta ya Libya ni wanajeshi wanao muunga mkono tu
 
Acha uongo
Kinachotokea sasa ni kundi la majambazi likifanya kazi ya kuuza mafuta na imefika wakati serikali ya libya ya sasa imebidi ikae chini na gang hilo ili waweze kuongea na kupanga jinsi ya kuuza mafuta hayo.enzi za gadafi haya hayakuepo
 
Kama hayo ni kweli kwanini WALIBYA WENYEWE walimpindua GADDAFFI walikuwa wamechoka hizo neema zote? naongezea fact nyingine, GADDAFI alimsaidia IDDI AMIN wakati wa ile vita yetu ya Kagera, something to think about for a true TANZANIAN!
 
Ni kweli kwamba Wa Libya walifurahia huduma za jamii nyingi sana zilizotolewa bure na serikali kwa namna ambayo huenda ilikuwa ni ya kipekee duniani. Tatizo kubwa lilikuwa kwamba hawakuwa huru, au hata kudiriki kuisema vibaya serikali, jambo ambalo lingekuletea hata kuuwawa. Ghadafi alitawala Libya kwa namna ambayo iliwafanya raia wote kuwa watumwa wake aliowapa zawadi nyingi kila siku. Libya haikuwa demokratiki chini ya Ghadafi, ambaye alikuwa ndiye polisi, mwendesha mashtaka, hakimu na mnyongaji.

Swali la kujiuliza ni moja; Je ni bora kuwa mtumwa wa tajiri kuliko masikini huru?

NI swali ambalo si rahisi kupata jibu moja.
 

Ni nature ya binadamu kuwa mvivu akipata chakula cha bure tu sasa habari gani apewe chakula, nyumba, elimu, afya na huduma zote hizo bure.. Achana na maisha ya matajiri wao tayari wana mzunguko endelevu wa vipato vyao tofauti na Libyans ambao mnasadiki walipewa bila kufanya kazi yeyote. Na tuseme waliendelea kufanya kazi ili wasaidie wengine kama unavyodai; sasa wamsaidie nani akati kila mtu anacho cha kupewa na serikali ama unataka sema walikua wanasaidia nje ya nchi yao
 
Haina mchango kwa watanzania. Inawezekena wewe mleta mada hii ni pro-CCM ambayo imefanya yote haya yashindikane. Upuuzi mtupu kutuleta hapa.

Utakua mgonjwa wa akili kama kila utendalo unataka lilete mabadiliko Tanzania
 

Mods wametoa icon ya LIKE anyway chukua LIKE toka kwangu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…