kweyamba_dave
JF-Expert Member
- Oct 2, 2012
- 961
- 483
Haina mchango kwa watanzania. Inawezekena wewe mleta mada hii ni pro-CCM ambayo imefanya yote haya yashindikane. Upuuzi mtupu kutuleta hapa.
Nimekusaidia sana kufikiri hata kama hutaki kusema.
Utakua mgonjwa wa akili kama kila utendalo unataka lilete mabadiliko Tanzania
Waliwahi kuletwa wanafunzi UDSM kutoka Libya nadhani walikuwa kama 15 hivi,miaka ile ya mzee Punch.Walikuwa na nyodo kuzizd hata wanafunzi waliotoka Ulaya.Kwanza wakilikataa kula chakula Cafeteria wakidai hawana imani na nyama inavyochinjwa heti wanaogopa kula haramu,enzi izo hata na nyati walikuwa wanapikwa cafeteria.Ubalozi wa Libya ukawa unawaletea chakula maalumu kutoka ubalozini,kuanzia breakfast na vinginevyo.Baadae wakadai hawataki vyoo vya kukaa,wakaomba chuo kiwabadilishie vyoo vyumbani mwao viwe vya kuchuchumaa,chuo kilipokataa walikatisha masomo na kurudi kwa.
Ni nature ya binadamu kuwa mvivu akipata chakula cha bure tu sasa habari gani apewe chakula, nyumba, elimu, afya na huduma zote hizo bure.. Achana na maisha ya matajiri wao tayari wana mzunguko endelevu wa vipato vyao tofauti na Libyans ambao mnasadiki walipewa bila kufanya kazi yeyote. Na tuseme waliendelea kufanya kazi ili wasaidie wengine kama unavyodai; sasa wamsaidie nani akati kila mtu anacho cha kupewa na serikali ama unataka sema walikua wanasaidia nje ya nchi yao
Kama unapewa nyumba bure, elimu na afya bure na kwa $0.15 unanunua mikate 40 watu huko wanafanya kazi kwaajili gani? Wapate nini zaidi
Huwezi judge nchi kwa kukaa week moja tu and likely ulikaa downtown tu kama ilivyo kwa wasafiri wengi pindi wawapo nchi za watu.
Nenda South Africa Leo kaa week Johannesburg downtown unadhani utasema kuna watu wanamaisha magumu south!? Na SA ina uchumi mkubwa kuliko Libya
Mkongwe umeongea vizuri na kuichambua ripoti ya libya kama vile ulikuwa ukiishi libya. Wanajuta na wameshapoteza dira ya umoja wao, Sasa nchi inayumba yumba "hawako huku wala hawapo kule" marehem col: Gaddafi alilewe utawala.ukweli ni kuwa jamii ya Libya inajuta kutokana na kukubali kuwa deceived na Westerns.yaliyotajwa si uongo wala si tambo za walibya ili waonekane wanamaisha bora.demokrasia ndiyo imeizika Libya ni jamii iliyokuwa na kiu ya kumuona mtu aliyekaa kwenye madaraka kwa miongo zaid ya minne akiachia madaraka.muamar alikula na vipofu bila kuwashika mkono ila kelele za majirani tena wale wa mbali zilishambulia maskio ya vipofu wale.walibya hawakujua kuwa gadafi ndiye mpishi wa yale yote,hawakujua kuwa ilihitaji mtu asiyejua kuwa pesa hazina mwisho.
jamii hii haijawahi lalamika juu ya huduma za jamii ilizipata kila ilipohitaji walilalamikia democracy.takwimu zilionyesha raia wa Libya wanaishi vizuri kuliko wa marekani.
Exactly Nyani Ngabu,kumbe tulikuwa wote UDSMOh yeah nawakumbuka sana hao jamaa. Ilikuwa miaka ya 86/87. Baadhi yao kama siyo wote, walikuwa wakiishi kwenye guest house moja hivi pande za Sinza.
Walikuwa wakikatiza tulikuwa tunawashangaa sana. Tulikuwa tunawaona sijui ni watu wa wapi tu.
Libya ina vuna mapipa Milion 2.9 kwa siku na bei ya pipa la wese kwenye soko la dunia ni above $ 80
Ukipiga hesabu ni kuwa Gadafi alikuwa anaweka Hazina Dola Billion kadhaa kwa siku na Libyans wapo chini ya watu Million 7 tu
Kweli ningekuwa Libyan ningefurahia unipe elfu 50 ktk maisha yangu yote ili hali wewe a day unakunja billions?Gadafi asingepona ktk dunia hii ya facebook!
Waliokuwa wanafaidika na mafuta ya Libya ni wanajeshi wanao muunga mkono tu
Umekosea jukwaa, ulitakiwa uende jukwaa la mapishi. Huku sio kwako
Inamaana wewe ungekuwa mmoja kati ya NTC? Sidhani kama hadi leo usingejutia uamuzi wako.kumbuka serikal ya Libya imejitahidi kuwekeza kuliko karibia serikali zote kama sio zote kabisa ndani ya Africa.gaddafi alijua kunyanyuka bila kushikwa na magharibi inawezekana na ndio maana alitoa wazo la USA kubwa kwa maana ya united states of Africa.hawakupewa elfu 50 kama ulivyosema bali walipewa dola elfu 50 around 75 millions za kitanzania.walipewa mahari kwa kila kijana anaeoa.mambo hayo hata America hawajayafanya.ni nchi ipi iliyofikia hatua yakudistribute wealth directly kiasi hiki kwa raia wake? Hata siku moja sijawahi kusikia walibya wakilalamika kuwa gaddafi alikuwa fisadi...baadhi ya mawazo ni yale yaliyosemwa na midomo ya waamerika kama anavyosemwa hasad leo hii na Obama.tunagesi songosongo tunaye rais kikwete iwapo gesi hiyo itasaidia japo kujenga nyumba ya kuishi wazee nitafute nina zawadi yako.
Yapo mataifa mangapi yaliyoshindwa kufanya aliyoyafanya gadafi? Congo wana utajiri kiasi gani? Nani anaufaidi? Tanzania tuna utajiri kiasi gani na nan anaufaidi?
Nadhani ukimpinga gadafi ni kuwasha taa ya hatari kwa rais wetu..tehtehteh natania utendaji wake n mzuri anatulisha kama gadaffi alivyofanya kwa raia wake
Jifunze kuandika vizuri kwanza kabla hujaanza kuleta hoja zako.Wewe Jamaa inaonekana unaongea vitu kwa ushabiki na hisia tu. Mimi sijawahi ona mtu anayefanya vizuri alafu anashambuliwa na jamii hiyo anayoifanyia mambo mema. Gaddafi unayemsema alikuwa ameigwa libya katika vipande walioajiliwa ni watu wa kabila lake na wengine walipewa viposho tu vya kujikimu huyo ndo mtu unataka kutuaminisha kuwa ni mwema kafanya mazuri.
Hilo siyotatitzo: Ulitakiwa uisome libya then utuambie njia ya kupita ilitufike huko unapopasema na siyo hizi takataka kutoka kwenye magazati ya Udaku.
Ila nimeendelea kuelewa akiri zako zilipo ila sitataja kama mtu mmoja alivyawahi kusema kuhusu wabunge wa dar.
Jifunze kuandika vizuri kwanza kabla hujaanza kuleta hoja zako.
Again, umekosea jukwaa. Ulitakiwa uende jukwaa la mapishi. Hapa sio kwako. Gracias!
Gaddafi alianza kuongelea US of Africa baada ya kukorofishana na mataifa ya kiarabu kwa hiyo huku ndo palikuwa pa kutokea kwa warafi. Kama unakumbuka vita ya kumtoa mataifa ya kiarabu yalitoa mchango mkubwa sana kuhakikisha anatoka madarakani kwa hiyo alikuwa kero tu. Hajawekeza popote Afrika ila kajenga misikiti.
Watu wa aina yako kwenye lugha ya wenzetu wanaitwa "puta"Watu wa aina yako wana jina kwenye lugha ya wenzetu. Wanaitwa " Penny wise Pound Foolish"
Huwezi kutolewa sehemu kwa kuwapa huduma nzuri raia wako acha story za vijiweni