The reason Gaddafi was ousted..he intended to withdraw all of the Libyan oil billions from Europe

The reason Gaddafi was ousted..he intended to withdraw all of the Libyan oil billions from Europe

Idd amini aliishi Libya na kufia huko?ama kweli huna ulijualo.Amin aliishi Saudi Arabia na ndipo mauti yalipomkuta.
Naweza kusema idd Amin alikuwa mtu wa bahati kutokana na Mahakama ya The Hague kumsahau mpaka alipofariki hakuwa ameshitakiwa kabsa.
 
Leo hii Benard Membe akisikia Gadafi kafufuka au Serikali ya Libya inakuja kudai mali na mapesa ya Gadafi sanjari na kukichunguza kifo cha balozi wa libya aliyekufa kimaajabu , hii ikitokea Tanzania lazima Membe atazimia Kwa pressure na kwenda kutibiwa India miaka 13 Kama Yule mtumishi wa Serikali anayesoma Japan Kwa miaka 13 Sasa .
 
Dah Libya si ilikua pepo hapa duniani ,ilikua na tofauti gani na Luxembourg ama Brunei ?
R.I.P Ghadafi japo ulikua na mapungufu yako lakini ulikua ni kiongozi mwenye maono ya kipekee
 
Sasa wamepisha wengine watawale lakini Nchi imekuwa sehemu ya mauaji hakuna raha tena wala huduma Zile zilizokuwa zikipatikana Kipindi cha Gadafi .
Yote yamesababishwa na Gaddafi kutotii mamlaka ya wananchi. Kama angeitisha uchaguzi, wakachagua, basi yote yanayotokea yadingetokea.

Kitendo cha Gaddafi kuruhusu vita, kuna watu waliuwawa. Sasa baada ya vita mtu amepoteza ndugu zake, amechanganyikiwa naye anataka madaraka.

Halafu ule usemi wa "...human creat seeds of their own destruction..." Ulitimia Libya kwa Gaddafi.

Kama unakumbuka, Gaddafi aliingia kwa kumpindua mtu na alikuwa na mass support. Baada ya mapinduzi, hakuanzisha sheria ya kudhibiti silaha mikononi mwa raia. Libya kununua smg kadhaa na risasi ilikuwa rahisi ktk utawala wa Gaddafi.

Idd zote walisherehekea kila mwenye bunduki kwa kupiga risasi hewani. Au mtu akifurahi, anaingia ndani anachukua silaha anaanza kupiga risasi. Hii pia ilimgharimu mjomba wako Gaddafi
 
Hakuna kiongozi kama Gaddafi,sio Libyans pekee watakao jutia kifo chake bali Africans kwa ujumla tutajutia unafki wetu.
Alikuwa na ndoto nzuri ju ya Africa but America turned it to nightmare
 
Damu ya Gaddafi itawatafuna sana raia WA Libya mpaka pale watakapofanya toba ya kwel. Pamoja na mapungufu yake ila alkua ameijemga nchi yake vzr.
 
Wewe inaonekana hajui chochote kuhusu Libya hakuna kabila linaitwa mabedui ni watu was mashambani hats hapa tunaye sasa hivi bedui
libya kama wewe hutoki kabila la wabedui ulikuwa huluhusiwi kua kiongozi lakini pia aliwakandamiza sana wananchi wake kihisia....katika maisha kitu cha kwanza ni uhuru...jiulize kwanini watumwa wa marekani na kwingine walidai uhuru kwani walikua hawali wa kunywa....jiulize kwanini wewe mwenyewe haupendi kuendeshwa na wazazi wako...
 
Binadamu haturiziki hata wangepewa nn bd baadh wangempinga tu....
Ndio maana Afrika tutabak masikin tu
Watu wamepewa maisha bora bd tu hawariziki hata wangedai uhuru wao wangefanya harakat kidogodogo tu sio km walivyofanya hata ingechukua miaka kadhaa wangeupata tu uhuru kwa aman
 
kwa kweli kama haya yote uyasemayo ni kweli mkuu @mzizimkavu,mwenyezi mungu aiweke roho ya gadhafi mahali pema peponi
 
Ni hulka za kibinadamu kutaka uhuru uliopitiliza unadhani wangejua kwamba matokeo yangelikuwa ni haya wanayoyaona leo wangekubali kumpindua gadafi thubutuu!
 
Suala sio unapewa nini ktk nchi yako, bali ni kwa kiasi gani nyote mna nafasi sawa za kimaisha ktk nchi yenu. Gaddafi hakuruhusu uhuru huo japokuwa aliwapatia huduma nyingi bure.

Mzizi, hata wewe akitokea mtu akasema anakupa kila kitu lkn usijihusishe na harakati mbalimbali za maisha utakubali?

Walibya sio wajinga, kumbuka waliitwa ni mende na panya.

Leo hii naamini kama Gaddafi angekubali kuitisha uchaguzi baada ya kufanikiwa yote hayo, angekuwa mtu maarufu zaidi duniani. Lkn kwa uroho wa kutawala yeye na familia yake, alipuuza sauti zilizodai uhuru wa kisiasa. Ni kosa kubwa sana
Kwani libya hakukuwa na Uchaguzi
 
Ni hulka za kibinadamu kutaka uhuru uliopitiliza unadhani wangejua kwamba matokeo yangelikuwa ni haya wanayoyaona leo wangekubali kumpindua gadafi thubutuu!
Walikuwa wana beep walichonacho..angalia mijengo yao ilivyobaki magovu na wanavyotapa pata na nchi sasa hivi.Kila mara kuvuka na Boti kwenda Italia na kuitwa wakimbizi.Angalia jinsi wanavyokufa Mideterenia kuhangaikia tu kutafuta maisha.Uhuru duniani hakuna hakuna kabisa.Fikiri Mungu alipoumba ulimwengu aliweka masharti ya kuishi bustanini si unaona kilichotokea kwa Adamu na Hawa?Binadamu hajawahi rizika hata umbebe,umpeleke chooni umchamb....umuogeshe umlishe ..vyote atasema hujafanya vizuri...Sasa Libya wanapata UHURU WAO WALIOUHITAJI.
 
Kilichomuua Gaddafi sio hicho. Hayo ni mema yake aloyatenda. Kanali aliuawa kwa sababu aliwahi kusaidiana osama bin laden kueneza ugaidi. Pia aliwahi kuangusha ndege kule lockaby, scotland. Amehusishwa na kueneza ugaidi na kwa njia za ujenzi wa misikiti inayofunisha radicalism..na kwa tanzania yeye ndiye aliyemsupport nduli idd amini dada wakati wa vita ya mwaka 1978/79. Dege lake la kivita likiwa na askari wenye ujuzi wa juu wa kivita lilidunguliwa kilimanjaro airport.
Nchi yake ilikuwa na mafuta na wazungu hawakupenda matumizi yake ya uchumi w mafuta.
Gaddafi alikuwa na mema yake na mabaya yake! Haikuwa sahihi kumuua kwani alistahili haki ya kuishi!
 
Hukuwahi kusikia mtu anamps mke wake kila kitu lakini kitenfo cha kumbana asitoke nyumbani kujichanganya na wenzake, kunamfanya mwanamke anakuwa kituko na Uhuru ni kila kitu! Mpe mtu kila kitu halafu mnyime uhuru uone kitakachotokea!
 
Yote yamesababishwa na Gaddafi kutotii mamlaka ya wananchi. Kama angeitisha uchaguzi, wakachagua, basi yote yanayotokea yadingetokea.

Kitendo cha Gaddafi kuruhusu vita, kuna watu waliuwawa. Sasa baada ya vita mtu amepoteza ndugu zake, amechanganyikiwa naye anataka madaraka.

Halafu ule usemi wa "...human creat seeds of their own destruction..." Ulitimia Libya kwa Gaddafi.

Kama unakumbuka, Gaddafi aliingia kwa kumpindua mtu na alikuwa na mass support. Baada ya mapinduzi, hakuanzisha sheria ya kudhibiti silaha mikononi mwa raia. Libya kununua smg kadhaa na risasi ilikuwa rahisi ktk utawala wa Gaddafi.

Idd zote walisherehekea kila mwenye bunduki kwa kupiga risasi hewani. Au mtu akifurahi, anaingia ndani anachukua silaha anaanza kupiga risasi. Hii pia ilimgharimu mjomba wako Gaddafi
Ujinga wa ukasuku na kugeuka panya wa Mpiga Filimbi wa Hamelin. Hatuwasikii hapa mkisema ubaya wa Wazungu walivyofanya Afrika kuanzia Algeria mpaka Cape Town. Nyie mkisika waarabu (Your Bougey Man) basi maskio yenu yanasimama kama mabua ya mahindi waafrika kila ovu wamefanyiwa na wazungu na bado hamkumbuki wala kujiskia vibaya eti Bwana Yesu ametufundisha kusamehe. Bwana Yesu hakufundisha kusamehe watu maalum. Ujinga wa kupokea tu yale unayoambiwa kwa sababu CNN na Fox News ni Wazungu. Kweli basi yule Mzungu Donald Trump anaposema akichukuwa madaraka atawabeba na atawatupa viongozi kadhaa korokoroni na kurudisha ukoloni Barani Afrika.

Sent from my HTC Desire 820s dual sim using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, usiweke udini, chambua hoja kisha ijibu. Kwani waliomuua Gaddafi ni wazungu au walibya wenyewe?

Waliomkata al islam kidole cha mkono wake ni wamarekani?

Na wanaoendelea kupigana pale kudai uhuru wa kisiasa, ni wazungu?
 
Dah Libya si ilikua pepo hapa duniani ,ilikua na tofauti gani na Luxembourg ama Brunei ?
R.I.P Ghadafi japo ulikua na mapungufu yako lakini ulikua ni kiongozi mwenye maono ya kipekee
Kwa kweli enzi hizo Libya ilikuwa iko juu sana kwa maendeleo, nilikuwa sijawahi kuona walibya wakiondoka nchini kwao kutafuta maisha kwingine zaidi ya kwao.
 
Back
Top Bottom