..Morogoro mji, au Morogoro mkoa?
..Sgr italeta mabadiliko gani ambayo barabara na Tazara zimeshindwa kuyaleta Morogoro?
..Morogoro ni mkoa wenye potential kubwa ili serikali imeshindwa kuuwezesha na kutumia ipasavyo.
..Badala ya kupoteza fedha kujenga mji wa serikali Dodoma naamini tungefaidika zaidi kuwekeza ktk kilimo na viwanda Morogoro.
Nimekusoma mkuu 'Jokaa', ila hapa naona unataka mjadala mpana tu, ambao nakubali utakuwa ni mjadala wa manufaa, siyo kwa Moro (Mkoa/Mji) pekee, bali kwa sehemu zote nchini Tanzania.
Kila sehemu ina 'potential' zake; na kote huko najuwa /natabiri tutakubaliana lawama inalala wapi, serikalini.
Mleta mada, kajikita kwenye Morogoro mji, lakini Morogoro mji hauwezi kutenganishwa na Moro mkoa. Neema ya mji, ni neema ya mkoa.
Hili la SGR na barabara; siku hizi kila nisomapo kuhusu haya mambo ya maendeleo yanavyopatikana sikosi kuona msisitizo kila sehemu juu ya umuhimu wa nyenzo hizi katika kuleta maendeleo ya eneo lolote. Kwa sababu hiyo, ndiyo maana nikaona Moro (mji/mkoa) inayo hudumiwa na njia hizi za mawasiliano itakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi kuzitumia kupata maendeleo. Uwepo wa miundo hiyo huko siku za nyuma iliyoshindwa kuinufaisha Moro (kwa kutokuwa tegemewa), hakuna maana hata hii mipya itashindwa kuleta huduma ya uhakika ili watu wa Moro wanufaike na miundo mbinu hiyo .
Kama tunavyo kubaliana sote, Moro ni mkoa/mji wenye 'potential' kubwa, kwa sababu mbalimbali; moja wapo ikiwa hiyo yakuwa na ardhi nzuri kwa kilimo, lakini pia kama tunavyojadili hapa; kwa "mahali ilipo" katikati ya majiji mawili makubwa, yenye uhitaji mkubwa wa bidhaa zinazozalishwa na Moro (mkoa/mji). Lakini pia 'potential' hiyo inatokana na "huduma" nzuri za usafiri zinazo patikana hapo Moro (mkoa/mji).
Mikoa ya Ruvuma, Iringa, Mbeya, Katavi na Rukwa imevuma sana katika kilimo. Sasa sijui tofauti iliyopo kati ya mikoa hiyo na Moro juu ya uhusika wa serikali kwenye shughuli za kilimo. Inawezekana Moro imesahaulika (sijui) na serikali?
Ili nisiandike gazeti refu sana la kukuchosha kusoma, ngoja nimalizie kwa kueleza kwamba hoja yako hiyo ya mwisho juu ya "...badala ya kupoteza fedha nyingi...", hili sikubaliani nawe moja kwa moja. Kuna mambo mengi sana ya kipuuzi yanayotumia hela za walipa kodi kuliko hili ulilolikazia wewe. Mfano, haya mapikipiki yanayogharamia pesa Tsh 54 bilioni...; na huu ni mfano mmoja tu, tena mdogo sana.
Utanisamehe, sikuweza kufupisha hili andiko uweze kulipitia kwa dakika moja, kwa sababu nilitaka nieleweke.