<br />Ghadafi aliijenga Libya na kwa ulevi wake wa madaraka amebomoa alichojenga! Mimi nikiambiwa nichague mtawala mwenye busara kati ya Ghadafi na Mubarak nitamchagua Mubarak. Hata kama aliondoka baada ya shinikizo kubwa la wananchi wake,lkn angalau aliona Misri ni kubwa kuliko urais wake,familia yake,marafiki zake na chama chake. Na kwa hali halisi ilivyo sioni kama utawala wa Ghadafi utadumu miezi 2 kuanzia sasa. Wanachofanya waasi kwa kusaidiwa na NATO ni kulivuta nje ya Tripol jeshi lake kwa kupigana ktk fronts nyingi. Mwisho waizunguka Tripol. Baada ya hapo mambo mawili yanaweza kutokea. Moja ni kwa wananchi waliopo Tripol kuandamana na kuuangusha utawala wa Ghadafi,pili ni vita ya umwagaji damu mkubwa ktk mitaa ya Tripol kati ya waasi na jeshi la Ghadafi.
<br />
hupaswi kulaumiwa kwani habari unazopata ni za CNN,BBC na Aljazeera. Kwa taarifa yako Gadaf anakubalika sana Libya kwa misimamo yake ya kutetea rasilimali za nchi, pia yuko vyema sana ground war, hivyo waasi na waroho wa mafuta Nato bado wana kazi kubwa kumng'oa Gadaf.