Waafrika mnaniacha hoi. Hata hapa kwetu wapinzani kama Chadema wakiandamana kwa amani wakidai haki wanaitwa wahuni, kisa ? wanaipinga serikali kandamizi ya CCM iliyoko madarakani na vyombo vyetu vya dola viko tayari kutumia silaha za moto dhidi yao. Wananchi wa Libya hawa tunaowaita wahuni na waasi walianza kwa maandamano kwa kuchoshwa na utawala wa kidikteta na tulishuhudia Gadafi, bila huruma, alivyoamuru washambuliwe na hata kuuawa.
Nakumbuka washabiki wa Gadafi walivyowabeza waasi kuwa hawatafanikiwa na kwamba Libya si sawa na Misri, hadi wengine wanaomtetea hivi sasa kudai hawaungwi mkono na Walibya. Nakumbuka matambo ya mtoto wa Gadafi, nakumbuka silaha zilivyogawiwa kama njugu kwa raia wa kawaida eti kuilinda Libya na kumlinda Gadafi. Ni mataifa ya Kiarabu ndio yalikuwa ya kwanza kuomba umoja wa mataifa kuingilia kati kuwaokoa Walibya dhidi ya muuaji Gadafi.
Tanzania kama kawaida yetu tulikaa kimya. Sasa tupende tusipende utawala dhalimu wa Gadafi umefika ukingoni na kutambua ama kutotambua kwetu tunaowaita wahuni ni kutoa machozi ya samaki. Wimbo wa Walibya wanatumiwa na nchi za magharibi ni wa kipuuzi kwa sababu Gadafi kakaa madarakani miaka 42, hizo nchi zilikuwa zinasubiri nini muda huo wote ? Membe anajua kuwa kuitambua Libya kutawaongezea Watanzania hamasa ya kuitosa CCM.
Poleni wapenzi wa Gadafi lakini imekula kwenu, utawala wa Gadafi na familia yake umefikia kikomo na sasa Libya itaweza kupumua tena. Sisi tulioshuhudia Gadafi akimuunga mkono Idi Amin kutushambulia Watanzania, tunasema good riddance kwa huyu mlevi wa madaraka. Ilifikia hatua alikuwa anapanga hata kujipachika cheo cha mfalme wa Afrika na kweli wapo weusi wenzetu walikuwa wapo tayari kuuza utu wao kwa tamaaa ya vijisenti vya Gadafi.