askari kanzu alikuja na mashamsham na vurugu akiwa habari kuwa mtoto wa Gadaffi sheikh Khamis ameuwawa.
lakini kamanda Nonda akamtuliza chini kisha akampa ushahidi kuwa Sheikh Khamis yuko hai na Salama.
Kesho yake Channel zake zikamuonyesha kisha akapotea nywiiii kama Konokono aliyemwagiwa chumvi.
Then ktk kupitapita kwake huko akatujia na Habari kuwa watoto watatu watukutu wa Kiongozi wa Libya anayetambuliwa mpaka na Mungu yaani Kanali Gaddafi wamekamatwa.
Then Kama kawaida GENERALI Nonda akamtuliza chini kisha akamueleza ukweli kuwa watoto wako hai na hawajakamatwa na Mbwa koko yeyote.
Na haikuishia hapo makamanda wakaonekana ktkt ya Tripoli wakiwa na mamia kama si maelfu ya wapambanaji wakiwa wenye afya njema.
then ndugu yako Askari kanzu akaingia chaka na kukauka nywiiiiii kama duduwasha aliyedokolewa.
Hakuishia hapo ndugu yangu huyu askari kanzu akakurupuka tena na habari za kuuawa kwa mara ya pili kwa Khamisi Gadaffi, ila safari hii hakuna aliyehangaika nae kwani nahisi siku ileile Khamisi alijitokeza na kumuumbua.
Baba huyu kahuishia hapa kwani alikuja kivingine na kisha akaanzisha Thread inayosema kuwa ''GADAFI KWISHA HABARI YAKE...WAASI SASA WAMEMZINGIRA''...
Tangu mwezi huu umeanza Gadaffi kazingilwa mpaka leo, na ndugu yangu askari kanzu sijamsikia kufumuka tena kutueleza kuwa Ghadafi amekimbia au bado kazingirwa.
So kwa kifupi mi nikionaga posti ya Askari Kanzu kwanza huwa nacheka then namkumbuka Al-Saaf yule waziri wa Habari wa Serikali ya Hayati Rais Saddam Hussein al-tikrit.
Kwani style zao za porojo ni mlemle yani