jambotemuv
JF-Expert Member
- Feb 7, 2008
- 224
- 62
Nilidhani waushangaa unafiki wa NATO na US kumbe waushabikia. Ulianza vizuri kuwa walidhamiria kwa kila hali kuhakikisha wamemuuwa Ghadafi na hata ilipovumishwa kuwa mwanaye kauwawa walishangilia. Leo kudai wataka kujichunguza ni jinsi gani walimuua Ghadafi yapaswa kuwa na nia nyingine tofauti na watamkayo.
Ni mojawapo ya hatua za kuhakikisha pia miongoni mwa waasi mpasuko mkubwa unajengeka ili wabaki kuuana wenyewe huku walowezi wakijichotea hazina za wa Libya bila tabu. Wanaitengeneza Ruwanda, Burundi, Kongo nyingine kama walivyozoea.
Kama twaombea Mugabe na wengine kutolewa madarakani na wapuuzi wa ulaya na marekani ni udhaifu mkubwa. Miaka yote wakidai Mugabe kakaa madarakani muda mrefu hawakuwahi kusema lolote juu ya Mubaraka zaidi ya kumuita mshirika wao na kumpa misaada mingi ya kijeshi. Huko Moroko wanakojichotea Phosforus wapendavyo hawasemi mfalme katawala miaka mingi.
Hivi Malkia alichaguliwa kidemokrasia kiasi gani na walipa kodi wa Uingereza hata kuhalalisha kuwepo madarakani mpaka ajifie?