The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

Mbona wamekuwa kama nyuki,kila nchi ya kikafiri imetuma midege yake.Hii yote ni no fly zone?.Iwapo wamekwenda mbali kuliko kutekeleza azimio la UN Ghadhafi alalamike wapi?.
Baada ya Libya Saudia itafuata.Visingizio vitakavyotungiwa maazimio ya UN havikosekani.Urafiki wa Saudia na US kuuziana takataka za kijeshi unaweza kubadilika usiku mmoja tu.
Allah atajibu.
 
iNGEKUWA ENZI YA BUSHI MAREKANI MBONA HUYU GADDAFI ANGEKUWA KASHATINDULIWA ZAMANI
 
Huyu mwehu anaweza piga watu wake mwenyewe kisha akanyooshe vidole allied forces!
 
Wewe unaongea kuhusu ukafiri na wakati Saudi huko nchi takatifu yenu wanasapoti na hata hizo silaha wako tayari kuzitumia dhidi ya asiye kafiri mwenzenu?
 
dah naona wakubwa wameamua kufanyia mazoezi ya midege yao kwa ghadaffi.
 
Naheshimu maoni yako lakini all in all Libya belongs to all Libyans, and not only to Gadhafi and his sons. Wananchi wametaka mabadiliko, alichotakiwa ni kuwasikiliza na kukaa nao chini, lakini aliamua kuwauwa na hayo ndio matokeo yake.
msnbc wanadai Gaddafi ku address Nation any time.
Back to the point,na mimi pia nayaheshimu maoni yako,hata hivyo nilidhani hasara ya vita ni kubwa zaidi kwa wananchi hao na Taifa lao....Na pia kudai kuwa unawatetea wananchi hao maslahi yao na huku unawatandika mabomu na kuwadisplace kwa mwananchi wa kawaida ataona maruwe ruwe tu.
Longterm consequences ndicho nilimaanisha,achilia mbali zile short term ama imediate ones ie loss of lives.
 


Kwa hiyo hata UAE na hizo nchi nyingine za kiarabu zinazoshirikiana wa the west ktk hii operesheni na makafir?
Ghadafi anatakiwa akalalamike kwa China, Chavez na Ahamedinajad. Hao ni maswahiba wake kinaoma lakini wameuchuna na kuufyata. Nilitegemea wangemsaidia kijeshi. Inamaanisha nini ama akina Chavez na wenzie ni marafiki wa wakati wa raha tuu?
 
Ni kweli Gadaffi amewafanyia wananchi wake yaliyo mema, lakini kwa kujiinua nafsi yake juu ya Mungu wa Israel hapo alipolitukana taifa la Israel na kuikashifu biblia alipokuwa uganda aliyafuta yoote mema ikiwa aliwahi kuwa nayo.
Na iwe kwake kama ilivyokuwa kwa mfalme Nebkadneza alipojiinua na kujivuna kwa kiburi chake juu ya Mungu wa Israel.
Aliondolewa fahamu na kutiliwa akili za mnyama wa pori na kuishi porini miaka saba.
Gadaffi nayampate makuu kuliko haya. Sii kama nitakavyo mimi bali mapenzi yakoo ee Mungu yakanitangulie kwa hili.
.
 
Mbona wamekuwa kama nyuki,kila nchi ya kikafiri imetuma midege yake.Hii yote ni no fly zone?.Iwapo wamekwenda mbali kuliko kutekeleza azimio la UN Ghadhafi alalamike wapi?.
Allah atajibu.
Kwa "ukafiri" una maanisha nini?
 
Mkuu kumbuka hii ni Operation ya NATO na Arab League countries so nchi zote zilizo chini ya NATO zinashiriki in one way or another kuna watakaotoa ndege wengine bases (Malta na Italy), wengine watasaidia logistics na maswala kama hayo.
 
Mkuu kumbuka hii ni Operation ya NATO na Arab League countries so nchi zote zilizo chini ya NATO zinashiriki in one way or another kuna watakaotoa ndege wengine bases (Malta na Italy), wengine watasaidia logistics na maswala kama hayo.

Ofcourse mkuu,kwani NATO si mataifa tu?Sasa unategemea wataacha kuenforce interests zao za kibiashara mara baada ya kumwondoa Gaddafi?
Hawajitolei bure.
 
hizo ndege zinaweza kukutana na SAM na anti aircraft artillery kutoka kwa Gaddafi maana ana hizi hapa ambazo zinaweza kumsaidia












 
Pentagon wansema Libyan Leaders and Govt are not targets....Na Gaddafi yuko onair now!Anaweza kuwashangaza wengi wenu humu...Teh teh teh!Hata hivyo Gaddafi haonekani live,bali ni sauti tu.
Source:msnbc news
 
ngoja wafundishwe-hao ndo wanaoweza kuwanyoosha hao ambao wanajiita si makafiri-Saudia haitafwata-Iran ndo itakayo fwata-wait and see
 
Security council si Arab League nor OIC......sikuwa nazungumzia Security Council bali Arab League

Arab League hadi baada ya Sarkozy na Clinton leo hawaungi mkono military intervention,wanachotaka ni no fly zone to protect civilians,westerners wanawatumia tu but msimamo wao haujabadilika

BTW: am not trying to answer....i know what am saying! :washing:
 
Gaddafi anasema wananchi wa Libya wanaomba msaada wa mataifa ya Afrika,ya kiarabu na kiislam kuwasaidia dhidi ya uvamizi wa crusaders.Anadai wanapigania uhuru.
 
Kwa mantiki hii potofu ina maana kuna makafiri kibao Africa?
Itakuwa hivyo mkuu,
back to the topic,Gaddafi katoa statement...Gaddafi anasema wananchi wa Libya wanaomba msaada wa mataifa ya Afrika,ya kiarabu na kiislam kuwasaidia dhidi ya uvamizi wa crusaders.Anadai wanapigania uhuru....Nadhani pia ana imply uislam uko under attack kama cjakosea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…