Nasikitika hata sisi wana wa Afrika hatujijui sisi ni akina nani na Gadafi ni nani. Kweli Gadafi kakaa madarakani kipindi kirefu. Je, ni kweli wananchi wake hawampendi? Hawa waasi kwanini watokee mji mmoja tu Bengazi na sio nchi yote? Gadafi ndio mwana- wa Afrika pekee anayewasumbua "Wamagharibi". Ni Gadafi pekee mwenye kuutetea Umoja wa Waafrika (Watu Weusi) - kumbuka yeye ni Mwaarabu! Bahati mbaya kabisa Gadafi anautetea Uislamu kumbuka sio Al-Kaida - na hili hasa ndio kinamponza ukiachilia mbali utajiri wa mafuta wa Libya. Kwanini - Wamagharibi wasiende Ivory Coast, Yemen, Baharaini, na kwingineko Arabuni - wanakufa wananchi huko. Inamaana Marekani inauchungu sana na waLibya kuliko wa weusi wa Ivory Coast? Je, wanaouwawa na majeshi ya Ushirika wa NATO sio raia wa Libya? Je, Califonia au Texas wangeasi na kutaka kujitenga Obama asingeingia kijeshi huko? Kumbuka: Tunisia, Misri na kwingineko Arabuni ni Uasi wa Umma na ndio maana Wamagharibi hawataki kupeleka jeshi. Uasi wa Libya ni wa kupandikizwa. Gadafi ni chambo tu! Mwana JF - naomba ufungue masikio na macho yote. Usiangaliea masuala haya kwa kengeza au kwa uziwi tafadhali.
RA
Sikushangai. Nahs umebebwa na fkra za knyonyaj, umetawaliwa tangu babu yake babu yako na bado hutak kuwa huru... Hv lini Afrìca tutakuwa "sisi"
Muafrika na muanzilishi wa AU anashambuliwa na raia zake wanauliwa na waAfrika wengine wanachekelea na kuona raha.
Wanadanganywa na "media" kabla ya mashambulizi kuwa Ghaddafi anaua raia zake, na mijuha mingi inakubali.
Wamesahau "crusade" aliyoitangaza Bush! Na wamesahau wamerekani walivyozuwa na kudanganya kuwa Iraq kuna silaha za maangamizi.
Waliosahau na wanaofurahia wanajulikana ni kwa nini wamesahau na ni kwanini wanfurahia haya yanayojiri.
Wakumbuke nguvu ya "crusade" haikushinda miaka na vikaka, itashinda sasa. Kumuuwa Saddam au Ghaddafi si ushindi ni ushindwa. Kwa mwenye kuelewa ataelewa na punguwani atabaki kuwa punguwani.
kumbuka kabla ya UN kupitisha NO FLY ZONE ilizingatia mambo matatu na mawili yalitimizwa ikiwemo
1.Kupata ridha ya ARAB LEAGUE 2.uvamizi kutovunja sheria 3.kupata ridhaa ya AU.
namba moja na mbili yalitimizwa kwa hiyo UN (France na washirika) wama exercise kijeshi ombi la waarab
Yote tisa,kumi ukweli ni kwamba,mataifa ya ulaya pamoja na marekani yako kimaslahi zaidi! Sidhani kama kweli wana uchungu na raia wanaokufa bila hatia. Kama ni kweli wana uchungu, basi nadhani wangetuma ngege za kivita plus askari wa nchi kavu sehemu nyingi tu za dunia zenye machafuko na hasa kipindi kile cha mauaji ya halaiki ya Rwanda na Burundi.
Pamoja na hayo, nchi nyingi za kiarabu zimekua zikiangaliwa kwa karibu sana na nchi za magharibi! Hii ni kutokana na neema ya mafuta waliopewa. Mbaya zaidi raia wengi wa nchi hizi ni wenye imani ya kiislamu,ambayo haikubaliki na mataifa haya ya magharibi na imekua ikibigwa vita kwa visingizio vya kila aina(ugaidi,siasa kali n.k)
Takwimu zinaonyesha Gadafi ni moja kati ya viongozi wachache shupavu duniani na amefanikiwa sana kuingoza Libya na hatimae kuwa na uchumi Imara. Nguvu ya umma iliyomtoa Mubarak Misri haiwezi kufananishwa moja kwa moja na mvutano unaoendelea Libya.
Jamani hizi taarifa zimetoka kwa la princessa,msichana ana nifurahisha sana na mawazo yake...leo hii tunasikia Gaddafi kumbe aliandika barua kwa ufaransa Sarkozy, Ban Ki Moon, na Daudi Cameroun wa Uk.. Kweli nimecheka .. Mzee mzima maji shingoni imebidi tu amwambie Mtu Mzima Obama 'Nakupenda' no matter what
UK's prime minister ni David Cameron na si Daudi Cameron
kwa nn hawa marekani na allies wasiwapige somalia wanaouwa watu ovyo, au wampige na kumng'oa gbabo?? wehu wote, kitendo cha marekani na wenzie kumpiga gaddafi ni uhaini ni uhuni na ubabe wa kis""|^^%enge..wanaoona gaddafi anapaswa kuuawa hawana sababu na they are driven by cnn, bbc and the like..they are brainwashed and they can't think for themselves..gaddafi anakataa ukoloni siku zote anasema afrika for afrikans..amefanya makubwa nchini kwake mara alfu hamsini ya mkwere wenu..Afrika lets stand up and unite and fight this colonialism..
AU walikaa kimya ila South Africa,Nigeria and Gabon walitoa picha ya AU otherwise wangekataa au wawe wanafiki kwa kutoka njee kama akina Russia.Vipi kuhusu namba3?
Yule bwana alokua akijifanya chizi kwa kuua watu wake kila kukicha, amepata akili baada ya kuchezea kichapo kutoka France, US na UK. BBC wameonyesha live viongozi wa jeshi wakitoa amri kwa vikosi vyote kusitisha mashambulizi ya aina zote kwa hao waliokua wanawaita 'rebels' wametoa amri kwamba badala ya kushambulia watu wahakikishe watu wote wako salama, hakuna ruhusa kushambulia mtu yeyote...Hongera Obama and the co, kumbe huyu bwana akili anayo ule uchizi ulikua wa kujifanyisha
hata mimi nakumbuka vizuri Gadaff alianza kwa kulaumu al-Qaeda ili apate support ya mkuu wa dunia(obama)
mataifa ya kiarabu yaliomba UN ipitishe hilo azimio hapo unasema je ?Yote tisa,kumi ukweli ni kwamba,mataifa ya ulaya pamoja na marekani yako kimaslahi zaidi! Sidhani kama kweli wana uchungu na raia wanaokufa bila hatia. Kama ni kweli wana uchungu, basi nadhani wangetuma ngege za kivita plus askari wa nchi kavu sehemu nyingi tu za dunia zenye machafuko na hasa kipindi kile cha mauaji ya halaiki ya Rwanda na Burundi.
Pamoja na hayo, nchi nyingi za kiarabu zimekua zikiangaliwa kwa karibu sana na nchi za magharibi! Hii ni kutokana na neema ya mafuta waliopewa. Mbaya zaidi raia wengi wa nchi hizi ni wenye imani ya kiislamu,ambayo haikubaliki na mataifa haya ya magharibi na imekua ikibigwa vita kwa visingizio vya kila aina(ugaidi,siasa kali n.k)
Takwimu zinaonyesha Gadafi ni moja kati ya viongozi wachache shupavu duniani na amefanikiwa sana kuingoza Libya na hatimae kuwa na uchumi Imara. Nguvu ya umma iliyomtoa Mubarak Misri haiwezi kufananishwa moja kwa moja na mvutano unaoendelea Libya.