Huyu jamaa kama kweli ni mbaya kiasi hicho (Dikteta) basi huenda Africa hatuna kiongozi na hata hawa viongozi wetu ambao sio madikteta wanatutesa kuliko ambavyo watu wa Libya wanateswa...
Ni mengi Gaddafi ambayo kaifanyia Libya ambayo sidhani kama kuna kiongozi wa Africa anaweza kusema amefanya hata nusu ya hayo :-
Elimu ya Bure
Tofauti na nchi nyingine za ki-islamu Libya elimu libya ni kwa wote na ni ya bure pote nchini na nchi za nje kuanzia chekechea mpaka masters
Afya
Matibabu bora na ya bure kwa wananchi pia 97% wanapata huduma ya maji masafi (sijui bongo ni asilimia ngapi)
The Great Man Made River Project
Kutungeneza huu mto imechuka takriban miaka 20 kwa gharama ya 20 billion us dollars ( na pesa zote zilitokea ndani ya nchi bila mikopo) hii inasaidia wakulima kuweza kumwagilizia mazao yao.
Pia inasemekana ni msimamo wake ndio ulipelekea nchi za magharibi zinunue mafuta kwa bei ambayo ni nzuri pia ametumia maliasili za nchi yake kwa manufaa ya wananchi wake.
Naombeni majibu wanajamvi kama huyu kiongozi hafai basi ni kiongozi gani wa Africa anayefaa….!!???
Na je kuwa na huyu Dikteta aliefanya kazi na kuleta maendeleo au kuwa na kiongozi anayekaa tu na kumaliza miaka yake kumi kwa kutofanya lolote kipi ni bora..
Colonel Muammar Gaddafi is he really that Bad !!!!!
Gaddafi si mbaya na anastahili credit japo kwa kutumia a minute percentage of national resources to calm the public for years. Gaddafi angekuwa ni perfect leader leo hii Libya na Qatar zingekuwa head to head in terms of infrastructure developments. Ukiongea na Mlibya tena aliyenufaika na hicho kidogo cha kuwadanganyia mpaka katika PhD level ndiyo utajua kuwa Gaddafi alikuwa ni sawa na baba mlevi, anatoa ofa za bia na nyama choma kwa wapambe mpaka wanacheua akiwa bar wakati nyumbani watoto wanakula ugali na kisamvu chukuchuku(Yaani kimechemshwa na kutiwa chumvi tu, no nyanya, no kitunguu, no mafuta etc).
Gaddafi amekuwa akiiendesha Libya kama vile family property. Kilichomfanya Gaddafi kuonekana mbaya ni pale alipoamua kuzima maandamano kwa kuua raia wasio na hatia, huku akijua fika kuwa ana maadui wengi nje ya Libya aliowatengeneza ndani ya miaka 42 ya uongozi wake. Angekuwa anashaurika, angeliandaa Taifa kuelekea kwenye utawala wa kidemokrasia baada ya dalili kuonekana. Lakini kama ilivyo kwa madikteta na watawala wengi waliojilimbizia mali kwa ufisadi (Hapa Tanzania pia imo), watawala kila siku huwa na hofu ya kufikishwa nguvuni baada ya kuachia madaraka kwa njia ya demokrasia kwa mtu asiyeweza kuwalinda, kama ambavyo tunavyoona viongozi wa Tanzania wanavyolindana.
Kwa ujumla ni kwamba Gaddafi amefanya aliyofanya kwa nchi yake kwa kuwa Libya ni Tajiri wa mafuta na alichoifanyia Libya ni kama kumtupia kolokoloni makombo ili ajisahau. Kwa hiyo usishabikiye sana na programme ambazo anafanya kwa kutumia small portion of National income. Kama walibya wote wangekuwa wanaishi kama walivyokuwa wanaishi watoto wake na jamaa zake wa karibu, basi leo hii Gaddafi angekuwa analindwa na wananchi siyo kutafutwa akamatwe.
BTW: Gaddafi aliisaidia Uganda (Under Idi Amini Dada) kwenye vita dhidi yetu ambapo maelfu ya vijana wetu walipoteza maisha, wewe mtanzania unayemtetea leo unatakiwa kujua kuwa ana damu ya ndugu zako mikononi.
