TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 25,225
- 25,488
Sawa Mkuu, nadhani kuna "wanamapinduzi" flani humu jamvini wanafikiri sina uchungu na bara la Africa eti kwa sababu simsapoti Gaddafi na utawala wake uliopitwa na wakati. Nilishasema huko mwanzoni, nimemfuatilia kamanda tangu alipochukua madaraka 1969 (sababu nilikuwa sekondari wakati huo, Mwenge Singida). Vile vile hata baada ya vita vya Iddi Amin bado jamaa nilikuwa namkubali lakini hili kasheshe lilipomfikia na yeye akaamua kuwa mbishi na kuanza kuwauwa raia wake basi nilijua sasa amechemsha. Kwa hiyo simwonei huruma kusema za kweli, ingawa vita hivi vimeiharibu Libya kwa muda mrefu ufuatao. Bado namlaumu Gaddafi kwa ubishi wake usio na mpango!
Nina wasiwasi na namna ulivyokuwa unamfuatilia Comred Gaddaf na kuelewa alichokuwa anakifanya kwa ajiri ya Walibya. Kwa kuzingatia hali ya siasa za ulimwengu zilivyokuwa wakati huo tangu ulipoanza kumfuatilia Col. Gaddaf (kama ulivyosema/andika) na siasa za ulimwengu wa wakati huu. Kama kweli wewe(Askari Kanzu) ni raia wa ulimwengu huu unayeitakia mema Afrika na watu wake, basi ulitakiwa kuwa mmoja wa wale ambao wanamuunga mkono(mimi nikiwa mmoja wao) Rais Col. M. Gaddaf wa serikali ya Libya inayoyumbishwa na "Wahuni wa bengharz" kwa tamaa ya uporaji wa rasilimali za walibya iliyowashika nchi za magharibi.