Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,036
- 9,331
kwahiyo unamaanisha haujali kuuwawa kwa watanzania wakati wa vita vya uganda?
Ina maana unafurahia gadaffi alishiriki kuuwa watanzania, kwahiyo hauna uzalendo? Au uzalendo wako uko libya? Ina maana ni bora kuuliwa sisi kuliko kuuwawa hao walibya?
Behold our beloved nation; if nationality is consent, the state is compulsion.
mkuu inabidi usapoti upande kulingana na convenience na kile unachokisimamia, mathalani mmarekani alisaidiwa na ufaransa kumn'goa mwingereza ili kupata uhuru, lakini mmarekani huyo huyo hakusita kumsaidia mwingereza adui yake wa zamani pindi mwingereza alipokuwa amezidiwa na majeshi ya ujerumani kwenye vita ya pili ya dunia.
Mwingereza, ufaransa na israel walivamia misri mwaka 1956 ili kuuteka mfereji wa suez uliokuwa umetaifishwa na gamal abdel nasser, mmarekani na soviet wakaungana kwa mara ya kwanza kukemea kitendo hicho cha mwingereza japo mmarekani na soviet walikuwa mahasimu wakubwa.
Leo hii mwingereza, mmarekani na mwingereza wameungana katika vita isiyo ya haki kabisa kumpiga member mwenzetu wa au, kwa kutumia kisingizio cha uwongo kabisa, lakini wewe unakumbushia bifu za mwaka 1979, fungua macho uone, ishu siyo ghadafi, ishu ni recolonization ya afrika kwa kuitandika nchi iliyokuwa kimbelembele kuunganisha nguvu za waafrika kujitegemea, wewe unafikir "africa monetary fund" nani alikuwa atoe share kubwa kuliko wengine?, wewe unafikiri eti kwa kuwa wamemuondoa ghadafi na biashara imeishia hapo?, vipi kuhusu makampuni yao ya mafuta kusign mikataba kama ya mangungo wa msovero kwa kupitia viongozi vibaraka watakaowapandikiza?.