The Saga Of Subcontracted Hit Men For Hire Who Outsourced Murder: Mtandano wa wauaji wa kukodisha waliouziana tenda ya kutisha kiasi cha Dolla 282,600

The Saga Of Subcontracted Hit Men For Hire Who Outsourced Murder: Mtandano wa wauaji wa kukodisha waliouziana tenda ya kutisha kiasi cha Dolla 282,600

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
The Saga Of Subcontracted Hit Men For Hire Who Outsourced Murder: Mtandano wa wauaji wa kukodisha waliouziana tenda ya mauaji kiasi cha Dollar 282,600.

Ndugu zangu watanzania, hii story ni fupi sana ukilinganisha na story zingine nilizowahi kuziweka humu JF, lakini inatoa funzo moja kubwa na muhimu katika maisha kuhusiana na suala zima la kuamini watu kupita kiasi katika masuala ya biashara na fedha kwa ujumla. Tafadhali isome kwa umakini.

asasdedews.jpg


Hapo zamani mahakama moja nchini China iliwahukumu watu sita juu ya uhusika wao katika jaribio lililogonga mwamba la "kuuziana kazi" na kupeana mkataba wa kuua kupitia mlolongo mrefu wa madalali. Wanaume hao walishtakiwa kwa jaribio la mauaji ya kukusudia na walipokea kifungo cha hadi miaka mitano jela katika mji wa Guangxi mnamo mwezi Oktoba, tarehe 17, kulingana na uamuzi uliotolewa na mahakama.

Kesi hiyo iliyojawa na sintofahamu nyingi, ambayo watu wengine nchini China waliiona kama mfano wa kujifunza katika maisha ya kisasa na kutoa funzo juu ya hatari iliyopo kwa wale wanaojihusisha na vitendo vya kifisadi na rushwa, ilianza wakati mmiliki wa biashara za majumba ya bei mbaya Tan Youhui alipowasiliana na mtu anayedaiwa kuwa ni muuaji mnamo mwezi Oktoba mwaka 2013, na kumuomba kumuua mshindani wake wa biashara, aliyejukana kwa jina la Wei .

Mtu alikodishwa, Xi Guangan, alipokea kiasi cha fedha ya China Yuan milioni mbili (sawa na $ 282,600) kumuua Wei, ambaye alikuwa amewasilisha kesi dhidi ya kampuni ya Tan juu ya mzozo uliokuwa unaotokana na mradi wa maendeleo.

asasdedewssdsd.jpg


Xi alichukua pesa na kisha kutoa dili hilo la kazi kwa mtu mwingine ambaye angekuja kutekeleza mauaji yale, aliyejulikana kama Mo Tianxiang, huku akibakiza nusu ya kiwango cha awali.

Mo, ambaye alipewa Yuan milioni moja ya Kichina (sawa na $ 141,300), pia aliamua kutokutekeleza mauaji yale. Badala yake, alitia mfukoni pesa kadhaa zilizopendekezwa na kutafuta "hitman" mwingine, aliyeitwa Yang Kangsheng. Yang alilipwa Yuan 270,000 za Kichina (sawa na $ 38,100) kama malipo ya awali na kuahidiwa kiasi kingine cha Yuan 500,000 za Kichina (sawa na $ 70,600) punde tu kazi hiyo itakapokamilika.

Yang kisha akazitia kibindoni sehemu ya pesa na kutoa kazi hiyo kwa mtu wa nne, Yang Guangsheng, na ofa ya kwanza ya Yuan ya Kichina 200,000 ($ 28,200), na bonasi zaidi ya yuan 500,000 za Kichina ($ 70,600) baada ya kukamilisha shughuli. Hati ya mahakama haikufafanua zaidi ikiwa hao akina Yang wawili walikuwa na uhusiano wowote wa kindugu.

asasdedewsaswed.jpg


Mlolongo wa kupeana dili lile la kazi uliendelea kwa zaidi ya miezi sita hadi kazi ilipofikia mtu wa tano, Ling Xiansi. Mpaka kufikia hapo, Ling alipewa pesa kiasi cha Yuan 100,000 tu ($ 14,100) ili kumuua Wei. Ling pia alipatwa na kiwewe juu ya namna gani nzuri ya kumuua Wei.

Lakini badala ya kumuua Wei au kutafuta mtu mwingine anayedhaniwa kuwa ni muuaji bora, aliamua kukutana na mtu aliyelengwa kuuawa moja kwa moja - na akajitolea kumsaidia kufoji/kughushi kifo chake. Wei alikubali kumruhusu Ling apige picha zake akiwa amefungwa kamba kama jaribio la kutaka kufanya mauaji.

Ling baadaye aliripoti juu ya "kufanikiwa" kwake juu katika kufanya mauaji kwa kufuata mlolongo ule ule (Chain of Outsouring), hadi habari zikafika kwa Tan - mtu aliyetoa tenda hii ya kikatili.

images (31).jpg


Wakati huo huo Wei pia aliripoti kesi hiyo kwa polisi, ambao walimshtaki Tan na wahusika wengine watano kwa jaribio la kupanga mauaji ya kukusudia. Tan alipewa kifungo cha miaka mitano jela kwa kuanzisha njama ya mauaji, wakati wale ambao wangekuwa wauaji watarajiwa walipokea adhabu ya gerezani kati ya miaka miwili hadi minne, kulingana na hukumu wa majaji na uamuzi juu ya kesi ile.

Kesi ile ilisababisha mijadala mipana mitandaoni huko nchini China. Watu Wengine waliifananisha kesi hiyo na mazoea ya kupeana tenda ambayo ni ya kawaida katika tasnia ya ujenzi wa nchi hiyo, ambayo mara nyingi imekuwa ikikosolewa kwa kusababisha majengo yasiyofaa kujengwa ama kujengwa chini ya kiwango.

images (32).jpg


Kuna muuaji mmoja alisikika akisema "Hata wauaji nchini China wameelewa madhara ya kufanya Subconstruction/Outsourcing katika kazi zao na hii ndio hali ya biashara pale unapojeka mazoea ya kupitiliza na kuamini sana watu".

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Kulikuwa na dada mmoja mrembo sana "Female Assassin" wa idara ya ujasusi ya KGB aliwahi kuficha risasi mbili ndani ya uke wake alipoenda kumuua mfanyabiashara mmoja maarufu sana katika hotelini huko jijini Minsk mji mkuu wa nchi ya Belarus.

Mfanyabiashara huyo alikuwa amepishana kauli na serikali ya USSR mwaka 1979.

Nipo ninaiandaa hiyo story alafu nitaiweka humu HARAKA SANA.
 
Vizuri lete vitu vingine adhimu ili tuzidi kuutambua ulimwengu wa historia.thanks a lot
 
Hitman watu hatari! Wnyewe wanakuambia Maisha yako yako mikononi mwao
South afrika na Brazil watu Hao wako sana
Mexico usiseme..... Wao wanasubiria Sim waingie kazini
Mjomba... Infantry Soldier hebu shusha mambo zaidi

Ova
 
Mlolongo wa kupeana dili lile la kazi uliendelea kwa zaidi ya miezi sita hadi kazi ilipofikia mtu wa tano, Ling Xiansi. Mpaka kufikia hapo, Ling alipewa pesa kiasi cha Yuan 100,000 tu ($ 14,100) ili kumuua Wei. Ling pia alipatwa na kiwewe juu ya namna gani nzuri ya kumuua Wei.

Lakini badala ya kumuua Wei au kutafuta mtu mwingine anayedhaniwa kuwa ni muuaji bora, aliamua kukutana na mtu aliyelengwa kuuawa moja kwa moja - na akajitolea kumsaidia kufoji/kughushi kifo chake.
Huyo Ling Xiansi aliyeghushi kifo cha huyo jamaa labda ni undercover Police au ni Informer wao.
 
duh hao jamaa wanaakili za kibongo,
udalali mwingi au ujanjaujanja kwenye big deal
 
Back
Top Bottom