The SGR War: Wakati Kenya wakisuasua, Uganda wameamua kujenga SGR. Hii ni fursa kwa SGR ya Tanzania. Is it viable? Tuichangamkie?

Paskali kujenga standard gauge ni kazi mmoja na kuendesha hiyo SGR kwa ufanisi na kwa faida ni kazi nyingine.
Kenya walioanza na SGR kutoka Mombasa hadi Nairobi na baade Naivasha.Operating cost kwa mwezi ni 14 million dollars lakini mapato ni 7 million dollars. Labda ndio sababu China imewanyima mkopo wa kufika Maraba mpakani mwa Uganda.
SGR sio muarobaini wa kila tatizo,bali ni uharaka wa kusafirisha mizigo.SGR ni aghali in short term tena ukiongezea SGR ya umeme lakini pakiwepo wingi wa mizingo ya kwenda na kurudi umuhimu wake upo wazi.
Serikali ya Magufuli imefufua na kuhimarisha meter gauge yaani Reli ya kati na Reli ya kaskazini na kuwezesha garimoshi kuongeza speed tokea 35 hadi 70 km kwa saa.Labda mfumo huo wa zamani usipuuzwe ni mbadala ya SGR.
Paskali Jumuiya ya Afrika Mashariki si kushindanisha hizi nchi bali kushirikiana na kuwawezesha wananchi wake wafaidi ummoja wao.
 
Mkuu tindo , tofautisha signing of MoU, Contract, kuweka jiwe la msingi, uzinduzi wa mradi, na makabidhiano. Hizo ni process tuu lakini kiukweli kabisa, aliyelileta bomba la mafuta la Uganda ni Magufuli, hivyo sifa kwake sio propaganda ni sifa za kweli!.
P
 
...mmhh

Hapa supu umeitia nazi. Bagamoyo ikijengwa ni kiama kwa bandari zetu na hilo deni la SGR halitalipika kwa wakati hivyo mchina atatutawala kwa muda mrefu sana.
 
Mkuu sblandes , asante sana kwa elimu hii, na kiukweli watu kama nyinyi wenye elimu au ujuzi kuhusu jambo fulani, ni big asset kwa jf kwa kuwaelimisha wengine. Kabla sijausoma, I had an opinion kuwa tunashindana, kumbe lengo sio kushindani bali kushirikiana by complimenting one another. Thanks.
P
 
...mmhh

Hapa supu umeitia nazi. Bagamoyo ikijengwa ni kiama kwa bandari zetu na hilo deni la SGR halitalipika kwa wakati hivyo mchina atatutawala kwa muda mrefu sana.
Mkuu carter , no!, it's the other way round, mzigo wa bandari pekee hauwezi kuishibisha SGR to the full capacity, ili SGR ishibe, bandari ya Bagamoyo inahitajika sana!.
P
 
Kamanda ipo siku utapata aibu kubwa sana maana unaishi maisha ya kusadikika. Yaaani Mozambique kuna mradi wa gas wa Usd bil 20? Yaani mradi wa kuzalisha Mw 450 utumie Tsh tril 40?

Bila aibu unatolea mfano mradi wa bandari Bagamoyo?

Yaani nchi iwekeze Tsh tril 40 kuzalisha Mw 450?

Mambo ya gas plant yana manufaa kuliko Hep? Nina mashaka na digrii yako
 
Ni jambo jema sana japo ingekuwa vyema zaidi mikataba ya ujenzi huo ikawekwa wazi na lingekuwa jambo zuri zaidi kama nchi ingekuwa na sera
Nchi hii huendeshwa na mtawala atakavyo yeye sio sera ya nchi hivyo kama Mwandishi msomi ni vyema uandike kitu ambacho baadae hutojutia kuandika ulichoandika .
Waandishi mnapaswa kuisaidia hii nchi kwa kuapishwa makala zenye kuisaidia nchi sio ushabiki na kutafuta maslahi yako binafsi tujitahidi kuchambua bila woga tutaongeza chachu ya mabadiliko.
Kingine hili neno mabeberu wananchi liacheni msiwasikilize sana wanasiasa wanaopenda hilo neno wengi wanatengeneza maslahi binafsi tu
 

Nasema hivi, hilo la bomba la mafuta ni nje ya mada, Kama muafaka wa kuchimba hayo mafuta ulikuwa bado, ule uzinduzi pale chongoleni Tanga ulikuwa wa nini? Kulikuwa na haja gani ya kutumia fedha za umma kujaza viongozi na wananchi pale kuweka jiwe la msingi, kwa mradi ambao ulikuwa bado miaka mitatu sasa? Na iweje wananchi wakaongopewa kuwa 2020 mradi utakuwa umekamilika wakati si kweli? Sioni kama una majibu ya hili, ndio maana nakuambia acha kuchafua uzi wakati huna hoja, zaidi ya kupiga Siasa mfu.

Nafahamu sana umuhimu wa miundombinu ya usafirishaji, achia mbali tu hiyo ya reli na sina tatizo la ujenzi wa miundombinu yoyote. Nilichomwambia anazungumzia hiyo SGR kufika Mwanza achia mbali hiyo Uganda, kwani hata kipande cha Dar-Moro kimekamilika? Kwangu nilitaka aongelee uhakika hata wa kufika hapo Dodoma kwanza, hizo njozi za linkages na Uganda ni kama kuandaa kachumbari ya pilipili, wakati ukijianda kwenda porini kuwinda, huku huna uhakika wa kupata mnyama.

Huhitaji akili ya chuo kikuu kujua hakuna uwezekano wa SGR kufika Mwanza ndani ya hii miaka 5 kwa fedha za ndani, labda Mchina atukopeshe, tena kwa masharti magumu kuliko aliyokuwa amekubaliana na JK hapo awali. Na akiingia rais mwingine iwapo huyu atakubali kishingo upande kutoka, usishangae naye akiachana na mradi wa hii SGR na kuanza mradi wa reli ya kwenda kusini, iwapo ujenzi wa hii SGR hatapata commission. Mfano wa tabia za viongozi wetu kila mtu kuanza ni vipaombele vya utashi wake iko wazi, kama Magufuli alivyotupilia Mbali umeme wa gas wa kuzalisha 5,000mw, na kuanza na mpya wa 2,115mw. Na pia alivyotupilia mbali makubaliano ya mwanzo ya ujenzi wa SGR toka mkopo na mkandarasi wa kichina, na kuanza na makubaliano mapya ambayo mkandarasi ni Mturuki ambapo tumekwama, na sasa tunarudi kwa mchina huyo huyo, ambapo gharama itazidi maradufu ya ile ya awali, na hiyo ni iwapo mchina atakubali kutoa pesa.
 
Itawachukua miaka 50 Uganda kujenga SGR!
 
Kongole Mkuu kwa hii post, miradi ya nchi haiwezi kuwekwa wazi maana mingi ina wizi ndani yake. Nilishangaa sana juzi rais anasema fomu za maadili ziwe siri ili watu wasijue kilichoandikwa! Sasa kama wananchi hawajui mali za viongozi wao watajuaje ukweli wa alichokiandika? Ukishaona serikali yoyote inataka usiri wa kila jambo, inabidi uwe na upeo mdogo kukubali kuwa inaoongozwa na watu waadilifu.
 
Mkuu carter , no!, it's the other way round, mzigo wa bandari pekee hauwezi kuishibisha SGR to the full capacity, ili SGR ishibe, bandari ya Bagamoyo inahitajika sana!.
P
Mkuu Pascal Mayalla nakuelewa sana. Ila ikishajengwa Bagamoyo port operations zake zote zitakuwa chini ya mchina. Na hiyo atafanya hivyo maana atakuwa ana dictate terms as ndie alietoa mkopo wa reli. Na kwakuwa hiyo port ya Bagamoyo itakuwa kubwa ukanda huu obvious ndio itatumia hiyo SGR zaidi kwa kubeba mizigo kutoa na kuingia. Automatically pia mchina atakuwa na upper hand in controlling the SGR too.

Hiyo tayari inampa mchina nguvu ya kuweza kuamua lolote kiuendashaji kwenye miundo mbinu hiyo miwili. Hata swala la ajira, uendeshaji na mapato atasimamia mchina. Kama ilivyo kwa jirani zetu Kenya hapo. Wachina wanaweza "kudanganya" hawapati faida na waka extend muda wa kulipishwa deni. Au wakachukua baadhi ya rasilimali nyingine kama collateral kwa mikopo yao hiyo. Nadhani umeshapitia maswala ya Mandarin weaponized loan, au china debt trap. Hao jamaa sio watu kabisa. Utakita kwa kujenga Bagamoyo na SGR tumewafaidisha wao mara 100. Hadi siku watuachie mradi unakuta umeshakwisha ni kuanza ku renovate upya.

Terms za mikopo mipya ya kumalizia hiyo SGR ziangaliwe vizuri. Ila kama ni kuifufua Bagamoyo hapo ni kupoteza uelekeo. Hizi bandari zetu zenyewe hatujazitumia to the maximum, why tuongeze bandari nyingine kubwa kwa sasa? Dar port kwa upanuzi ulipo sasa ni bandari kubwa na ya kisasa kwa ukanda huu. Inatutosha sana.
 
Hilo la bomba la mafuta ni nje ya mada,ila nilitaka nikuweke sawa,kuweka jiwe la msingi ndio mwazo wa safari ya ujenzi wa bomba.

Kuhusu China kufinance ujenzi wa Sgr ni mpango ambao ulianza toka mwaka 2019. Kwa hiyo usihofu na sidhani utakuwa ni mkataba wa kugharamia kwa mashariti mabaya kama walivyotaka kujenga bandari ya bagamoyo.

JPM kuachama na na umeme wa gas lilikuwa ni jambo jema,hata mtoto mdogo hawezi kuhoji hili. Maana hakuna gad plant inayoweza kuzalisha Mw 2115 kwq mkupuo. Kumbuka Kinyerezi mpaka sasa ni mw 240. Ingechukua muda mrefu kupata mw 2115 amabazo tukijaaliwa tutazipata JNHP.

Kwa hiyo achana na hisia mbaya kuwa Sgr to mwanza inaweza isifike,kikubwa pesa ipatikane. Maana moro to Dodoma ni tambalale hapo ni kujaza tuta na kutandaza reli. Dodoma to Isaka kazi ni mlima Saranda na wenyewe sio kama Ngerengere. Nina uhakika China watatoa pesa bila mashariti ya kinyonyaji.
 

Unahitaji kuwa mwendawazimu kuongea ulichoongea. Unaweka jiwe la msingi zaidi ya miaka mitatu inapita, huku ukiwa umetumia fedha za umma kuandaa hiyo hafla, kibaya zaidi wakati wa hiyo hafla rais wetu akasema mradi utakamilika 2020, leo bado siku tano mwaka uishe, kisha unaleta maneno ya kitapeli sijui MoU, Contract, jiwe la msingi! Mkuu naona umeamua kujitoa ufahamu kutetea aibu.

Magufuli hajaleta hilo bomba kwa ushawishi, bali gharama ya mradi kutokana na jiografia ya Kenya, na usalama hasa kitisho cha Alshababu kwa hilo bomba ndio kumechangia Museveni na Total, kulazimika kutumia route ya Tanzania. Kama Magufuli ana ushawishi wa kuleta hilo bomba, tusingeona jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa dhaifu kuliko ilivyokuwa kabla hajawa rais. Sifa za kuwa Magufuli ndio kaleta hilo bomba, wanaweza kuamini watu wasio na ufahamu wowote kwanini hilo bomba halikupita Kenya, ama watu kama nyie mnaopotosha kwa makusudi, ili kutumia udhaifu wa serikali kupenda kusifiwa kwa ajili ya kusaka maslahi binafsi.
 
Hizi concept hazipo duniani zipo Afrika peke yake kuhusu ujenzi was SGR, sio Europe, America and Asia nchi zimejenga reli ya SGR eti kuhudumia mizigo ya nchi jirani ndio ziwe economically viable! Paskali utambue kuwa SGR inatakiwa iwe socio-economically viable kwa nchi yenyewe kwanza kabla ya hizo siasa za kubeba mizigo ya nchi jirani. Ni bahati mbaya uendeshji was uchumi wet sio was kimkakati, laminitis ungekuwa hivyo tulitakiwa kuwa na manufacturing/production clusters ambazo tulitakiwa kuzinganisha na Sgr kabla ya kukimbilia kwa majirani wakati uchumi wetu haujaunganishwa. Na huu ni mwenndelezo wa colonial economic concept!
Paskali, a project of SGR type that is socio-economic inaanza kurudisha mtaji/ uwekezaji wake kuanzia miaka 50 sio huo uongo mnaojazwamchina
 
Mkuu chagu wa malunde , naunga mkono hoja, kitu wanachotushinda wa Kenya kwenye utalii, ni Kenya wanautangaza zaidi utalii kupitia kwao kuliko sisi Tanzania, hivyo hata mlima Kilimanjaro, wanautangaza sana, na wapanda mlima wengi zaidi ni kupitia Kenya, baada ya sisi kununua ndege na kuimarisha viwanja vyetu, Kenya wameamua kujenga uwanja mpya wa ndege chini ya mlima kwa upande wao, hivyo watalii wa kupanda mlima Kilimanjaro, wale wataopitia uwanja mpya wa Kenya, watafika haraka zaidi kuliko wataokapitia KIA!.
P
 
Mkuu Yusuf Kashaju , kwanza nakubaliana na wewe, sisi Tanzania tuna tatizo la kupanga mipanga mkakati bila wenyewe kujipanga kimkakati, tulikimbilia kununua mi dege, bila kuwa na business plan, as a results, midege imepaki tuu, huku hata timu zetu, zikikodi ndege za jirani kwa safari za kimataifa!. Ili SGR izalize kwa faida, ni lazima ipate mzigo wa kushiba, hivyo tulipaswa saa hizi tunavyojenga, at the same time tunajenga uwezo wa kuzalisha mzigo wa kusafirishwa na SGR. Kuchangamkia fursa: WaTZ tuna matatizo!. Pongezi Rais Magufuli kuwa M/Kiti SADC, usiposaidia WaTZ kuchangamkia fursa, tutaishia kuwa watazamaji tu!.
P
 
Unaweza kuwa sahihi lakini sio kwa kwa kiwango kikubwa, watalii kupanda mlima kilimanjaro ni process ndefu sana, maana lazima wakala wa utalii awaandalie wabeba mizigo,wapishi na mahema. Na safari hii huwa inachukuwa muda zaidi ya wiki kufika kileleni. Ndio maana nasema ni ngumu kwa Kenya kudanganya ili inufaike na mlima Kilimamjaro. Kampuni nyingi za uwakala zimeweka mambo hadharani kwenye mitandao. Hata booking na malipo ni online maana dunia imebadilika.

Pia watanzania lazima tubadilike maana utalii ni ishu ya kijumuia zaidi. Ndio maana kuna mtalii anaanzia Capetown,anapita Zanzibar anaende Masai mara Kenya kisha anamalizia serengeti.

Kama udangangifu labda ilikuwa zamani. Lakini leo hii hakuna mtu atakuja Kilimanjaro kisa eti amedanganywa upo Kenya. Jambo la msingi ni kuutangaza utalii ili tunufaike zaidi.
 

Mkuu pascal Hongera kwa bandiko ka kufikirisha
Nina swali moja tuu ambalo linaweza kuzaa maswali mengine
Hivi unafikiri kati ya Mradi wa SGR na Stieglier gorge ni upi unaweza kuingiza pesa faida kwa Haraka?
Megawatt 2115 na 2700kmSGR
Then hela itakayopatikana hapa ilipe mradi Mwingine
Assume kama tungeanza na Mradi mmoja!
pascal
 
Hili la bomba la mafuta naomba ukae kimya, kwanza ni nje ya uzi na huna jipya.

Hilo la China kufinance mradi wa SGR ulianza 2019. Hiyo 2019 ndio serikali iligundua ile porojo ya kuwa tunajenga kwa fedha za ndani hailipi? Kama tuliwakwepa wachina mwanzo kuwa huo mradi ulikuwa overestimated kwa $7b+, je sasa hivi bei ndio itakuwa chini kwa sehemu ambayo watatoa pesa? Kwa hili ww au mimi hatujui, na sababu hasa ya kuficha itakuwa na aibu ya gharama kuwa juu.

JPM kaachana na umeme wa gas kwa mtazamo wako hata mtoto mdogo hawezi kuhoji, labda ww na mtoto wako ndio hamuwezi kuhoji. Miaka mitano iliyopita kabla ya Magufuli kuwa rais, yeye alikuwa waziri kwenye serikali iliyokuwa inatuimbisha kuhusu umuhimu wa umeme wa gas. Kwanini wakati huo hakuonyesha kuwa umeme wa gas siku sahihi ni ghali kuliko huu wa maji? Iwapo kila rais akiingia anakuja na ukweli anaoujua yeye, na wote tunatakiwa tumuamini wala tusihoji maamuzi hayo, siku akiingia rais mwingine akasema umeme wa upepo ndio sahihi maana wa maji kuna tatizo la mabadiliko ya tabia nchi utaweza kuhoji? hiyo 240mg mpaka sasa kumbuka tulikopa $1.2b, hiyo ikiwemo na ujenzi wa bomba toka Mtwara. Je tungeweka 3t maana bomba tayari liko Dar, tusingepata hiyo 2,115mw, na hiyo hiyo 3.5 tukaingiza kwenye kilimo? Lengo letu sio kupata umeme 2,115mw kwa mkupuo, bali ni kupata umeme unaotosheleza mahitaji yetu. Tungeweza kuongeza kila mahitaji yetu kila inapohitajika, na fedha nyingine kuingizwa kwenye mahitaji mengine. Sio sasa hivi watu hawaajiriwi kisa pesa zinajenga mradi wa umeme wa ziada. Na wanaojenga huo mradi wao hawasikii maumivu ya wengine kukosa ajira, maana kwenye misafara yao wana mpaka maVX 70 na helikopta angani, achia Mbali kupata huduma zote kwa gharama ya serikali, na mishahara yao kwa wakati.

Nimesema hakuna uwezekano wa hiyo reli kufika Mwanza kwa fedha za ndani, maana ukweli wa mapato yetu kwa sasa uko chini. Moja na la dhahiri ambalo ni nje ya uwezo wetu, ni janga la corona. Na la pili ambalo bila corona lazima tungekwama, ni mwenendo wa awamu hii kwenye sekta binafsi, ambayo ndiyo inayotoa kodi kwa wingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…