Mkuu
Mackanackyyy , uko kwenye industry ipi hiyo inayokwambia mombasa port inailisha Dar port? Uko serious katika hilo kweli? Halafu unaposema Tz imelala kwenye kuchangamkia shehena kubwa ni shehena zipi hizo tumeshindwa kuzichangamkia?
Unaweza kufananisha SGR ya kenya na hii yetu inayojengwa? Mbona ni vitu viwili tofauti kimuundo na uendeshaji? Halafu unadhani ni rahisi tu kwa Uganda nae kuchukua standards ya reli ya kenya na kuacha ya Tz?
Benguela railway inatoka Lobito kuunga na Lubumbashi, hiyo bado haizuii mizigo ya Congo kupita Tz. Kikijengwa kipande cha reli kutoka Tabora to Mpanda Karema port watu watafika Kalemie na Eastern Congo kwa haraka zaidi. Hivyo unaona kabisa kenya ndio iko kwenye losing side, kwanza kwa SGR ya kizamani na pili hawako eneo la kimkakati kufikia masoko(nchi) za mbali. Na wao hawana eneo kubwa kijiografia na lenye uzalishaji wa bidhaa zenye uzito mkubwa za kusafirishwa kwa reli.