KUANZA KUUJUA UKWELI
Naomba tuendelee sisi tulikuwa na group la tuliomaliza primary miaka hiyo ya 90's mwishoni, sasa kama mnavyojua mkiwa na group halafu wote mnajuana toka utotoni kunakuwa na utani mwingi sana,na me nilikuwa miongoni mwa wachangia mada maarufu kwenye group, sasa siku hiyo mada ilikuwa NDOA,wakawa tunasemwa watu ambao hatujaoa katika story kuchanganya ukatoka mkeka pale yakawekwa majina ya watu wote ambao hawajaoa na nini utani uakawa mwingi sana na mimi nikiwepo kwenye list.Badae kidogo yule Rafiki yangu nurse akanitext inbox
Nurse: mambo vp
Mimi: nikamwambia poa
Nurse: Huonekani siku hz?
Mimi: Nikamwambia nipo huwa nakuja ofisini kwako lakini tunapishana
Nurse: akasema poa, nimeona jina lako hapo kweye mkeka kwani we bado hujaoa?
Mimi: Nikamwambia ndio ni kweli bado sijaoa
Nurse: Yule unayekuje nae ni nani kwako sasa?
Mimi: Nikamwambia yule ni mchumba wangu bado hatujaoana tutaanza mchakato soon tukitulia.
Akanijibu tu okay, ikaisha hivyo
Kumbe yale maswali alikuwa anuliza vile kwa sababu kuna kitu alikinotice kitambo na aliambiwa na nurse mwenzake ambaye mara Nyingi alikuwa anamuattend yule mchumba wangu pale clinic na siku za mwanzo alinitambulisha kwake na walituona nilivyokuwa naenda pale hospital na mchumba wangu.
Baada ya kumjibu vile aliondoka kutafakari mwenyewe nakuomba ushauri huko (hii alikuja kuniambia badae sana kwamba anikaushie mshakaji wake au anisanue ukweli), kwasabau alikuwa anajua sisi ni wanandoa Tayari na yeye kumbe yule Rafiki yake nurse mwingine akamwambia mbona huyu mkwe wa Rafiki anakuja na card mbili alikuwa anawatoa kidogo wanajaza detail kwenye card zote mbili.na hizo card 2 za clinic zina majina mawili ya baba tofauti moja langu lingine la huyo baba mwingine sasa yeye aliogopa hapo mwanzo kusema alihisi mayb tumeshaoana akaja kuvunja ndoa ya watu akaona akaushe sasa nilivyomwambia hatujaoana ni kama nikampa mawazo mengine ya kuomba ushauri nakutafakari aniambie au aendelee kukausha kingine akawa hana uhakika kama kati yetu pale nani ndio mwenye mtoto.
Ukapita kama mwezi na siku kadhaa hv nikaja kuonana nae tukasalimiana nae fresh badae jioni akanitumia text akaniambia naomba utafute time tuongee na nakumbuka aliniandia baadhi ya maneno nayakumbuka hadi leo "naomba uje ukiwa peke yako ukiwa na utulivu na akili za kiutu uzima"
Me sikutilia umakini sana hayo maneno coz me ni mtu wa utani sana kwenye class letu so nikahisi tu nipunguze utani na nini basi,siku ikafika ilikuwa wekend j2 nakumbuka nikaonana nae baada ya story 2 3 anakaniuliza una kifua nikamwambia ndio, akaniambia bwana kuna kitu amekiona kwa mchumba wangu aliambiwa na staff mwenzake pale ofisini kwao na kuna siku aliitwa kwenda kuangalia mchumba wangu alivyoenda pale clicni ckuwa mchumba wangu inaonyesha ana card 2 za clinic zenye majina mawili tofauti hivyo akaniomba nifanye utafiti wangu kama ni kweli.
Sasa alivyoniambia hivyo me sikumwelewa mana nilikuwa sina kabisa huo utaalamu na by then nilikuwa sijazisikia sana hizo story, akanielewesha kuwa card zina majina ya baba wawili tofauti moja ni wewe nyingine ni mtu mwingine naomba uwe mtulivu ukafatilie hili.Me moyoni nilishtuka ila sikutaka kumwonyesha pale, basi nikamshukuru pale tukaagana.Nikarud home nilikuwa na mawazo kweli nikajikaza pale nikazuga tu issue za kazi na nini,nikawa nafikiria jinsi ya kutafuta nafasi ya kuangalia hiyo card yingine ipo wapi na nilishindwa kucheck kwa haraka coz yeye bado alikwa kwenye ile ya kuwah kutoka job kwasababu ya kutoka martenity karibuni so nikawa natafuta upenyo wa kuweza kuitafuta hiyo card nyingine.Sikumwonyesha kama nimenotice chochote ila nikawa nidigest tu mwenyewe kindani ndani inawezekanaje hili basi nikawa natafakari.
Bahati nzuri week ile ile kukawa na nasafari katikati ya week ilikuwa siyo siku ya kazi aliniomba nimpeleke mahali wanaenda na dada anayetusaidia kazi na bahati nzur yule mkwe wangu alikuwa ameondoka mara moja then atarud so ikawa tunaondoka wote me nikawa na funguo kuwa nawapeleka huko then wakimaliza nitaenda kuwafata.
Basi baada ya kuwafikisha tu chap nikurudi fasta nikaaza kutafuta taratibu kwenye vitu pale nyumbani kwenye documents ambapo najua card huwa inawekwa ikawa hola, nikaona ile card moja yenye jina langu badae nikaenda kwenye kabati la nguo zake nikatoa zote hadi chini sikuiona kitu nikawa naanza kukata tamaa nikasema nirudishe nguo moja moja sasa nikawa nakung'uta naicheck nikaenda nikakuta kwenye vitenge flani vilikuwa vipya havijavaliwa alipewa zawad ya kujifungua alivipanga pamoja katikati nikakuta bahasha na nilivyoifungua ndio nikaiona hiyo card.
Kiukweli nilishtuka sana yani mikono ikawa inatetemeka hivi kuifungua, kweli baada ya kufungua nikaona hiyo kwenye jina la baba lipo lingine nakumbuka kichwa kilikuwa kizito sanaa ile unaskia "nziiiiii",nakumbuka nilijilaza kwenye kitanda naangalia ceiling kama 1hr hv mawzo mengi kichwani kichwa Kizito.
Likanijia wazo hili swala ni zito ngoja nisali kwanza nipate hekima ya kudeal nalo, huwa nakuwa huivyo nikipata kitu kizito sana huwa nasali ili niweze kudeal na jambo lolote linaloniendesha.Baada ya kusali nakumbuka nilirudi kitandani kichwa kinauma nilisinzia kama nusu saa hv then nikashtuka nikarudisha vile vile vitu ila kabla ya kurudisha kitu kikniambia nikipige picha then nikachukua na kile chenye jina langu nikachukua boda nikaenda stationary ya za maeneo ya chuo nikavitoa copy nikaweka kwenye bahasha nikarud navyo home ili kesho yake nikavifiche ofisini.nikarud tena kitandani kutafakari na kuamua nisimuulize chochote kwa sasa nifatilie vitu vingine kwa umakini,badae nikawafata nikawarudisha home.
Sikumwonyesha chochote ila kichwa na moyo wangu uliingiwa na uzito flani wa ajabu sana kuna muda nikiwa nacheza na mtoto namwangalia moyo unauma namwomba Mungu anipe busara na uvumilivu nitajua tu.
Zikapita siku 2 3 nikawa bado natafakari chakula hakipandi,nikapungua ghafla.nikiwa najiuliza nitapataje evidence nyingine kwasababu mchumba wangu alikuwa anaongea sana so nikataka sababu ya uhakika zaidi na mtoto sina access nae ya full time ya kusema umchukue ukapime DNA,kuna wazo likanijia kama card nyingine ipo na ina information inamaana huyo mzazi mwengine pia ana mawasiliano nae nikasema ngoja niangalie simu yake kwasababu nilikuwa sina mazoea ya kushika simu yake kabisaaa.
Nikawa namfatilia ili nipate nafasi ya kuishika simu yake ilikuwa na password ya pattern nilifanikiwa kumfatilia hadi nilijua password yake na ,nikafanikiwa siku moja alikuwa nje nikafanikiwa nikaijua kwenda kwenye message hamna kitu nikasema niende kwenye call history nikaona kuna no.kama kwa siku 4 mfulukizo inapiga asubuh na jioni mida ya saa tisa au 10 jioni.Nikaichukua hiyo no na zingine 2 zilizotokea kwenye call history mara nyingi hv niakenda kutest kuchek jina ikaleta jina moja kama la yule kwemye card.
-Siku moja nikachukua tena nikasema kama kuna issue inawezekana kuna ndugu yake mmoja walichat nae, nikaenda kuserch kuangalia conversation ya ndugu zake nikaja kukuta conversation ya muda mrefu ya yule sister ake waliokuwa wanakaa nae kwenda huko nikakuta conversation za kuna muda anamtaja yule jamaa anamuulizia anaendeleaje ,huyu anajibu hajambo kuna text akawa namuuliza sasa utafanyaje mchumba wangu akawa anajibu yani amechanganyikiwa sijui it seems jamaa alikuwa anasumbua kiaina.Nikazipiga picha zile text nikarudisha simu.
Kipindi hicho kulikuwa na mshakaji mmoja alikuwa nafanyia kazi mtandao wa simu ya ile no nikamwomba anichekia hiyo no ya huyo jamaa huwa inapiga saa ngapi kwenda no ya mchumba wangu na location ya hiyo no mara nyingi inaonekana inapiga ikiwa wapi?jamaa alikuwa mtata kidogo kunipa hizo info coz kuwa wanabanwa sana kutoa taarifa ilibidi nimdanganye kwa kutengeneza story flani ya uongo na nikamwomba anisaidie kindugu me sitaweza kusema nimetoa wapi me nataka nipate info za kuanzia tu,basi nikapata taarifa kuwa jamaa mara nyingi anapiga asubuh na jioni mida ile ile kabla sijarud na pia huwa anamtumia mpunga kidogo na kujua jamaa kumbe yupo dar hapa hapa,kingine yule mshkaji wamtandao akanipa no nyingine inayowasiliana sana na ile no ya jamaa kuchukua ile no kuchek ni jina la kike nikajua huwa itakuwa kazi yake nyingine.
Muda wote huo ilikuwa kama week imepita since nijue ila sikumwambia chochote ila alinotice siku hz nakuwa na mawazo nikawa namdanyanga kuna kazi ofisini zina presurre kubwa sana na chakufanya kwasababu huwa narud usiku nikifika kuoga na kulala halafu usingizi hauji hadi ile kazi ya uber nikastop kufanya nikawa sirud home mapema nasema kuna kazi nyingi ila haikuwa hivyo nilikuw anatoka ofisini nafika mahali napaki gari naanza kufikiri.
nikaingia mission nyingine ya kutaka kufaham sura ya mshkaji, nikaingia facebook nikaanza kuseach jina la yule jamaa nikakosa nikasema nitest jina la ile no nyingine ya mwanamke niliyopewa na yule jamaa yangu ya mtandao nikamwona na picha zake nikaona ni mmama amabye anafamilia na watoto wakubwa tu na pia kunapicha zingine yupo na muwe wake ambaye ni mtu mzima kidogo akiwa amemtag kwa jina la sirname ambayo halipo facebook ila linaendana na kwenye ile card basi name then nikaichukua screenshot ya picha yake.
Then siku moja kuna time nilichukua simu ya mchumba wangu nikaisave ile no nikaenda whatsapp kucheck dp ni no ya yule yule jamaa anaoenakana ni mtu mzima mwenye umri kama 46-50 hv basi nikajirisha nikachuka na picha ya kwenye dp, ila kiukweli ilikuwa ni tukio la wiki kama moja na nusu - 2 ila nilikwisha yani nilikongoroka kabisa.
Wekend iliyofata nikamwomba twende mahali tutoke out,me kabla ya kwenda kule nilichukua ile copy ya vyeti nikaweka kwenye bag la laptop nikampitia tukafika pale piga story mbili tatu me nikachomekea mada kwasasa toka tumefahamiana kuna kitu gani ambacho yeye hajaniambia aua amenificha?akaniambia hamna kila kitu nakijua hajanificha kitu,akaniuliza kwann nauliza nikamwambia nataka kufaham akasema hakuna.
Nikamtajia jina la jamaa unamfaham flan
Yeye:flani yupi?
Mimi:Nikamtajia full name yake lote
Yeye: akasita akasema hamjui ila usoni nikawa namuona ameshachange kabisa
Mimi:Nikachukua picha nika mwonyesha, akasema hamjui,no ya yule jamaa nilikuwa nimeisave nikamwonyesha ile no akasema hajui chochote huku uso wa hofu
Yeye:Hajui chochote
Mimi:nikamwomba simu yake akasita badae akanipa nikmwomba atoe password,moja kwa moja nikaenda kwenye call list yake nikamwonesha ile no nikamuuliza ile no imefata nini kwenye simu yake na huwa anapigiwa mara kwa mara?
Yeye:akasema ni mtu ambaye anamfatilia kumuaproach
-Baada ya kumbana sana na evidence akasema yule ni ex wake,nikamwambia kama ni ex mbona mnawasiliana hadi sasa hv?
-akawa hana majibu
-Badae nikatoa zile copy za vyeti nikamuonyesha nikamuuliza hiki ni nini mbona mtoto wetu ana card mbili na moja wapo ina jina la huyo unayesema ni ex wako?
I see yule dada aliishiwa nguvu kidogo azimie akaanza kulia kwa sauti na kuomba msamaha analia kwa sauti nikaona hapa balaa watu wakawa wanashangaa kuna nini palee ikabidi nimwombe anyamze tuondoke pale alikuwa haelewi.
Nilichofanya nilimbeba nikaondoka nae nikamrudisha nyumbani nikampeleka ndani bado analia anaomba msamaha anatamka kila neno unalolijua wewe hapa duniani.
-nikamake sure ameingia ndani ilikuwa usiku kidogo me nikaondoka zangu nikaenda sehem kuna baa nikapaki gari nikalaza kiti nikawa natafakari tu peke yangu.
-akaanza kunipigia simu sikupokea missed call kibao me nikamute simu, badae dada ake huo usiku nae akawa nanipigia me sikupokea simu badae nikaizima.
-Nilikaa pale nje hadi kukakucha nikarud zangu nyumbani nikakuta ameondoka na mtoto ameenda kwa dada yake pale wamemuacha dada wa kazi,nilivyofika nadhan aliwaambia badae kidogo wakaja na dada yake
Itaendelea …….