Kuna jamaa mmoja alisoma Mzumbe Sekondari miaka ya nyuma, alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kusolve Pure Maths...kimsingi hakuna swali la hesabu lililokuwa linakatiza mbele yake iwe kitabu chochote....
Pia miaka ya nyuma pale Makongo Sekondari kulikuwa na mwalimu mmoja akiitwa Mzee Yona Kazibure. Kabla ya kuwa mwalimu pia alipata kuwa Fundi mitambo RTD na kabla ya hapo alipelekwa na Serikali kusoma nchini Uingereza.
Akiwa nchini Uingereza alipata kusoma na mwanaFizikia maarufu ambaye ni mtunzi wa vitabu almaarufu kama NELKON kwa elimu ya A-Level.
Inaaminika Tanzania haijawahi kutoa mtaalamu wa masuala ya Fizikia kama huyu jamaa. Kwa ubabe wa Kambarage alichoma vyeti vya huyu bwana kama alivyopata kuwanyanyasa wasomi wengine kama kina Tuntemeke.
Mifano ipo mingi...naungana nawe kuwa tatizo ni mfumo wa nchi yetu.