The Tourist: Let's go to Bahamas, a way forwad to USA

Mleta uzi umenifurahisha sana hapo kwenye picha.

Jambo lingine hujatuambia transit Visa kupitia US. inakuwa je; kumbuka ni lazima

Kitu cha pili naomba kujazia nyama kuwa kwa wale wote wanataka kujilipua inabidi wafanye utafiti kuhusu kazi zinazopatikana kwa wing I huku. Wasije kwenda kung'angania kazi zinazofanywa na wazawa; itakuwa ngumu kuzipata

God save us
 
Kizazi hiki tulicho ni cha wapumbavu. mababu zetu walikuwa watu WA kimataifa. Makabila yetu yote Tanzania yalitoka mataifa mengine kuja kuanzisha makazi Tanzania. mababu wa kingoni mfano walisafiri nchi kibao toka Afrika Kusini kabla ya kutua Songea Tanzania wakisaka maisha bora.

Wachaga, wanyakyusa, Masai, nk
Lakini kizazi hiki cha wapumbavu hata kutoa passport tu shida na kwenda nje ya nchi kimejaa woga wa kipumbavu

Ina Maana Wale wazee wetu WA kale walikuwa na uthubutu wa kimataifa pamoja na kuwa walikuwa hawajui kusoma wala kuandika!!!

Sasa tuna wasomi akisikia mtu anazamia anasikia kutetemeka hadi kujiharishia

Wazee wetu walikuwa international traveller's sisi kizazi chao cha sass ni local and we are proud to be local!!!!

Nampongeza huyo anayetaka kuzamia ruksa I wish him all the best likitokea LA kutokea ajali kazini lakini walau amethubutu kufurahisha walau mizimu ya babu na bibi zake ambao walikuwa international travellers kutafuta maisha
 

Kwanza hilo swali zuri sana kuhusu hiyo transit visa ya USA maana inabidi uipate na maswali ni kama unaomba visa yao hapo [emoji45]
La pili kama una hela za ziada unaweza ukakaa kwa muda ukiangalia hali ya hapo na kama unaweza kufanya biashara ndogo ndogo
Najua wahamiaji wengi duniani wanaanza na biashara ya chakula
Imagine uanze kupika pilau au mishikaki na chips na mengi tu
Kumbuka tusingeijua pizza au biriyani bila ya wageni na imewatoa haswa
Good luck [emoji6]


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Halafu huku eti kuna watu wanajiita warembo, unamiliki rangi mbili na wigi kwenye mwili wako halafu unajiita mrembo angalieni color hizo original hakuna sugu hapo wala dalili za kukomaa very very soft...
Nchi nyingine yenye watoto wazuri Venezuela na Colombia,ni hatari
 
Uzi mzuri sana huu kwa vijana wenye ndoto ya kuishi na kutafuta maisha nje ya nchi.

Maisha ni popote pale ukiamua inawezekana
Wengi hata vigogo WA vyama Na serikali wengi maendeleo hawajayapatia vijijini kwao walikozaliwa wameyapatia Mbali kwingine ukiona maisha yamebana kwako binafsi Tanzania usiogope kutimka kutafuta maisha nchi zingine. Wengine wasiojielwa utasikia oh how hapa hapa pana maisha!!!! Sio kwa kila mtu. Mfano Marekani kwa watanzania kuna fursa kibao wakati huo huo wamarekani wanawaza kuja Tanzania kwa kuona kuna fursa. mnapishana angani kwenye ndege mmarekani anakuja kuchukua fursa Tanzania Na mtanzania unaenda kuchukua fursa marekani ndivyo yalivyo maisha ni kitendawili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…