Hao watoto wa yesu walifanya maajabu gani?
MKE WA YESU
Biblia inasema kwamba Bwana Yesu Kristo alikuwa akipatikana na mwanamke mmoja aitwaye Mariam Magdalena.
Yeye alikuwa karibu sana na Yesu. Vitendo vyao vinaonesha kwamba, walikuwa mume na mke au marafiki wapenzi.
Sisi hatuamini kwamba nabii anafanya urafiki na mwanamke na kumpangusa miguu yake kwa kichwa na kum’busu, bali yeye alikuwa mke wake. Tusome Biblia kisha tuone kwamba huyo alikuwa nani?:
1. “Na tazama, mwanamke mmoja wa mji ule, aliyekuwa mwenye dhambi, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Farisayo, alileta chupa ya marhamu. Akasimama nyuma karibu na miguu yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake, akiibusu-busu miguu yake na kupaka yale marhamu. Basi yule Mfarisayo aliyemwalika alipoona vile, alisema moyoni mwake. Mtu huyu kama angekuwa nabii angemtambua mwanamke huyu amgusaye, ni nani, na ni wa namna gani ya kwamba ni mwenye dhambi. (Luka 7:37-38).
2. “Basi mtu mmoja alikuwa hawezi Lazaro wa Bethana, mwenyeji wa mji wa Mariamu, dada yake.
Ndiye Mariam yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu kwa nywele zake, ambaye Lazaro nduguye alikuwa hawezi (Yohana 11:1-2).
3. “Basi Mariam akatwaa ratili ya marhamu ya nardosafi yenye thamani nyingi, akimpaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake.’’ (Yohana 12:3).
4. “Akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, wamuona mwanamke huyu? niliingia nyumbani kwako, hukunipa maji kwa miguu yangu, bali huyu amenidondoshea machozi miguu yangu; na kuipangusa kwa nywele zake. Wewe hukunibusu; lakini huyu tangu nilipoingia hakuacha kunibusu sana miguu yangu. Hukunipaka kichwa changu mafuta; bali huyu amenipaka kichwa changu mafuta’’ (Luka 7:44-46).
5. “Basi Mariamu pale alipokuwapo Yesu, na kumuona, alianguka miguuni pake, akamwambia Bwana, kama ungalikuwepo hapa, ndugu yangu hangali kufa. Basi Yesu alipomuona analia na wale Wayahudi aliyofuatana nao wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake akasema mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo utazame. Yesu akalia machozi.’’ (Yohana11:32-35).
6. “Biblia inaeleza habari ya arusi moja, iliyofanyika huko Kana ya Galilaya. Imeandikwa: “Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo, Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai. Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia. Mamaye akawaambia watumishi, lolote atakalowaambia, fanyeni. Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. Yesu akawaambia, jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaza hata juu. Akawambia, sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka. Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), Yule mkuu wa meza alimwita Bwana arusi, akamwambia, kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.” [Yohana 2:1-10].
Katika aya hizi mambo yafuatayo yanathibitisha kwamba arusi ile ilikuwa ya Bwana Yesu Kristo.
(A) Bwana Yesu, mama yake na wanafunzi wake walikuwepo huko. Kualikwa katika arusi ya mtu mwingine haingewezekana. Kwa sababu hawakuwa na uhusiano mzuri na watu wengine, ila waalikwa wote.
Basi arusi ilikuwa ya Yesu mwenyewe.
(B) Wakati divai ya arusi ilipokwisha, Mariamu mama yake Yesu, alishituka na alihangaika sana, na mara moja alikwenda kwa Bwana Yesu kumwambia afanye chochote sasa, maana itakuwa fedheha mbele ya wageni.
Mahangaiko ya Bi Mariamu yanaonesha kwamba yeye hakuwa mgeni bali alikuwa mwenyeji na msimamizi wa arusi ya mwanawe Yesu. Waila wageni hawatishiki kwa kupungua au kwisha chakula.
(C) Wakati Bwana Yesu aliambiwa apange mpango wa kuongeza divai ya arusi, alimwambia mama yake kwamba leo mimi ni bwana arusi, hivyo siwezi kuhangaika. Kwa sababu ya kukaa juu ya kiti cha Bwana arusi, saa yangu haijawadia.
(D) Bi Mariam aliwaita wanafunzi kumsaidia Yesu kupanga mpango wa divai, wote walishughulika
kufanya kazi ile. Hiyo inaonesha kwamba arusi ilikuwa ya Bwana Yesu na wanafunzi wake walikuwa wakimsaidia katika shughuli za arusi. Maana hawakuwahi kufanya kitu kama hiki kabla.
(E) Mkuu wa meza alikuwa mtu mwingine. Kama arusi alikuwa siyo Yesu basi yeye angekuwa mkuu wa meza kulingana na heshima yake. Lakini kama Yesu alikuwa bwana arusi basi mwingine anaweza kuwa mkuu wa meza.
(F) Yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi na kumpongeza kwa kutengeneza divai nzuri. Kwavile bwana Yesu ndiye aliyetengeneza divai basi ni yeye pia aliyekuwa bwana arusi.
Basi arusi ya Kana ya Galilaya ilikuwa ni arusi ya Bwana Yesu.
Je, mtu aliyeendelea kufanya mapenzi na mwanamke au aliyeoa anaweza kuwa mungu?