Thiery Henry ukocha si kama ulivyokuwa unauza sura SKY SPORTS , hii ni kazi ngumu hasa .

Unapataje ujasiri wa kusema haezi fika popote kwa timu mbovu kama ile? Leonardo Jardim mwenyew kwa uwezo wake alonao kashindwa kupata ushindi kwenye mechi sita za ligi zote kapigwa af unategemea Henry afanye nini!
Kuna Mtu anaitwa Louis Van Gaal hata ukimpa African lyon anaweza fika mbali, ameprove mara kibao na vikosi vibovu kufika mbali.

Kina Sam Allardyce timu makocha wote wakishindwa inashuka daraja muite yeye ataikomboa

Leo hii hicho kikosi kibovu anaweza akapewa wenger na ukashangaa timu inafika mbali.

kaanza Garry Neville sasa huyu Henry, liwe somo kwa pundits wanaobwabwaja ovyo na kuponda makocha kila siku.
 
Kuna utofauti wa kuwa kocha bora, mchezaji bora na mchambuzi bora

Sio kila mchezaji mzuri atakuwa kocha mzuri, sio kila mchambuzi basi atakuwa kocha mzuri

Gary Neville Yalimkuta Haya Alipokuwa Valencia

Gary Neville hajawahi kuwa mchezaji mzuri, Wala hajawahi kuwa mchambuzi mzuri. Yaliomkuta Valencia hayakuwa ya ajabu kabisa.
 
Gary Neville hajawahi kuwa mchezaji mzuri, Wala hajawahi kuwa mchambuzi mzuri. Yaliomkuta Valencia hayakuwa ya ajabu kabisa.
Garry Neville hajawahi kuwa mchezaji mzuri? Loh umeanza kuangalia mpira lini? Hizi honors za G Neville.

1. Kikosi bora cha ligi ya uingereza mwaka.
-1996/97
-1997/98
-1998/99
-2004/05
-2006/07

2. Kikosi bora cha karne alikuwepo tuzo ya 2007

3. Jarida la michezo la ulaya kikosi bora mwaka 1997/98 (akimpita mtu kama Cafu.)

4. Fwa tribute award 2012

5. Kikosi bora cha muongo ligi ya uingereza 1992 mpaka 2002

6. Kikosi bora cha miongo miwili kuanzia 1992 mpaka 2012

7. English football hall of fame 2015.

Sasa niambie mkuu tuzo zote hizo alikuwa ni mbaya? Miaka 3 mfululizo unapata tuzo ya beki bora namba mbili huyo ni mchezaji mbaya? Ulimuangalia garry neville anaanza kucheza mpira 1992 ama umekuja kumuona kibabu nevile mwenye miaka 36 akigeuzwa na nasri?

Kama neville ni mbaya unaweza ukanitajia beki namba mbili ligi ya uingereza nzuri kushinda neville kwenye miaka ya 90 hadi mwanzo wa miaka ya 2000?
 
Shida ya Monaco inaweza kua sio kocha aisee
Naunga mkono hoja

Najaribu kuitazama namna ilivyobomolewa na timu zenye pesa mara baada ya kufanya vizuri misimu 2 iliyopita

Angalia Bernard Silver na Mendy wameenda City, Mbape amekwapuliwa na PSG, Fabinho amekwenda Liverpool, Bakayoko alichukuliwa na Chelsea, kuna yule winger black anayetumia mguu wa kushoto sijui alichukuliwa na nani

Kiufupi ile timu ilibomolewa kabisa, kwa hiyo inahitaji kujengwa upya
 
Hajui anachozungumza huyu

Eti hajawahi kuwa pundit mzuri, halafu yupo sky sports

Angekosoa uwezo wake wa ukocha ningemuelewa, japo hakufundisha kwa muda mrefu so kumuhukumu pia ni kumuonea
 
mimi sikujua kama wazungu nao wana ujinga kama sisi pale ubeligiji alikuwa msaidizi wa kocha mwenye ujuzi kwa hiyo mafanikio ya Ubeligiji wakayahamishia kwake kiukweli yule jamaa bado sana asipojiangalia heshima yake itapotea bure muda wote kumkosoa Wenger kumbe yeye ndio bomu zaidi
 

Wewe hujui unachongea kuhusu Neville

Hajui anachozungumza huyu

Eti hajawahi kuwa pundit mzuri, halafu yupo sky sports

Angekosoa uwezo wake wa ukocha ningemuelewa, japo hakufundisha kwa muda mrefu so kumuhukumu pia ni kumuonea

Bora nikuacheni tu, Mana kazi itakua sindogo
 
Hali mbaya mno ! jana kapigwa 4-0 nyumbani na PSG
 
Bergkamp anafanya vizuri pale Ajax akimsaidia Frank De Boer!
 
Hakufanya uungwana mi niliumia kupita Wenger mwenyewe. Na hii dhambi itamtafuna daima hadi aombe radhi.
Mkuu ngozi nyeusi usiiamini kabisa, popote duniani utakapoikuta! Kile alichofanya T14 ni mf halisi wa tabia zetu wazaramo....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…