Things fall apart, the centre cannot hold (The 2nd Coming)

Kiranga

Platinum Member
Joined
Jan 29, 2009
Posts
78,790
Reaction score
128,275
The Second Coming

Turning and turning in the widening gyre
The falcon cannot hear the falconer;
Things fall apart; the centre cannot hold;
Mere anarchy is loosed upon the world,
The blood-dimmed tide is loosed, and everywhere
The ceremony of innocence is drowned;
The best lack all conviction, while the worst
Are full of passionate intensity.

Surely some revelation is at hand;
Surely the Second Coming is at hand.
The Second Coming! Hardly are those words out
When a vast image out of Spiritus Mundi
Troubles my sight: somewhere in sands of the desert
A shape with lion body and the head of a man,
A gaze blank and pitiless as the sun,
Is moving its slow thighs, while all about it
Reel shadows of the indignant desert birds.
The darkness drops again; but now I know
That twenty centuries of stony sleep
Were vexed to nightmare by a rocking cradle,
And what rough beast, its hour come round at last,
Slouches towards Bethlehem to be born?
 
Juzi rafiki yangu mmoja kanitumia ujumbe huu.

Anasema:-

Nimeongea na kada mmoja kindakindaki, ni wale "piga ua, humwambii kitu kuhusu CCM" aka "waliokunywa maji ya bendera". Anasema "hili la mkataba wa bandari has completely changed the Tanzania we used to know." How? I asked. He said "things have fallen apart, the centre cannot hold".

Kaka yangu huyu amenikumbusha hili shairi la W.B Yeats linaitwa "The Second Coming" alipoutaja huo mstari wa "Things fall apart, the center cannot hold".

Watu wengi wakisikia "Things Fall Apart" wanakumbuka kitabu cha muandishi wa ki Nigeria Chinua Achebe, wengi tulikisoma kitabu hiki shule za sekondari kama sehemu ya English literature. Lakini Chinua Achebe naye aliupata huo mstari kwenye shairi hili la W.B Yeats. Mshairi wa ki Irish aliyeliandika January 1919, nafikiri baada ya kuona dunia inabadilika kwa kasi kubwa sana baada ya vita vya kwanza vya dunia, na viongozi wa siasa kutoweza kukabiliana na mabadiliko hayo ya dunia.

Kuanzia hapo, shairi hili, na hususan huu mstari, ni shorthand ya kuwakilisha maafa makubwa na uongozi usioweza kuyakabili maafa hayo.

Ni mstari unaoashiria mabadiliko makubwa sana yanatokea au kutabiriwa, na wale wanaotakiwa kuongoza kuyakabili kushindwa kuyakabili.

Nimekuwa nikinukuu shairi hili, hususan huu mstari, mara nyingi, kwa miaka kadhaa sasa, hususan ninapoona jahazi la nchi yetu linakabiliwa na mawimbi makubwa na kuelekea kwenda mrama, na uongozi unapoonekana kupwaya kwenye usukani, kama sasa.

Kwa mujibu wa kaka huyu na wazee wengi wenye heshima zao ambao nawaondoa kwenye siasa za kawaida za upinzani za kupinga serikali kila siku, ukiondoa heshima zetu za kawaida za Kitanzania za kila siku ( zile za kusema "rais ana nia nzuri, ila washauri wake ndio wanampotosha"), inaonekana watu wengi sana wanaona kuna ombwe la uongozi, nchi ipo katika autopilot, tunakwenda kwa kudra za mwenyezi Mungu tu (ambaye wengine hatuamini yupo) na urahimu wa kawaida wa Watanzania wasiojua au kupenda sana kusisitiza haki zao za uraia.

Maoni yako tafadhali.
 
"the centre cannot hold" ningependa kufahamu ni nini hiyo au ni akina nani kabla sijatoa maoni yangu zaidi?
 
The Second Coming

W.B Yeats 1919

Turning and turning in the widening gyre
The falcon cannot hear the falconer;
Things fall apart; the centre cannot hold;
Mere anarchy is loosed upon the world,
The blood-dimmed tide is loosed, and everywhere
The ceremony of innocence is drowned;
The best lack all conviction, while the worst
Are full of passionate intensity.

Surely some revelation is at hand;
Surely the Second Coming is at hand.
The Second Coming! Hardly are those words out
When a vast image out of Spiritus Mundi
Troubles my sight: somewhere in sands of the desert
A shape with lion body and the head of a man,
A gaze blank and pitiless as the sun,
Is moving its slow thighs, while all about it
Reel shadows of the indignant desert birds.
The darkness drops again; but now I know
That twenty centuries of stony sleep
Were vexed to nightmare by a rocking cradle,
And what rough beast, its hour come round at last,
Slouches towards Bethlehem to be born?
Ina maana Dr Mpango ndio atachukua usukani?
 
They have too little to care.

If they can rigg the entire election then what?

Opposition can be lured by few chunk of elected MPs and keep quite, then the game is on.

We have everything in our disposal, then what..
 
"the centre cannot hold" ningependa kufahamu ni nini hiyo au ni akina nani kabla sijatoa maoni yangu zaidi?
Yani kwa lugha nyepesi ni kama vile una tairi, halafu pale katikati ya tairi panapolibeba tairi zima na gari/ baiskeli, pale katikati pavunjike kutokana na kuzidiwa na mzigo.
 
Si umeona issue ya bandari wasemaji
Ni wakina mwijaku,Steve nyerere nk

Ova
 
Yani kwa lugha nyepesi ni kama vile una tairi, halafu pale katikati ya tairi panapolibeba tairi zima na gari/ baiskeli, pale katikati pavunjike kutokana na kuzidiwa na mzigo.
Naomba kuuliza kwanini hadi leo sijaona au kusikia msimamo au maoni ya VP.

Unafikiri ni bahati mbaya au kuna mikakati,mipango,mbinu,maono ya kuhakikisha katika hili la Bandari hachafuki,hausiki !.
 
They have too little to care.

If they can rigg the entire election then what?

Opposition can be lured by few chunk of elected MPs and keep quite, then the game is on.

We have everything in our disposal, then what..
They don't care about us.
-Michael Jackson
 
Naomba kuuliza kwanini hadi leo sijaona au kusikia msimamo au maoni ya VP.

Unafikiri ni bahati mbaya au kuna mikakati,mipango,mbinu,maono ya kuhakikisha katika hili la Bandari hachafuki,hausiki !.
Kwa sasa hivi, kimantiki, ukiona mtu yupo juu serikalini na hajautetea mkataba huu, ujue hakubaliani nao, ila anashindwa kuupinga kwa sababu serikali inaendeshwa kwa "collective responsibility" tu.

Ama hivyo, ama hata kama anakubaliana nao, na hajalazimishwa kutoa msimamo, inawezekana ikawa anaona bora akae kimya kwa sababu mkataba haukubaliki kwa watu wengi.

Ili, kesho keshokutwa akitaka kuwa rais, aweze kuukana mkataba na kusema kuwa yeye hakuukubali mkataba, ila alilazimika kwenda nao kama sehemu ya serikali iliyoupitisha tu.

Hata rais wa sasa kimsingi anakosoa mambo mengi yaliyofanyika chini ya Magufuli (mfano plea bargaining na scandal ya hela zake) wakati yeye mwenyewe alikuwa sehemu ya serikali iliyopitisha mambo hayo na hatukuwahi kumsikia akilalamikia hayo wala kujiuzulu awali.

Na hata Magufuli wakati akiwa Waziri, kuna siku baba yangu alimkosoa sana Mkapa kuhusu sera zake za ubinafsishaji mashirika ya umma yaliyokuwa yanatengeneza faida, baada ya mzee wangu kumkosoa sana Mkapa, kesho yake Magufuli, akiwa waziri, alimpigia simu na kumpongeza sana.

Magufuli alikuwa akimwambia baba yangu kuwa baba yangu amekuwa shujaa sana kwa kusema kile kitu ambacho wao kina Magufuli wamejaribu sana kukisema katika baraza la mawaziri, lakini wamesema kidogo tu, Mkapa aka wa shut down, wakamuogopa kwa kuwa yeye rais, ila baba yangu alisema kwa kirefu sana, Magufuli akawa anamshukuru baba yangu kwamba amefanya kazi kubwa ya kishujaa ya kupinga ubinafsishaji mashirika ya umma yaliyoleta faisa.

Hivyo hata Magufuli naye alikuwa katika serikali ya Mkapa, alikuwa hataki ubinafsishaji wa Mkapa kwa mujibu wa maneno yake aliyomuambia baba yangu wakati akiwa waziri, lakini hakuweza kukosoa sera za ubinafsishaji hadharani, wala hakujiuzulu uwaziri.
 
Juzi rafiki yangu mmoja kanitumia ujumbe huu.

Anasema:-

Kaka yangu huyu amenikumbusha hili shairi la W.B Yeats linaitwa "The Second Coming" alipoutaja huo mstari wa "Things fall apart, the center cannot hold".

Watu wengi wakisikia "Things Fall Apart" wanakumbuka kitabu cha muandishi wa ki Nigeria Chinua Achebe, wengi tulikisoma kitabu hiki shule za sekondari kama sehemu ya English literature. Lakini Chinua Achebe naye aliupata huo mstari kwenye shairi hili la W.B Yeats. Mshairi wa ki Irish aliyeliandika January 1919, nafikiri baada ya kuona dunia inabadilika kwa kasi kubwa sana baada ya vita vya kwanza vya dunia, na viongozi wa siasa kutoweza kukabiliana na mabadiliko hayo ya dunia.

Kuanzia hapo, shairi hili, na hususan huu mstari, ni shorthand ya kuwakilisha maafa makubwa na uongozi usioweza kuyakabili maafa hayo.

Ni mstari unaoashiria mabadiliko makubwa sana yanatokea au kutabiriwa, na wale wanaotakiwa kuongoza kuyakabili kushindwa kuyakabili.

Nimekuwa nikinukuu shairi hili, hususan huu mstari, mara nyingi, kwa miaka kadhaa sasa, hususan ninapoona jahazi la nchi yetu linakabiliwa na mawimbi makubwa na kuelekea kwenda mrama, na uongozi unapoonekana kupwaya kwenye usukani, kama sasa.

Kwa mujibu wa kaka huyu na wazee wengi wenye heshima zao ambao nawaondoa kwenye siasa za kawaida za upinzani za kupinga serikali kila siku, ukiondoa heshima zetu za kawaida za Kitanzania za kila siku ( zile za kusema "rais ana nia nzuri, ila washauri wake ndio wanampotosha"), inaonekana watu wengi sana wanaona kuna ombwe la uongozi, nchi ipo katika autopilot, tunakwenda kwa kudra za mwenyezi Mungu tu (ambaye wengine hatuamini yupo) na urahimu wa kawaida wa Watanzania wasiojua au kupenda sana kusisitiza haki zao za uraia.

Maoni yako tafadhali.
Umeandika kifalsafa kubwa na kisomi sana....wabongo wengi hawataweza kujadili hii mada, labda wasomi

Labda ungeweka na umbea umbea,utani au uzushi ungeshangaa jinsi ambavyo wangechangia
 
Dah,

Mkuu, unajua mara ya kwanza nilitaka kuweka shairi tu kutoka post ya kwanza, bila ya maelezo hayo ya post ya pili.

Nikaona sitaki kuwa mtata sana, ngoja niweke maelezo ili kufunguka zaidi.

Sasa, nimeweka maelezo kufunguka zaidi kuepuka kuwa mtata, wewe bado unaniambia nitaonekana mtata?
 
Naomba kuuliza kwanini hadi leo sijaona au kusikia msimamo au maoni ya VP.

Unafikiri ni bahati mbaya au kuna mikakati,mipango,mbinu,maono ya kuhakikisha katika hili la Bandari hachafuki,hausiki !.
Kila akitawala muislam nchi ipo autopilot!?..wametoka shimoni hata waliokana Imani zao!
 
Umepata wapi tafsiri hii mkuu?
Kuna umbea... nasisitiza... umbea.... unazunguka mitaani kuwa mama haelewani na mzee wa Msoga kabisa, na kuwa mzee wa Msoga na kundi lake wamepania kumwondoa uchaguzi ujao. Umeshausikia? What do you make of it?
 
So things falls apart whenever the centre cant hold🤗

Nice observation sir
 
Back
Top Bottom