Ina lingana na nani anauliza, kuna costs tofauti zitazotokana na shipping..... kuna export tax na loading fee kutoka kwa port hadi kwa meli ambayo ni nchi husika inaamua, kuna the actual shipping fee ambayo Shipping lines ndo huamua bei ya usafirishaji kwa meli zao, kuna landing cost na import tax ambayo nchi yako ndo inaamua.... Hio garama yote itaskumiwa muagizaji bidhaa na yote itaitwa shipping cost.
Lakini tunachogusia hapa ni hii nauli ya kusafirisha bidhaa kupitia meli..... Kampuni tofauti za meli ziko na bei zake, yule shipping agent ndo ataamua kampuni gani ni cheaper au nzuri kusafirisha mzigo wako, lakini akishaamua hilo, hana nguvu ya kuchagua ni njia gani mzigo huo utafikishwa kule uendako. Agent akishalipa kampuni ya meli, wao wenyewe wanaamua jinsi gani watafikisha mzigo wako salama. Inawezekana hata meli ikakwama njiani na wakaamua kontena yako isafirishwe na helicopter hadi bandarini, hio si shida yako bora mzigo wako ufike salama salmin.
Shipping line wakiamua ni cheaper mzigo wa Tanzania kutoka Saudi Arabia uende hadi Durban port SA ndo urudi hadi TZ, nyinyi kama Watanzania hamna budi ila kukubali manake wamewarahishia uchukuzi na kupunguza garama ya shipping.