Al-Watan
JF-Expert Member
- Apr 16, 2009
- 11,891
- 14,583
Hujaonyesha nilipokosea wapi, zaidi ya kulalamika lalamika bila muelekeo wala mantiki hivyo hata kama nimekosea, wewe umekosea zaidi.Kwa kweli wengi wetu bado tunahitaji elimu ya kutosha, huna elimu unahoji mwenye elimu hata kama feki kama unavyoita wewe.
Uvivu wa kusoma utatufikisha pabaya watanzania, inafika mahali idadi kubwq ya watu wanahoji uhalali wa UDSM kumtunuku Magufuli shahada ilihali hata ufahamu wao kuhusu shahada aliyotunikiwa hawaijui!!
Naomba tujaribu kuchambua mambo kwa kina kabla ya kurukia kutoa maelezo potovu, tena kwa taasisi iliyojojengea sifa ndani na nje ya nchi kwa muda mrefu
Sent using Jamii Forums mobile app
Unajuaje sina elimu?
Elimuni nini?
Unajiridhishaje nina uvivu wa kusoma? Wewe mpaka leo umesoma vingapi vilivyokufanya ujiridhishe kwamba mimi ni mvivu wa kusoma?
Wiki hii umesoma vitabu vingapi?Umejifunza nini? Sasa hivi unasoma nini?
Unataka tulinganishe posts zako na zangu ni za nani zinataja usomi zaidi, zinataja vitabu zaidi, zinataja research zaidi halafu tulinganishe, kwa ushahidi wa habari zetu za JF tu, nani ana uvivu wa kusoma kuliko mwenzake?
Wiki hii tu wewe hapa JF umemjibu mtu gani kwa ku recommend kitabu/ vitabu vingapi?
Unaweza kwenda nami toe to toe tuangalie kati yangu mimi na wewe kwa uashahidi wa posts za JF tu, nani ni mvivu wa kusoma?
Ufahamu wangu kuhusu shahada aliyotunukiwa Magufuli na UDSM una mapungufu gani ambayo wewe umeyaona?
Unaomba tuchambue mambo kwa kina wakati wewe mwenyewe unavyoomba tuchambue mambo kwa kina umesema mambo kwa juu juu tu bila kugusia undani wa justification wa sentensi zako zinazoelea elea hewani tu kama maajabu ya bustani ya mfalme Nebukadneza?
Unaomba tuchambue mambo kwa kina wakati maombi yako hayana hata kina cha dimbwi la maji barabarani?
Practice what you preach.Kama unataka tujadili mambo kwa kina kweli, eleza maoni yako kwa rebuttal ya kina.
Sio unarusha maneno tu "tuchambue kwa kina" wakati post yako inaonyesha wazi hata kina ukikiona huwezi kukijua!
Utakiingia kwa pupa na kuzama kama ulivyoyaingia haya maji marefu kwa pupa na sasa unazama.