Uchaguzi 2020 This is Bishop Gwajima in his true colours

Uchaguzi 2020 This is Bishop Gwajima in his true colours

Halima ni mwanafamilia lakini ubunge umetosha sasa, hakuna analofanya jipya kawe
Sina tatizo na Dada yangu Halima na namkubali mno na hata Yeye pia ananikubali sana ila nadhani kwa sasa imetosha aache Gwajima ashinde pia.
 
Kama hizo sifa alizompa Magufuli ni za kweli ina maana Kawe isingekuwa na hayo matatizo aliyosema yamesababishwa na Mdee, Gwajima hajielewi, atambue wapiga kura wa Kawe sio wale waumini wake waliomzoesha kumshangilia tu hata akiongea ujinga.
 
Binafsi sina shida na mauno ila ukabila na ulaghai wa mtu huyu.
Amekuambia kuwa akiwa Mbunge Wasukuma wote watahamia Kawe? Hivi kuna Mtanzania asiye Mlaghai / Tapeli? Acheni Unafiki na Chuki zenu pia.
 
GWAJIBOY AKIMKARIBISHA JPM: Mheshimiwa Rais karibu sana jimbo la Kawe. Watu wa Kawe wamekusanyika hapa kwa wingi kukupongeza kwa kazi kubwa uliyowafanyia. Kwa miaka mitano ya uongozi wako umetatua kero ya muda mrefu ya maji maeneo mengi ya jimbo letu.

Umepeleka umeme kata nyingi, umejenga vyumba vya madarasa kwenye kata karibu zote, umetanua barabara ya Bagamoyo kutoka Morocco hadi Mwenge ili kupunguza msongamano, umejenga barabara nyingi za mitaa kwa kiwango cha lami na zinapitika muda wote. Mheshimiwa Rais tunakushukuru sana.

GWAJIBOY AKIMZUNGUMZIA MDEE: Mheshimiwa Rais jimbo hili ni kama halina mbunge. Kwa miaka mitano ya viti maalumu na 10 ya ubunge huyu mama hajali shida za wananchi kabisa. Maeneo mengi ya jimbo letu yana shida ya maji. Kata ya Mabwepande, Madale na Goba maji yanatoka mara moja tu kwa wiki na wakati mwingine hadi wiki mbili hayatoki.

Baadhi ya maeneo mtandao wa umeme haujafika kama kule Kisauke na Mbopo. Maeneo ya Mabwepande kuna uhaba wa vyumba vya madarasa watoto wanasongamana darasani na wengine wanakaa chini. Barabara nyingi za mitaa hazijakarabatiwa na hazipitiki. Mbunge yupo tu hakuna anachofanya. Kazi yake ni kuchochea migomo na kutoka bungeni.
Weka video yake hapa, nimecheka jamani 😂😂
 
Nitampima 'Mbunge' wangu mtarajiwa Gwajima baada ya miaka yake Mitano na kuhusu 'Mapungufu' yake ya Kibinadamu hata Sisi pia tunayo sana.
Mkuu pamoja na kumpima baada ya miaka mitano hii kauli yake unaichukuliaje?!

Mtu makini anaweza kujichanganya kiasi hicho?!
 
Back
Top Bottom