GWAJIBOY AKIMKARIBISHA JPM: Mheshimiwa Rais karibu sana jimbo la Kawe. Watu wa Kawe wamekusanyika hapa kwa wingi kukupongeza kwa kazi kubwa uliyowafanyia. Kwa miaka mitano ya uongozi wako umetatua kero ya muda mrefu ya maji maeneo mengi ya jimbo letu.
Umepeleka umeme kata nyingi, umejenga vyumba vya madarasa kwenye kata karibu zote, umetanua barabara ya Bagamoyo kutoka Morocco hadi Mwenge ili kupunguza msongamano, umejenga barabara nyingi za mitaa kwa kiwango cha lami na zinapitika muda wote. Mheshimiwa Rais tunakushukuru sana.