This is for you Ticha Jael...

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,379
Reaction score
41,294
Habari ya jumamosi wadau.

Niko bongo kwa kitambo tuu, leo mchana niliingia gereji kukagua toyo yangu iko poa kuingia kitaa? Sasa wakati nachokonoa mavitu kwenye boneti nikakwama mahali, nikahangaika weeh mwisho nikasema kwa nini nisimuulize Ticha wangu anikwamue huu umakenika?

Kweli nikamuendea hewani akanielekeza namna na mahali nigusanishe nyaya... Waaaraaa toyo ikawaka.

Nikafurahi nikampigia ticha kumshukuru, halafu nikaendeleza stori akaniambia Kasie unajua niko jikoni napika... Woow nikahamaki, ticha unapika nini? Akasema supageti za beef na veggies, Kasie baadae nna wageni napika akamalizia hivyo na kukata simu.

Daah akanipa wivu, nikaachana na mambo ya toyo nikaingia jikoni, kila kitu kitu kipo, nikatoka nje nikawaambia majirani wanne msipike leo naingia jikoni kwa ajili yenu. (Msiulize majirani wa kike au wa kiume).

Wapi nazi, wapi mazagazaga, wapi mchele... Taadaaa saa moja na nusu usiku msosi tayari. Nikapakua nikawaita jirani wale.... Wamefurahia mapishi ya chukuchuku...

Karibuni nanyi mle kwa macho.


Wali wa kusteam.


Njegere za nazi na mambogamboga (carrots, hoho, biringanya, nyanya chungu,viazi, bamia)


Papai..


Sahani yangu ina nyongeza ya magimbi na mihogo... Wali kidoogoo.

Namshukuru Maulana, majirani baada ya kushiba wakaosha vyombo sasa natupia vitu laini kulainisha koo...



Ticha Jael, asante kwa kunipa hamasa. Am happy for my Saturday. Cheers!!

Kasinde Platinum Matata.
 
Asante Kasie nimekula kwa macho wali unavutia
Ila sipendagi kabisaaaa mapapai na magimbi


Ooh karibuu na asante kuvutika na pishi la Kasie.

Pole kwa kutokula gimbi na papai, mie yamenikuza hayo ni matamu hatarii.

Nimekumbuka kipindi nasoma nikiwa likizo kwa shangazi, nilikuwa nakula futari ya magimbi hadi nikakifu.
 
Yes akiwa home aingie jikoni anavutia mno kimahaba.. unaweza kuanzisha tu jikon huko huko


Aahahahahhahaaa acha kabisa, Dadii akiwa anapika huwa namsumbua sana jikoni hadi anitulize kwanza na kamoja ndo anamalizia kupika, maana huwa situlii.

Mara namuendea, naomba nisaidie kufungua zipu imenishinda nimebanwa...
Mara, nasikia kiu ya madafu, twende tukayatafute...
Mara niimbe na kucheza cheza huku namtekenya... Basi vurugu tuu aahahahahaaa ghafla naona jiko linazimwa halafu shwaaap kamoja tuu, natuliaa na mapishi yanaendelea eeheheheheheheee.

Kasinde P Matata.
 
Kama ulidhani ntakuonea wivu, jaribu tena siku nyingine...

View attachment 1201167


Woow... Wooow Babuu, ujue kanywaji nnakokunywa kamenipa Mahaba tilalila.

Halafu kwa nini ombi langu unalipuuzia lakini au hadi nikuanzishie sredi?? aahahahahahaa.

Baharia mwenzio Daby aliripoti K' haijakuacha salama zaidi ya kukuacha mtaroni... Oooh sikumalizia alisema K' Vant aahahahahahaa sio K uliyoielewa wewe eeheheheheheheee

Naomba uukanushe huo udaku bin uvumi malabuku zako.

Ila nimekumiso mmuaah!!, sema SU nije...
 
Ooh karibuu na asante kuvutika na pishi la Kasie.

Pole kwa kutokula gimbi na papai, mie yamenikuza hayo ni matamu hatarii.

Nimekumbuka kipindi nasoma nikiwa likizo kwa shangazi, nilikuwa nakula futari ya magimbi hadi nikakifu.
Asanteee

Mie hayo magimbi nimejitahidi sana kula lakini yamenishinda...mapapai na machungwa nayo yashanipitia kushoto
 

Achana na Daby kijana mjinga sana huyo... K Vant ndo mpango mzima, hata bibi yenu kashahamiamo...


Kuhusu mambo yetu yale... nilikuita PM ukachomoa kunipa mawasiliano wakati maandalizi yalikuwa mukide...

 


Aahahahahahaaa Babuu, kilemba changu nilichokutumia ndo umempa bibi akifunge looh haya banaa acha afaidi na Vant yenuu.

Hebu ngoja kwanza, hiyo PM naomba ifowadi tena naona kuna mkono wa mtu, sijapata malabuku zako mwaka na nusu sasa hivi, laah uliituma kwa mchepuko wako ukafikiri imekuja kwangu.

Babu Hiyo bedi imeniamshaa.... hadi nimejiona nikiongoza kwa staili moja Matata.....

Fanya basii....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…