This is for you Ticha Jael...

This is for you Ticha Jael...

Aahahahahhahaaa acha kabisa, Dadii akiwa anapika huwa namsumbua sana jikoni hadi anitulize kwanza na kamoja ndo anamalizia kupika, maana huwa situlii.

Mara namuendea, naomba nisaidie kufungua zipu imenishinda nimebanwa...
Mara, nasikia kiu ya madafu, twende tukayatafute...
Mara niimbe na kucheza cheza huku namtekenya... Basi vurugu tuu aahahahahaaa ghafla naona jiko linazimwa halafu shwaaap kamoja tuu, natuliaa na mapishi yanaendelea eeheheheheheheee.

Kasinde P Matata.
Huyo "Dadii" huyoooo!

Hongera zake.
 
Habari ya jumamosi wadau.

Niko bongo kwa kitambo tuu, leo mchana niliingia gereji kukagua toyo yangu iko poa kuingia kitaa? Sasa wakati nachokonoa mavitu kwenye boneti nikakwama mahali, nikahangaika weeh mwisho nikasema kwa nini nisimuulize Ticha wangu anikwamue huu umakenika?

Kweli nikamuendea hewani akanielekeza namna na mahali nigusanishe nyaya... Waaaraaa toyo ikawaka.

Nikafurahi nikampigia ticha kumshukuru, halafu nikaendeleza stori akaniambia Kasie unajua niko jikoni napika... Woow nikahamaki, ticha unapika nini? Akasema supageti za beef na veggies, Kasie baadae nna wageni napika akamalizia hivyo na kukata simu.

Daah akanipa wivu, nikaachana na mambo ya toyo nikaingia jikoni, kila kitu kitu kipo, nikatoka nje nikawaambia majirani wanne msipike leo naingia jikoni kwa ajili yenu. (Msiulize majirani wa kike au wa kiume).

Wapi nazi, wapi mazagazaga, wapi mchele... Taadaaa saa moja na nusu usiku msosi tayari. Nikapakua nikawaita jirani wale.... Wamefurahia mapishi ya chukuchuku...

Karibuni nanyi mle kwa macho.

View attachment 1201115
Wali wa kusteam.

View attachment 1201117
Njegere za nazi na mambogamboga (carrots, hoho, biringanya, nyanya chungu,viazi, bamia)

View attachment 1201118
Papai..

View attachment 1201120
Sahani yangu ina nyongeza ya magimbi na mihogo... Wali kidoogoo.

Namshukuru Maulana, majirani baada ya kushiba wakaosha vyombo sasa natupia vitu laini kulainisha koo...

View attachment 1201126

Ticha Jael, asante kwa kunipa hamasa. Am happy for my Saturday. Cheers!!

Kasinde Platinum Matata.
Hahaha
 
Back
Top Bottom