This is for you Ticha Jael...

This is for you Ticha Jael...

Habari ya jumamosi wadau.

Niko bongo kwa kitambo tuu, leo mchana niliingia gereji kukagua toyo yangu iko poa kuingia kitaa? Sasa wakati nachokonoa mavitu kwenye boneti nikakwama mahali, nikahangaika weeh mwisho nikasema kwa nini nisimuulize Ticha wangu anikwamue huu umakenika?

Kweli nikamuendea hewani akanielekeza namna na mahali nigusanishe nyaya... Waaaraaa toyo ikawaka.

Nikafurahi nikampigia ticha kumshukuru, halafu nikaendeleza stori akaniambia Kasie unajua niko jikoni napika... Woow nikahamaki, ticha unapika nini? Akasema supageti za beef na veggies, Kasie baadae nna wageni napika akamalizia hivyo na kukata simu.

Daah akanipa wivu, nikaachana na mambo ya toyo nikaingia jikoni, kila kitu kitu kipo, nikatoka nje nikawaambia majirani wanne msipike leo naingia jikoni kwa ajili yenu. (Msiulize majirani wa kike au wa kiume).

Wapi nazi, wapi mazagazaga, wapi mchele... Taadaaa saa moja na nusu usiku msosi tayari. Nikapakua nikawaita jirani wale.... Wamefurahia mapishi ya chukuchuku...

Karibuni nanyi mle kwa macho.

View attachment 1201115
Wali wa kusteam.

View attachment 1201117
Njegere za nazi na mambogamboga (carrots, hoho, biringanya, nyanya chungu,viazi, bamia)

View attachment 1201118
Papai..

View attachment 1201120
Sahani yangu ina nyongeza ya magimbi na mihogo... Wali kidoogoo.

Namshukuru Maulana, majirani baada ya kushiba wakaosha vyombo sasa natupia vitu laini kulainisha koo...

View attachment 1201126

Ticha Jael, asante kwa kunipa hamasa. Am happy for my Saturday. Cheers!!

Kasinde Platinum Matata.
nasubiria harufu ya ush**z* wako sio kwa kupakia huko
 
Sio fresh kusema ukweli hadharani,siku nyingine sikukaribishi tena kuja kula kwangu eehehehhee.

Kweli bana wali napikaga kwenye rice cooker ndo maana nikasema wali wa kusteam. Una maji na chumvi tuu hauna mafuta.

Ila nikipika wali wa maua, yaani wenyewe carrots na njegere naukaanga kwenye sufuria na mwiko. Laah pilau pia nalikaranga pembeni na sufuria na mwiko mwanzo mwisho.
Sasa huo mwingine ndio wali mtamu, unajua mapishi yana asili na wali mtamu asili yake mashariki ya kati au bara hindi...

Huo wa kuvukisha ni mapishi ya far east kwa jamii za wachina...
 
Kenzy nashangaa quote yako sikuiona...
Mie sijambo buheri wa afya, karibu tubwie ugoro eeheheheeer.

Likijeba lipi hilo? lina mapengo ???
1568040949121.png
 
Saanaa (ila sio akiwa kazini aka Chief, sexy akiwa anapika nyumbani..) yaani hadi huwa naona aibu kwa jinsi Mahaba yanavonifunika.... heheheheheee.
Nna bahati ya kufahamiana na wanaume wajuzi wa mapishi sijui kwa nini....
Sean na mjeda wanakula kwa mama muuza
 
Saafii ndo matunda ya kuoa hayo, mara moja kwa mwaka nawe umsapraisi waifu umkarangizie walau mayai tuu.
Leo wakati natoka kukusanya mamilioni uraiani nimemletea mama yeyooo zawadi ya congo dust na kachori nne.
 
Sasa huo mwingine ndio wali mtamu, unajua mapishi yana asili na wali mtamu asili yake mashariki ya kati au bara hindi...

Huo wa kuvukisha ni mapishi ya far east kwa jamii za wachina...

Na wewe ni muasisi wa cheche chafuu??

Utanikarangizia one day?
 
Back
Top Bottom