This is for you Ticha Jael...

This is for you Ticha Jael...

Ugoro tena!! Bwia mwenyewe mi bado kijana barobaro handsome.. bado naangaika na Hawa vimwali wa sasa Si unajua vijana tuna mengi..
Hilo likijeba utakuwa umelisahau na limeacha kukusumbua Bibi yangu..

Eehehehehee ndo unikumbishe sasa hilo likijeba ni lipi??
 
Eehehehehee ndo unikumbishe sasa hilo likijeba ni lipi??
Bibi achana nalo tu ushalisahau.. lkn Leo nami nataka Kula pishi lako sijui utanipikia Nini wivu umenishika mi mjukuu wako wanakula jirani tu nami nataka..
 
Bibi achana nalo tu ushalisahau.. lkn Leo nami nataka Kula pishi lako sijui utanipikia Nini wivu umenishika mi mjukuu wako wanakula jirani tu nami nataka..

Pishi umepata,sema wataka kula nini, kwa sharti la kunikumbisha hilo jitu likijeba... ehehehe
 
Pishi umepata,sema wataka kula nini, kwa sharti la kunikumbisha hilo jitu likijeba... ehehehe
Ha ha! Bibie naona umedhamiria Kuna uzi wako fulani ulikuwa unalalama Kuna jitu linakusumbua ndo nikaamua kuliita kijeba mapengo has nothing to do with it.. Leta pishi
 
Ha ha! Bibie naona umedhamiria Kuna uzi wako fulani ulikuwa unalalama Kuna jitu linakusumbua ndo nikaamua kuliita kijeba mapengo has nothing to do with it.. Leta pishi

Mmhh sikubali, naenda soma nyuzi zangu zote hadi niupate huo wa jitu lililonisumbua...

Hujasema wataka kula nini....
 
Mmhh sikubali, naenda soma nyuzi zangu zote hadi niupate huo wa jitu lililonisumbua...

Hujasema wataka kula nini....
Utachopika ila kiwe amazing kuzidi Cha hao majirani just do it for kenzy sweet Bibi...
 
Utachopika ila kiwe amazing kuzidi Cha hao majirani just do it for kenzy sweet Bibi...

Aaahahahhaa shaka ondoa, ila inabidi iwe weekend maana weekday sipikagi sana.

Halahala tuu Dadii asikusikie eehehehehee.
 
Hata tukipika ugali na misumari?

Ebwana dagaa wa ziwa Victoria ila wawe wamevuliwa Bukoba, ni wale wale kama wa mwanza ila tofauti yake wanavyowaandaa....

Ukiwakarangiza na veggies (carrots, ho ho, biringanya, bamia, nyanya chungu) halafu na kaugali ka dona, yeeuwiii. Tumbo niachie nimbakishie manenge eehehehheee.

Na wewe unajua kupika?
 
Habari ya jumamosi wadau.

Niko bongo kwa kitambo tuu, leo mchana niliingia gereji kukagua toyo yangu iko poa kuingia kitaa? Sasa wakati nachokonoa mavitu kwenye boneti nikakwama mahali, nikahangaika weeh mwisho nikasema kwa nini nisimuulize Ticha wangu anikwamue huu umakenika?

Kweli nikamuendea hewani akanielekeza namna na mahali nigusanishe nyaya... Waaaraaa toyo ikawaka.

Nikafurahi nikampigia ticha kumshukuru, halafu nikaendeleza stori akaniambia Kasie unajua niko jikoni napika... Woow nikahamaki, ticha unapika nini? Akasema supageti za beef na veggies, Kasie baadae nna wageni napika akamalizia hivyo na kukata simu.

Daah akanipa wivu, nikaachana na mambo ya toyo nikaingia jikoni, kila kitu kitu kipo, nikatoka nje nikawaambia majirani wanne msipike leo naingia jikoni kwa ajili yenu. (Msiulize majirani wa kike au wa kiume).

Wapi nazi, wapi mazagazaga, wapi mchele... Taadaaa saa moja na nusu usiku msosi tayari. Nikapakua nikawaita jirani wale.... Wamefurahia mapishi ya chukuchuku...

Karibuni nanyi mle kwa macho.

View attachment 1201115
Wali wa kusteam.

View attachment 1201117
Njegere za nazi na mambogamboga (carrots, hoho, biringanya, nyanya chungu,viazi, bamia)

View attachment 1201118
Papai..

View attachment 1201120
Sahani yangu ina nyongeza ya magimbi na mihogo... Wali kidoogoo.

Namshukuru Maulana, majirani baada ya kushiba wakaosha vyombo sasa natupia vitu laini kulainisha koo...

View attachment 1201126

Ticha Jael, asante kwa kunipa hamasa. Am happy for my Saturday. Cheers!!

Kasinde Platinum Matata.
You got sexy finger nails😍😍
 
Ebwana dagaa wa ziwa Victoria ila wawe wamevuliwa Bukoba, ni wale wale kama wa mwanza ila tofauti yake wanavyowaandaa....

Ukiwakarangiza na veggies (carrots, ho ho, biringanya, bamia, nyanya chungu) halafu na kaugali ka dona, yeeuwiii. Tumbo niachie nimbakishie manenge eehehehheee.

Na wewe unajua kupika?
Hahah sina uhakika kama najua...

Halafu next time usipike wali kwa rice cooker kama huo hapo juu...
 
Hahah sina uhakika kama najua...

Halafu next time usipike wali kwa rice cooker kama huo hapo juu...

Sio fresh kusema ukweli hadharani,siku nyingine sikukaribishi tena kuja kula kwangu eehehehhee.

Kweli bana wali napikaga kwenye rice cooker ndo maana nikasema wali wa kusteam. Una maji na chumvi tuu hauna mafuta.

Ila nikipika wali wa maua, yaani wenyewe carrots na njegere naukaanga kwenye sufuria na mwiko. Laah pilau pia nalikaranga pembeni na sufuria na mwiko mwanzo mwisho.
 
Back
Top Bottom