Nataka mtambue kwamba Kenya ni nchi Hatari sana Afrika.
Kuna sababu ofisi nyingi kubwa za kimataifa zimepiga kambi Nairobi. Toka huko nyumba viongozi wa Kenya kuanzia Kenyatta walishirikiana vizuri na Marekani na Uingereza katika ubepari wa kuinyonya Afrika.
Ukiangalia historia, ndiyo maana hata Jaramogi Oginga Odinga alifarakanishwa na Kenyatta akajiuzulu umakamo wa rais na kuwa mpinzani. Mpaka leo tunaongea kama mpo makini, juzi tu Raila amepokonywa ushindi, walionyooshewa vidole kushiriki kwenye uchakachuaji ni Uingereza na Marekani. Kwanini, Raila anaegemea sana kwenye social welfare system kuliko capitalism, maana yake ni kwamba, uraisi wa Raila hauna tija kwa mataifa kama Marekani na Uingereza ila Ruto ni rahisi kumtia kibindoni.
Tizama ujumbe alioutuma Joe Biden kuhudhuria sherehe ya uapishaji wa Ruto, ulikuwa ujumbe mkubwa na muhimu sana, baada ya hapo, wakakutana na Ruto DC, na wiki hii tumeona ujumbe mwingine wa Marekani ikulu ya Kenya, baada ya hapo kilichofuata ni tangazo la Ruto kutoa zuio la GMO.
Tayari Ruto ametekwa na ni Hatari sana kwa maendeleo na mustakabali wa taifa la Kenya.
As things stand now, Ruto might be the most bogus president soon in Kenya in the recent times.