This is why all mama mean nothing to some people!

ila huwez jua jamani mama yenu alikua anateseka nn ucku mana mchana mulikua mwamuona anacheka na nyie tu ila ucku hujui alikua anapokea kichapo kiasi gani ............sema alikua anaficha sura ili asubui hata aweze kuangaliana na majirani
mm ni mwanamke believe me kuna kitu beyond that thing just take ur time think then go an talk to her
na kwann baba yenu haongelei mabaya ya mkewe wala nn ina mana anajua kilicho mtoa mkewe kwake believe or not kuna kitu nyuma ya pazia am tellin u
tena ktk hali hiyo na mama yako kutoroka baba akiwa kazini ina mana baba yako anauwezo so amma yenu hajakimbia shida (njaa) bali kakimbia mateso kutoka kwa baba yako
tena umenipa uchungu mnoooooo unavosema haumfeel mama yako .......kwanza mungu akusamehe mana hujui ulitendalo na pili usiingilie magomvi ya watu wazima ww hata cku moja so talk to ur momy tena haraka iwezekanavyo na umsihi kama mwanao akueleze kilichomsibu believe me akikuambia waweza hata utamani kulifukua kaburi la babako na kumtia mboko kwa kwenda kia,
mwisho naomba roho mtakatifu akuongoze mana kwa akili zako nilivokusoma huwezi kumface maza ako so u need help from our almighty GOD na kama ww ni muislamu basi rehema na mtume wetu(s.a.w) ikawe nawe wakati wamfata maza ako ok
ameeeeeeeeeeen
 
Wanaojitokeza kutelekezwa na mama ni wengi kwenye thread hii, ikimaaniasha tatizo ni kubwa kuliko tulivyokuwa tukifikiri

Poleni nyote mlotelekezwa na ama mama au baba.
 

Hapa ni kweli kwamba baba huwa ndo wanaooa lakini si kukimbia familia
na ndiomaana imekua vigumu kwa huyu mtoa mada kuamini kilichotokea
baba akioa huwa anaendelea na majukumu kama kawaida lakini mama
huwaacha watoto wake na kukimbia moja kwa moja kwa kifupi anayejua
mtoto ni wa nani ni mama na mara zote mwanamke hasingiziwi mtoto
kwani yeye ndo anazaa ila mwanaume anaweza singiziwa ndo maana
wanaume wanaweza kukimbia
 
Flovans,usijali nimeshamsamehe nae pia anahitaji msaada wangu,mimi kama kijana wa kiume nakua ananihitaji sana,pole kwa yaliyokukuta!
 
AMINATA,nina uhakika life ilikua positive na kulikuwa hakuna shida,hatakama mfano ingekuwepo,hakutakiwa afanye aliyoyafanya!
 
ww nawe kama ni mwanamke kweli na umesoma na ulishawai kuingia ktk mahusiano huwezi kumchukia mama yako hata cku moja
nakuambia hakuna watu wanaroho mbaya hapa duniani kama wanaume am tellin u
ndoa nyingi zimeficha maovu sana na wanawake wengi wanavumilia koz ya watoto tu basi ila kuhusu wao kupata raha ktk 100 labda 2% ndio wanafuraha sana ktk ndoa zao............hawa watu ni wagomvi sana na cjui hua wanawaza mwanamke ni kitu gani kwao i dont know kwakweli
na pili mama yako atakua anakuchukia kutokana na mambo baba yako aliyomtendea so akikuona ww anapata hasira bado juu ya baba yako na atakua alimueleza huyo baba yako wa kambo dats y huyo baba hakukutesa ww koz alikua naelewa mkewe anakutreat ivo kutokana na pain alizopata kwa baba yako mzazi
pengine alipoibeba iyo mimba alifukuzwa na baba ko na akaolewa mwingine brand new
ila mm ninachokushauri usijudge chochote kuhusu mama yako kabla hujamuuliza why
mi nashangaa kweli kwann usimuulize na ni mama yako ..........mulize umepitia nn mama mpaka wanichukia ivi au kama ukimuuliza ww waweza kumtia hasira sana basi tumia hata nyanyako au shangazi amuulize mama ili ujue ukweli na ukisha ujua ndio utajua jinsi ya kumsaidia jinsi ya kuepukana na machungu aliyonayo
ngoja niachie hapa nisije lia bure mana i love my mama kupitiliza koz najua kuna mambo mengi anayavumilia ila hasemi na she still there 4 us...........[video=youtube_share;DBrZ06tU91g]http://youtu.be/DBrZ06tU91g[/video]
 
Uko sawa harakati,wakati mwingine ni vigumu kuamini mtu anakubeba miezi tisa halafu anakutelekeza!
 
Flovans,usijali nimeshamsamehe nae pia anahitaji msaada wangu,mimi kama kijana wa kiume nakua ananihitaji sana,pole kwa yaliyokukuta!
mulize basi usimuwazie tu mabaya uliza kwann watz hamuwezi kuhoji munapenda kulalama tu..........mi cpendi watu wa ivi bwana ala.........
mulize basi mamako kwanza kabla ya kulalama namna hiyo loh
 
AMINATA,ni bora ukatili wa baba kuliko wa mama,asikwambie mtu,usikie kwa jirani tu,mama ndo anakua muda mwingi na watoto,hebu fikiria anapokuwa mkatili inakuaje?Au anakimbia!
 
Thanx Gaijin at least dunia italiangalia jambo hili kwamtazamo mwingine na kutoka kwenye mazoea ya kijinga!
 
siku yangu ya leo imeharibika ghafla baada ya kusoma hii thread,nimeumia sana kwani nami yamenikuta,tangu nilipozaliwa sijawahi kumuona baba na nimepitia ktk shida nyingi nikiwa na mama yangu mpenzi(nampenda sana),mwaka 2003 nikamuuliza mama kuhusu baba ila mama alilia sana ikanisababisha nami kulia mno na nikaapa sitauliza tena kuhusu baba wala sitahitaji kuonana nae maishani mwangu,mwaka 2006 alipiga simu kwa dada yangu akiniomba kuonana nami wkt nikiwa mwaka wa 2 chuo,nilitoa onyo kali kwa yoyote ndg yangu atakayesababisha mimi na yeye huyo anayeitwa baba kuonana.Sina mapenzi yoyote na huyo na huwa ni vigumu sana kutamka neno baba,hata gf wangu wkt mwingine huwa namuita mama kwa jinsi ninavyowaheshimu wanawake.
wana mmu jitahidi kutofanya kosa km hili ktk maisha yako yote.
wengi huanza kushauri eti samehe lkn ni ngumu na akina baba tumezidi kusababisha haya matatizo.
HAKUNA KM MAMA INGAWA WACHACHE WANASALITI ASILI YAO YA UPENDO
 
Pole sana,am very sensitive na story zinazohusu watoto(malaika wa Mungu wasiokua na makosa). Nakubaliana na mitazamo tofauti ya watu sababu kila mtu kapitia vitu tofauti wengine wamekimbiwa na baba wengine mama.
Ila MAMA anaekimbia watoto wake aiseee huyo ana uwalakini kichwani kwake hata kama alilazimishwa kuingia kwenye ndoa na kuzaa bila mapenzi yake bado haiwezi ku justify kukimbia watoto wako uliowazaa jamaniii.....kama unaona kuna mambo umeshindwa kuyavumilia kabisa kwa huyo mzazi mwenzio basi beba wanao ondoka nao lakini sio kuwatelekeza ili nani akulelee wanao?????mama wa kambo loooh hapana aiseee,asante. Mimi nina amini ile kubeba mimba miezi tisa tayari unakua umeshatengeneza bond kati yako na mtoto it gives you a sense of responsibility and when the baby is born that increases the feeling that the baby actually exists. Mateso yote uliyopata ukiwa mjamzito mpaka unajifungua salama mtoto anafikisha miaka 2(mfano)yani kanatembea halafu unamkimbia??????!!!!!!! Kuna wanawake wana roho ngumuuuuuuuu.....ndio maana siku zote huwa nasema wanawake ni wauaji ila wanaume ni wanyama. Ukikuta mwanamke ana roho mbaya utatamani sakafu ifunguke uingie loooh......

Eiyer nisamehe ila mama yako ni mmoja kati ya wanawake wenye roho ngumu!!! Msamehe bure,endelea na maisha yako mpe heshima yake kama mama lakini huwezi kuwa na mapenzi nae itakua ni unafiki. We all must know this....what makes you a woman/man is not the ability to have a child but the courage to raise one.
 
AMINATA,iwe sababu iwayo.Still hakutakiwa aache hata kutusalimia achilia mbali kutukimbia!How can u trying to find an excuse!!
 
Mama Tuli i real like u!Nimependa sana msisitizo kwenye ujumbe wako,Mungu akubariki na familia yako,duh!
 
mulize basi usimuwazie tu mabaya uliza kwann watz hamuwezi kuhoji munapenda kulalama tu..........mi cpendi watu wa ivi bwana ala.........
mulize basi mamako kwanza kabla ya kulalama namna hiyo loh


Wewe mshukuru Mungu kwa kuwa hujapitia waliyopitia wenzako kwahiyo mtu akitoa dukuduku lake usiseme analalama.......hujui machungu yake ni bora ukae kimya. Amuulize ili iweje????je akimjibu baba yako alikua muuaji ikabidi nimkimbie ndio itakua inamsaidia nn Eiyer kwa sasa???!!!maana baba ameshafariki anaweza kusingiziwa chochote marehemu wa watu. Tatizo letu wanawake always tunapenda kuonewa huruma wakati ni wanafiki tu.
 


Thats why I have forgiven her
But utamu wa ngoma uingie ucheze.....Thus kama yangekukuta lazima ungesikia uchungu wake.
Inauma sana unapokuwa shule marafiki zako wanasimliana mama oooh,mama that wakati wewe wala hujui hata kionjo cha huo upendo wanaosimlia wenzio.
Unaona sherehe za wadogo zako mama anachakalika kuweka mabo safi lakini yakwako anakuwa kama hayupo,dont talk that way coz hujaexperience AMINATA
For sure nilimpenda sana Baba yangu wa kambo(RIP daddy) kuliko my mom,Atleast yeye wakatimwingine alikuwa anatambua kuwa kimbe kama mimi niko ndani ya nyumba hiyo.
 
Mama Tuli i real like u!Nimependa sana msisitizo kwenye ujumbe wako,Mungu akubariki na familia yako,duh!

Ameeen,asante na wewe Mwenyezi Mungu azidi kukutia nguvu na umuombe avunje hiyo roho ya kukimbia watoto maana haya mambo bwana hukawii kurithi aisee. Sali sana wangu.
 
Flovans uko sahihi,mimi ninapomuona mtu anafurahi na mama yake huwa napata uchungu na mawazo mengi sana hakuna atakaeziba hilo pengo,labda nitakapo oa mke wangu anisaidie kujua upendo huo!
 
Mama Tuli,usijali siwezi kurithi ujinga na ukatili,i will prove to the world how great i will be to my kids!
 
kweli mama ni mama,lakini tujiulize kama kweli huyo mama hakuwa na tatizo kwa nini hakutaka kuwatembelea wanae hadi alipolazimishwa na marehemu mumewe ndo akafanya hvyo,inavyoonekana mumewe hakuwa na shida na mkewe na ndo maana alimwomba awe anakuja kuwatembelea watoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…