Hehehe mambo bado !!!
HATUA ya mbunge wa Mbita Bi Millie Odhiambo 'kutoa mabango' ya matusi kwa Rais Uhuru Kenyatta Jumanne imeibua hisia kali miongoni mwa wanawake wanaounga mrengo wa Jubilee mkono.
Katika taarifa ya habari kutoka mshirikishi wa maendeleo ya wanawake katika kaunti ndogo ya Pangani Bi Eddah Gitau, wamemtaka mwakilishi wa wanawake wa Nairobi Bi Rachel Shebesh kumkabili Bi Odhiambo kwa ukali sawa na matusi yake kwa rais.
“Wapi Bi Shebesh katika kizaazaa hiki? Anafaa kuwa amemcharura Bi Millie Odhiambo. Hata wale warefu ajabu sisi huwapanda kwa ngazi!” akateta.
Alisema kuwa Bi Odhiambo alidhihirisha kuwa “kusoma kwingi sio mwisho wa ujinga” kwa kuwa “Bi Odhiambo licha ya kuwa huongea Kizungu na kuonekana kuwa aliyepevuka macho, maneno ya msukumo wa Bongo lake yako na eti eti katika darubini ya ulainifu wa kimawazo.”
Bi Gitau aliteta kuwa “sio mara ya kwanza Bi Odhiambo ameonyesha madharau ya wazi kwa rais”,
akirejelea kikao cha ufunguzi wa bunge mwaka wa 2016 “ambapo rais akihutubia bunge hilo la pamoja na Seneti, Bi Odhiambo alikuwa akijipondoa hadharani akiangaziwa na kamera za vyombo vya habari.”
Alimtaka Bi Odhiambo aelewe kuwa
“heshima sio utumwa” na ikiwa “unatarajia nasi kama wanawake wa Jubilee tumtukane kinara wenu Bw Raila Odinga ili tuonekane weledi wa matusi, pole, hatujafikisha ujinga hapo.”
Nusu mkate
Alimkumbusha Bi Odhiambo kuwa “hata wakati huyo Odinga wenu alikuwa amegaiwa nusu mkate katika serikali ya muungano wa kitaifa chini ya Rais Mwai Kibaki, hakuna hata wakati mmoja sisi wanawake wa kutoka Mlima Kenya tulipatikana popote tukimtukana.”
Alimtaka Bi Odhiambo aelewe kuwa “wewe kama kiongozi unategemewa pakubwa kutoa mifano ya kuigwa na watoto wetu wasichana na ikiwa hizo ndizo tabia zako, basi wakikuiga watajipata katika kila hatari ya kimaisha na hata kutupwa jela kupitia tabia za kijambazi