Nabii kibonge
JF-Expert Member
- Mar 15, 2018
- 277
- 310
Kiufupi mimi ni mfuatiliaji wa ligi mbalimbali tofauti na wadau wengi ambao kwao EPL ndio ligi. Na huwa wanazi-refer hizi ligi nyingine kama ligi za wakulima na hazina ushindani na sishangai wakisema hivyo.
Watakwambia hizo ligi hazina wachezaji wa kutisha na wenye changamoto lakini mda huo huo utasikia wanamsifia mchezaji kama Lingard, hao hao watakwambia Trent Alexander anatisha kuliko Cafu, watakwambia ndiye beki bora wapembeni duniani kwa sasa. Achana na hayo.
Thomas Muller, wajerumani wanamwita Raumdeuter huku wakimaanisha 'space intepreter' jina ambalo linatokana na uchezaji wake. Sio mtu wa kudrible sana kama unavyomwona Neymar, pia sio mtu anayehitaji akuonyeshe skills kama Marseile Turn ndio ujue ni hatari, lakini uwezo wake mkubwa wa kuusoma mchezo na good positioning ndio silaha kubwa ya mwanajeshi huyu wa Kijerumani
Kiufupi tu Thomas Muller akiwa na miaka 20 tu alimaliza na goli 5 world cup 2010. 2014 akamaliza na goli 5 tena. Nilikuwa natarajia angevunja record ya Miroslav Klose na kumpiku Ronaldo de Lima kwa magoli mengi ya World cup lakini imeshindikana 2018 na kwa hili namlaumu 100% Pep Guardiola
Siku zote katika kutafuta mrithi wa kocha aliyedumu kwa kipindi huku akiwa na mafanikio huwa ni shida kidogo, rejea hata David Moyes baada ya kibabu Fegi. Bayern waliingia kwenye dimbwi hilo hilo ni wazi Pep alikuwa anashinda mechi nyingi na winning rate kubwa tu maana alishinda mechi 22 katika 27 za mwanzo ila bila kuficha Pep alikuwa anaharibu soka natural la wajerumani
Tactics za Pep zinahusisha pasi nyingi na ndio maana alivyotua Bayern akaanza kuwanufaisha viungo wake kina Thiago Alcantara. Ni wazi soka la kijerumani la piga nikupe zile counter attacks, soka la kumfanya mpinzani mda wote awe na mashaka chini ya collabo ya Robben na Ribery lilipotea na hapo ndipo kiwango cha Thomas Muller kilianza kudorora na si Muller pekee, wapo wachezaji wengi tu
Kiujumla Thomas Muller ametwaa Uefa champions League, ametwaa World cup na ubingwa wa Bundesliga mara 9 na amehusika katika kutengeneza magoli 141 huku akifunga 162 kwa ngazi ya club na kwa national team kahusika kutengeneza mabao 54 katika timu ya taifa.
Kilichonisikitiaha zaidi ni kushuka kwa kiwango cha mchezaji huyu hadi kuhusishwa na kuondoka katika kalbu hiyo. Lakini ujio wa kocha Hans Flick ambaye ninaamini ndiye mrithi wa Jupp Hynckess, Thomas Muller amerudi kwenye ubora wake na sasa ndiye Raumdeuter wa kweli
Msimu huu tu Thomas Muller ametoa assist 21 na kufunga mabao 8 huku akichangia zaidi ya 30+% ya magoli ya Lewandowiski aliyemaliza na mabao 31 bado Thomas Muller atakuoffer vitu mbali mbali ikiwemo defending kutokana na uwezo kwa kupora mipira akiwa eneo la mbele nadhani hata KDB hagusi hapa ila KDB anachomzidi muller ni uwezo wa kUtengeneza nafasi nyingi na kufunga magoli mengi lakin Thomas Muller ni mzuri katika kudefend pia.
Katika mafanikio ya sasa ya Bayern ni wazi utakuwa mchawi usipomtaja Thomas Muller lakini yote haya hayaonekani. Bayern anaonnekana tu Lewandowski na Gnabry huku wakisahau mtu wa muhimu Thomas Muller.
Ni wazi chini ya Hans Flick ambaye ameshinda mechi 27 kati ya 29 za mwanzo timu imeimarika na sasa naiona Bayern mpya inarudi chini ya usimamizi wa mwamba Oliver Khan
Bahati mbaya kwako Muller unacheza mpira katika zama za mpira ambazo watu wanaabudu maneno na ushabiki tu kwani anayeonekana anacheza mpira ni Bruno Fernandes, Greenwod, Alexander Anold na wajinga wenzao kina Dele Ali lakini Ujerumani wala Italia hamna mpira. Naamini hata Zlatan ambaye ameenda AC Milan dirisha dogo na katika mechi 18 ana magoli 10 na assist 6 huku akiwa ameanza mechi 16 tu ingekuwa England wangempa na uchezaji bora kabisa wa ligi.