THRDC: Mchakato wa haki ulianza kuvurugwa tangu Tundu Lissu alipokamatwa

THRDC: Mchakato wa haki ulianza kuvurugwa tangu Tundu Lissu alipokamatwa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeeleza kubaini kasoro na changamoto mbalimbali za kisheria zilizojitokeza wakati wa kukamatwa, kufikishwa mahakamani na kuwekwa mahabusu kwa kiongozi wa chama cha upinzani, Tundu Lissu.

Akiwasilisha taarifa ya ufuatiliaji wa shauri hilo, Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, amefafanua kuwa taratibu za kisheria hazikuzingatiwa tangu hatua ya ukamataji, kwani kiongozi huyo alipaswa kupewa wito rasmi badala ya kukamatwa katikati ya mkutano wake. THRDC imesisitiza kuwa ukiukwaji huo wa taratibu uliathiri mchakato mzima wa utoaji haki unaopaswa kuendeshwa kwa uwazi.

Hali kadhalika, mtandao huo umekosoa vizuizi vilivyowekwa kwa wananchi, wafuasi, viongozi na mawakili waliotaka kufuatilia shauri hilo mahakamani. THRDC imekumbusha kuwa mashauri ya viongozi wa umma ni masuala ya wazi yanayotakiwa kuendeshwa kwa uhuru ili kuruhusu wananchi kushuhudia utendaji wa mhimili wa mahakama.

 
Back
Top Bottom