Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) umeishauri CHADEMA kutafuta suluhu ya kudumu ya changamoto zao ikiwemo shauri la mwenyekiti wake, Tundu Lissu, kwa njia ya mazungumzo yenye maslahi mapana kwa umma.
Aidha, THRDC imewashauri wanasiasa wote kwenda kwenye meza ya mazungumzo kwa ajili ya kutatua changamoto zilizo kwa njia ya majadiliano.