THRDC Walaani mwandishi wa Watetezi TV kukamatwa na kupigwa akiwa kazini

THRDC Walaani mwandishi wa Watetezi TV kukamatwa na kupigwa akiwa kazini

Makumbele

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2009
Posts
312
Reaction score
1,433
IMG_8729.jpeg


Mwandishi wa Habari wa Kituo Cha Watetezi TV, kinachorusha matukio ya ukiukwaji wa Haki za Binadamu na kinachomilikiwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) Ndugu JAHA Harith, Aliyechukuliwa tarehe 31/10/2025 na askari waliovalia kijeshi wakatiwa maandamano amepatikana ametupwa Kibaha akiwa hoi baada ya kupigwa na kupokonywa vifaa vya waandishi (Kamera na simu).

Alikamatwa wakati anatimiza Majukumu yake ya Kiuandishi ya kufuatilia watu waliopoteza na kujeruhiwa wakati wa maandamano Jijjini Dar es Salama. Askari hao walichukua vifaa vyake vya kiuandishi na Mawasiliano, hali ambayo ilizua sintofahamu ya mahali alipopelekwa.

Leo tarehe 1/11/2025, majira ya jioni alifanikiwa kurudi nyumbani na kueleza kuwa alipigwa sana na kutelekekezwa kibaha Pwani. Ameeleza kuwa walikuwa wanamuuliza kwanini unafuatilia na kurekodi matukio wakati wa maandamano. Wamechukua vifaa vyote vya kazi za mwandishi na kuondoka nazo.

THRDC inakemea Vikali Kitendo hicho Cha Kukamatwa mwandishi huyu, kupigwa, kutishiwa uhai pamoja na kunyan’ganywa vifaa vyake vya kazi.

Tunatoa wito kwa Mkuu wa Polisi na Jeshi kuhakikisha vifaa vya mwandishi huyu vinapatikana na askari waliohusika wawajibishwe kwa kuwa ni kosa kumzuia mwandishi aliyekuwa anatimiza wajibu wake wakati wa maandamano. Itambuliwe kwamba waandishi wa habari wana haki ya kufanya kazi popote pale penye matukio yanayohusu jamii.

Tunasikitika sana kuona wandishi wengi wamezuiwa kufanya kazi zao wakati huu. Askari wote wanapaswa kuheshimu muda wote haki za waandishi wa habari na sio kuwakamata na kuwapiga wakati wanatimiza wajibu wao.

THRDC- 1/11/2025

IMG_8730.jpeg
 
Ata mimi nilikamatwa ila sema mimi mtu mzito wakanambia factory reset simu nzima daaah
 
Back
Top Bottom