THRDC yalaani madai kukamatwa viongozi Chadema ,waandishi wa habari

THRDC yalaani madai kukamatwa viongozi Chadema ,waandishi wa habari

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274
Snapinsta.app_454973538_468406426083191_5413459697461362077_n_1080.jpg

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), umeungana na wadau wengine kulaani madai ya kukamatwa kwa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wanahabari wakielekea katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani jijini Mbeya.

THRDC imetoa tamko hilo leo Jumatatu, Agosti 12, 2024, ikidai takribani watu 300 wamekamatwa na Jeshi la Polisi, akiwemo Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, Tundu Lissu, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu.

Wengine wanaodaiwa kukamatwa ni Wakili Deogratias Mahinyila na waandishi wa habari wa Jambo Tv ambao ni Ramadhan Khamis na Fadhil Kirundwa. Pia wamo viongozi wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Twaha Mwaipaya, Moza Ally, Deusdedith Soka na wengine
 
Back
Top Bottom