Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
TAMKO KULAANI KUKAMATWA KWA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA
Dar es Salaam, Tanzania - Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) unalaani vikali vitendo vya kukamatwa kwa waandishi wa habari mbalimbali nchini, hasa siku za hivi karibuni. Tukio la hivi punde ni kukamatwa kwa mwandishi wa habari Constatine Mathias wa Uhuru Media mkoani Simiyu. Constatine alikamatwa usiku wa kuamkia leo, Juni 18, 2024, na polisi walikagua nyumbani kwake wakachukua vifaa vyake vya kazi ikiwemo simu na laptop yake. Hadi sasa, polisi hawajaweka wazi ni wapi wanamshikilia mwandishi huyo na tuhuma zipi zinamkabili, ingawa inasemekana amesafirishwa kwenda mkoani Mwanza.
Mnamo Juni 13, 2024, mwandishi wa habari na mmiliki wa Dima Online TV, Dinna Maningo, alikamatwa nyumbani kwake Tarime mkoani Mara na kusafirishwa hadi mkoani Mwanza kwa tuhuma za kutumia nyaraka za siri za Jeshi la Polisi kuhusu kesi inayomhusu aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Yahaya Nawanda, anayedaiwa kumlawiti binti wa miaka 21 mnamo Juni 2, 2024, katika eneo la baa ya the Cask, viwanja vya jengo la Rock City Mall. Hadi leo, Dinna bado anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza bila ya kupewa dhamana, kinyume cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
Tarehe 16 Juni 2024, mwandishi wa habari ambaye pia ni Naibu Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri, Manyerere Jackton, alikamatwa na kushikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro kwa zaidi ya saa mbili na nusu kwa tuhuma za kupiga picha lori lililopinduka. Manyerere alipiga picha tukio hilo akiwa safarini eneo la mji wa Same, ambapo lori lililobeba mafuta ya kula lilipinduka na wananchi walikuwa wakichota mafuta hayo. Polisi walimkamata, wakachukua simu yake na kufuta kila alichorekodi. Manyerere aliachiwa baadaye kwa amri ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Simon Maigwa.
Kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, waandishi wa habari wana haki na uhuru wa kukusanya taarifa na kuuhabarisha umma. THRDC inasisitiza kuwa ni kinyume cha katiba na sheria za nchi kuwakamata waandishi wa habari wakiwa wanatekeleza majukumu yao.
### Hatua Zilizochukuliwa na Mtandao
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania umetoa maelekezo kwa wakili Amri Linus aliyepo mkoani Mwanza kushughulikia kesi za waandishi wote wawili waliokamatwa mkoani Mwanza. Hata hivyo, dhamana haijaweza kupatikana kwa mwandishi Dinna Maningo hivyo asubuhi ya leo wakili Linus amefungua kesi Mahakama Kuu masijala ya Mwanza dhidi ya Jeshi la Polisi mkoani Mwanza ili kudai dhamana ya mwandishi huyo.
### Wito wa THRDC
1. THRDC inatoa wito kwa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kuwaachia mara moja waandishi wa habari Dinna Maningo na Constatine Mathias kwani wao ni watoa taarifa tu ambazo Polisi wanapaswa kuzifanyia kazi na sio kuwakamata na kuwaweka kizuizini kinyume cha Sheria.
2. THRDC inatoa wito kwa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kuwarudishia waandishi wa habari vifaa vyao vya kufanyia kazi ili kuhakikisha kwamba wasiingie gharama ya kununua vifaa vingine. Hii itawasaidia waandishi hao pia kuendelea kufanya kazi ya kuipasha habari jamii.
3. THRDC inatoa wito kwa Jeshi la Polisi kufanya upelelezi kwa kuzingatia Sheria na Amri Kuu za Jeshi la Polisi (PGO) ili kuhakikisha kwamba haki za waandishi wa habari hazikiukwi kwa makusudi.
Imetolewa na,
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),
Juni 18, 2024