Thread niliyoiweka humu JF miaka mitatu iliyopita imeshughulikiwa! Namshukuru Rais Samia, na tuendelee kusema kupitia JF, tunasikilizwa!

Thread niliyoiweka humu JF miaka mitatu iliyopita imeshughulikiwa! Namshukuru Rais Samia, na tuendelee kusema kupitia JF, tunasikilizwa!

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Miaka mitatu iliyopita, niliweka thread humu JF na kuainisha wazi kabisa jinsi serikali ilivyokuwa ikiwanvunjia Watanzania haki zao za binadamu. Leo hii nina furaha sana kuona hili limesikilizwa! Wakati huo tulikuwa chini nya Raisi Magufuli, lakini niliona kuna haja ya kumweleza ukweli kutokana na uonevu uiliokuwapo.
Asante sana mama Samia. Tuendelee kuijenga nchi yetu

Kwa hiyo siku hizi polisi na mahakama wanatimiza wajibu wao kwa 100%, kwa kutowaweka watu hovyo lock up baada ya kutoa haya malalamiko yako humu jukwaani!
Kutakuwa na matatizo katika utekelezaji wa hii sheria mpya, kama tunavyowajua Polisi wetu. Lakini sasa tuna msingi wa kupambana nao, maana mtafrisiri sheria ni Mahakama sio polisi

Siku haimaliziki bila kutajwa jina la marehemu,

Ukiona unashinda na mtu alikufa alafu anakushinda Basi ujue unapambana na spirit tofauti ambayo siyo yeye
 
Kwa hiyo siku hizi polisi na mahakama wanatimiza wajibu wao kwa 100%, kwa kutowaweka watu hovyo lock up baada ya kutoa haya malalamiko yako humu jukwaani!
Bado wanaua panya road na kujitapa hadharani bila kuwafikisha mahakamani.

Anaongelea HAKI za binadamu zipi?
 
Bado wanaua panya road na kujitapa hadharani bila kuwafikisha mahakamani.

Anaongelea HAKI za binadamu zipi?
Nadhani unaleta suala la msingi sana, kwamba sheria hii inaweza kuwa kichocheo cha polisi kujichukulia hatua mikononi wakijua hawawezi kukuweka ndani kama hawana ushahidi. Kwa hiyo wanaamua wakupotezee yaishe.
 
Miaka mitatu iliyopita, niliweka thread humu JF na kuainisha wazi kabisa jinsi serikali ilivyokuwa ikiwanvunjia Watanzania haki zao za binadamu. Leo hii nina furaha sana kuona hili limesikilizwa! Wakati huo tulikuwa chini nya Raisi Magufuli, lakini niliona kuna haja ya kumweleza ukweli kutokana na uonevu uiliokuwapo.
Asante sana mama Samia. Tuendelee kuijenga nchi yetu

Rais Samia Suluhu aliahidi kulinda haki ya mwananchi na nchi pia na sasa amefanikiwa
mwisho siku 90 kufanya uchunguzi wa kesi ni jambo jema sana aisee maana zamani ilikua inakaa hata miaka mi 3
 
Kwa hiyo siku hizi polisi na mahakama wanatimiza wajibu wao kwa 100%, kwa kutowaweka watu hovyo lock up baada ya kutoa haya malalamiko yako humu jukwaani!
Big up kwa mama Samia.
Anapitia humu JF na kuona yale yanayofanywa na watendaji wa serikali yake.
Zamani ulikuwa ukisikia wakuu wa vitengo na hata polisi wakisema , hatushughulikii mambo ya mitandao.
Sasa hata wao wanasoma na kushughulika, Big Up Mama Samia.
 
Mbona hata sielewi...

Huyu huyu ambaye bado amepiga marufuku mikutano ya kisiasa kama Katiba inavyotaka au mwingine?

Huyu huyu anayewataka viongozi aliowateua kula kwa urefu wa kamba zao au mwingine?

Huyu huyu anayeruhusu wananchi tuibiwe hela zetu tulizozitolea jasho na akiba zetu kupitia tozo au mwingine?

Yaani anayechagua kati ya haki na haki ipi ni haki zaidi...hapana, bado sana.
 
Back
Top Bottom