Thread ya Show ya "I am Zuchu": Kutoa Tsh. million 5 kumuona Zuchu kwenye VVIP inaitaji uwe na utajiri wa Bakhresa

Alafu nilimsahau huyu mwamba dula makabila aisee jamaa aliua Sana ila aliyopiga inaitwa classic singeli wakati alivyoitwa kupanda stage nikajiuliza singeli na tukio la event jamaa atafanya Nini? lakini the end of the day amenishangaza Sana.
Combination ya Jide na Zuchu ilinitoa machozi.. Jide kakutana na mashetani wengi mnoo.. Lakni bado anasimama..

Hail to the Queen...
 
Acha wivu ruby wakati wake ushapita hata kama humpendi kubali uwepo wake nw japo waumia
 
Hebu angalia mawazo ya watu hapa wengi wanasemaje kuhusu perfomance ya zuchu,wewe umekuja kusifia na watu wanatoa maoni,sasa ulileta uzi wa nini kama kama kukosoa ni chuki
Mzee baba Hili jukwaa tunajuana Sana so usijifiche kwenye Hilo chaka wewe sio tu una chuki dhidi ya Zuchu Bali unachuki na Wasafi kwa ujumla Nani asiyekujua
 
Kwaio ngoja kwanza hii show ilikia ya zuchu ama wcb pili.. kama ni ya zuchu yy amefunika au amefunikwa

Mm naona tudeal na hayo tu hayo mengine siku nyingine
 
Kabisa Jide was much better kuliko huyu Zuchu. Ndo maana wasafi walikuwa wanasita kumsainisha kwa miaka minne. Believe me asingekuwa mtoto wa Khadija Kopa asingesainishwa pale WBC.Frankly speaking kuwa mtoto wa Khadija Kopa ndo kumemfanya ainginzwe WBC
 
Dada watu yupo vizuri sema wivu wako binafsi ndio unaokusumbua.
 
Kwa hiyo mleta unataka kusema show nzima haikuwa na kasoro au mapungufu? Yaani mada yako nzima ni kusifia na kupongeza tu, wakati watu wengi wanasema wameona mapungufu kibao.

Japokuwa mimi sio mpenzi wa mziki wa bongo flavour kabisa lakini by default nimejikuta nawajua wasanii wengi wa Bongo flavour. Na kiukweli kabisa Zuchi mpaka sasa simjua kabisa. Hivyo nahisi huyo binti huenda atakuwa overrated au underground fulani.
 
Tatizo linaanzia kwako team kiba...nyuzi zako mbona zipo wazi kbisa..[emoji3][emoji3]
Huyo sio team Kiba maana pia anampondaga Sana kiba I think ana upande lakini sijui Ni upi?
 
Wewe tena tokea lini ushawahi isifia WCB,mara walikuwa wanampa harmonize hela ndogo,mara Mondi mchawi,mara Babutale kamtoa kafara mkewe (mtazani mlikuwa wote kilingeni),leo tena kwa Zuchu.Tatizo unaongozwa na chuki so huwezi ona zuri lolote upande wa WCB.

Alafu unaonekana una undugu na Robidinyo hamtofautiani,ila hata ukiponda haumpunguzii kitu.

Ila ninacho wakubali haters huwaga wa kwanza kutizama events za WCB,sio mbaya umeongeza traffic.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…